Nimeamua kuachana na CHADEMA na kurudi CCM

Nimeamua kuachana na CHADEMA na kurudi CCM

Umeachana!? Kwani CHADEMA ilikuoa lini mwenzetu!? Mbona ilipokuoa haukututangazia kwamba umeuaga ukapela!?
 
Chama hiki kimekuwa hakina shukrani kabisa nchi hii na wala uzalendo kwa taifa ndio maana katibu mkuu mzee Slaa anaiunga mkono Rwanda

Kila kizuri cha Kikwete au CCM lazima CHADEMA wakitie kasoro,chama cha CHADEMA kinajulikana vizuri sana ni chama
kinachofadhiliwa na vyama vya makanisa ya Ujerumani na Denmark, hatujaona hata siku mija CHADEMA kinawasiliana na nchi za kiislamu duniani.mimi ni mchaga na sifurahikii kabisa na mipango ya CHADEMA wanavyofanya najua wakija kupata Urais wa nchi hii basi vitu viwili vikubwa vitatokea vita vya dini na ukabila na ndivyo CHADEMA wanavyoelekea.

kumtukana JK si kwa sababu ni mpinzani wao bali ni kwa sababu ni muislam mbona mkapa alivyokuwa anatawala CHADEMA wala vyama vingine walikuwa hawamtukani? kwa sababu ni mkristo? au kuna jingine?

wewe ni oil chafu so nenda zako kwa amani
 
Utumiaji wa tumbo kufikiri badala ya Akili ni hatari kwa afya yako. Tafakari chukua hatua
 
nilikuwa CHADEMA lakini sasa nimeamua kuondoka

mnafiki tu na pumba zako.sasa ivi kuna kila dalili ya udini na ukabila je cdm ipo madarakan?unajipa ukichaa bila sababu hata hy ccm yenu mbona kuna mataifa mengi tu dunian haina mahusiano nayo?!mwiguru bana....
 
Mleta mada ni mnafiki na mzandiki,mkabila na ni mdini sana huyu.. Toka na propaganda zako na id yako mpya ili ujidai umehama chadema... Mafsadi mtatukoma tu vijana hatudanganyiki na ccm.
 
Cartoon_ZAPIRO_South_Africa_ANCYL_Julius_Malema.jpg
 
rudi kwa wachumia tumbo wenzio,kaongeze idadi ya punda huko ccm
 
Kadi yako ya CDM ni namba ngapi na ulikuwa mwanachama kupitia tawi gani?

Lakini ni vema ukawa na tangible evidence ya hiki unachokiita na kuonesha kama udini wa CHADEMA! Unaweza kutuambia ni zuri gani la JK ambalo CDM wamelibeza?

Lakini niseme tu kwamba ufahamu wangu ni kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu kwa ajili ya kutenda mema. Hivyo ni wajibu wa kila mwanadamu kutenda yaliyo mema, hivyo binafsi huwa sitarajii mtu akitenda mema asifiwe bali akitenda kinyume na matarajio ni lazima akemewe kwa nguvu zote na kila mtu.

Ukumbuke uwingi wa madhaifu katika utawala wa sasa ndio umekifanya CHADEMA washamiri na wananchi kufunguka macho na kutambua wamekuwa wakifanyiwa ndivyo sivyo na watawala waliowachagua wenyewe...

Tukirejea kwa utawala wa Mkapa, ukweli ni lazima usemwe, jamaa alijitahidi sana kuimarisha uchumi wa nchi hii na kuiletea heshima nchi na wananchi wake mbele jumuiya ya kimataifa. Mkapa ameiacha nchi na akiba ya kuridhisha. Thamani ya sarafu yetu ilikuwa imara dhidi ya sarafu za nje kama dola ya Marekani, n.k. Hii haimaanishi hakuwa na mapungufu, yalikuwepo kama ya uuzaji wa makapuni na viwanda bila umakini wa kuhakikisha uuzwaji huo unakuwa wa kuyaendeleaza makampuni na viwanda hivyo kwa ajili ya kulinda ajira za watanzania na kuendelea kukuza uchumi wetu.

Alichofanya JK alipoingia madarakani tu ni kutoa ahadi nzuri nzuri kama upitiaji wa upya wa mikataba ya madini, lkn kumbukumbu zangu haziniambii kama hili limewahi kufanyika na wananchi kuambiwa kilichofanyika na nini tulikuwa tunapoteza na sasa tunakipata. Alipoingia alishughulikia uhalifu uliokuwa umekithiri chini ya uongozi wa IGP Mahita, lkn hili halikupa uhai wa kutosha badala yake tumekuwa tukishuhudia madhara kwa raia yanayoaminika kutenda na askari wetu na kila mara wakija na tume cha kuchunguza na kuishia hapo zaidi zaidi utasikia amepigwa na kitu kizito, kitu che ncha kali, n.k.

Lakini hatimaye una uhuru kamili kwa mujibu wa katiba kuchagua kujiunga na chama chochote cha siasa au kuchagua kutokuwa na chama chochote pia! Salaam zao uendako CCM
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kunena kuwa ukiona mtu analeta mada za udini na ukabila kwenye siasa,ujue dhahiri kuwa huyo mtu amefilisika kisiasa.

Gamba huyu aliyeleta post hii,siyo tu amefilisika kisiasa,bali pia anaweweseka,kwa kuwa anaona mwaka 2015 ndiyo umekaribia,na kete zote za kuimaliza Chadema, zote zimebackfire.

Walianza na Chadema chama cha wachaga,wakaja gundua, hata wanyakyusa, wasukuma,waha,wahaya,wahehe,wafipa,wameru,waarusha na makabila mengine wanaisupport kwa nguvu sana Chadema!

Wakaja na kete kuwa Chadema ni chama cha wakristo, kete hiyo nayo imefeli vibaya sana baada ya mamilioni wa madhehebu mengine,kuisupport kwa nguvu sana CDM!

Mwigulu Nchemba hivi karibuni akaja na gia ambayo alitamba nayo kuwa ataitolea ushahidi hata mbinguni kuwa Chadema ni chama cha kigaidi. Hili nalo Mwigulu Nchemba na CCM yake wamepata aibu ya karne,baada ya majaji wenye weledi wa hali ya juu,kuzitupilia mbali kesi zote hizo za kubambikiwa na polusiccm na DPP wao Feleshi,ambaye amesababisha taaluma ya sheria hivi sasa TZ,kuonekana sawasawa na machinga anayetembeza nguo barabarani.

Kwa hiyo huyu mleta post,namsihi asiweweseke,bali atulie asubiri kunyolewa bila maji,ifikapo mwaka 2015!!
 
Chama hiki kimekuwa hakina shukrani kabisa nchi hii na wala uzalendo kwa taifa ndio maana katibu mkuu mzee Slaa anaiunga mkono Rwanda

Kila kizuri cha Kikwete au CCM lazima CHADEMA wakitie kasoro,chama cha CHADEMA kinajulikana vizuri sana ni chama
kinachofadhiliwa na vyama vya makanisa ya Ujerumani na Denmark, hatujaona hata siku mija CHADEMA kinawasiliana na nchi za kiislamu duniani.mimi ni mchaga na sifurahikii kabisa na mipango ya CHADEMA wanavyofanya najua wakija kupata Urais wa nchi hii basi vitu viwili vikubwa vitatokea vita vya dini na ukabila na ndivyo CHADEMA wanavyoelekea.

kumtukana JK si kwa sababu ni mpinzani wao bali ni kwa sababu ni muislam mbona mkapa alivyokuwa anatawala CHADEMA wala vyama vingine walikuwa hawamtukani? kwa sababu ni mkristo? au kuna jingine?
Ungekuwa VERIFIED USER ningeamini kuwa umehama... we utakuwa wa buku saba tu..... na njaa zenu msizosema nazo hizo, zitakuja kuwafikisha pabaya..
 
Mwana-CCM au yeyote anaweza kufungua ID na kujifanya CHADEMA kisha akatangaza kuhamia CCM kama ilivyo mbinu yenu ya kununua/kuchapa shahada mpya za CHADEMA na kujifanya zimerudishwa

Umenikumbusha story ya Le Mutuz na kadi zake feki za chadema zilizotengenezwa china. Jamaa kazunguka nazo kwenye ziara zake mikoani lakini hazijasaidia kitu!
 
Naona ulichotumwa kukipeleza ndani ya CDM hukufanikiwa kukipata sasa unajifanya kurudi CCM. Ukifika huko hata Elfu saba hautopata maana jasho lilivyokutoka na bado umerudi mikono mitupu.
 
Back
Top Bottom