Mwezi March katikati niliona nafasi hapa jamvini pale Ubalozi wa UK, mtoto kapuku nikajitutumua, kama masihara vile siku moja niko zangu ofsini nikapigiwa simu na dada mmoja mwenye sauti nyororo akitema ngeli iliyotulia akinieleza niende kwenye intavyu nikamwambia nitatia timu bibie,basi akakata simu,dakika chache smartphone yangu ikatoa mlio wa email kucheki ni yeye kama Ass Hr amenitumia maelekezo yote,mwanaume nikatia timu siku niliyopangiwa tukapepetana nao kama saa 1 zima hivi,wazungu 2,mbongo mmoja wa kike,yule aliyenitwangia yeye alikuja kunipokea receiption tu na kunipeleka kwa wale wenzie,after 1 week akanitumia tena mail akasema wamempa nafasi mtu mwingine aliyefanya vizuri zaidi yangu,na kunishukuru huku akiniomba nisiache kuomba kama kutatokea nafasi zingine siku zijazo,nakamjibu poa mrembo,na wala sikuumia sana maana kazi ninayo kitambo tu,ila nilitaka nichangamkie fursa kwe taasisi ya kidplomasia