Nimeamini! Huyu Mwanadada Amebarikiwa....!

Nimeamini! Huyu Mwanadada Amebarikiwa....!

mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
2,170
Reaction score
3,106
Nilikuwa Nikizisikia Sana Nyimbo Zake Hasa Kwa Vijana Wa Bodaboda Lakini Sikutilia Maanani Kwa Kuwa Mimi Sio Mwamini.

Juzi Nikiwa Ndani Ya Daladala Kuna Msichana Alisahau Album Yake Kwenye Seat, Ikiwa Ni Mpya Kabisa Katoka Kununua Nikasema Ngoja Niichukue Mtaani Nikikutana Na Mpendwa Nitamuuzia Hata Kwa Buku Jero, Cha Kushangaza Nilipofika Mtaani Kila Mteja Alisema Kuwa Yeye Tayari Ana Nakala Ya Hiyo Album, Nikaona Isiwe kesi Ngoja Nikaisikilize Mwenyewe Gheto Japo Sio Type Zangu.

Sikuamini Nilivyo Sikiliza Kwa Makini Nyimbo Zake Haswa Ule Wa "Mzee Tupatupa(kampeni)", Kuna Ule Wa "Maamuzi Yako Leo Ndio Matoke Ya Kesho", Nimebarikiwa Gafla Yaani Haswa Kile Kibao Cha "dunia Haina Huruma". Huyu Dada Wa Kuitwa Bahati Bukuku Jinsi Anavyoilenga Jamii Katika Nyimbo Zake Na Sauti Yake Ya Base, Nampigia Salute! Waungwana Nisaidieni Kama Kuna Album Zake Nyingine Nitajieni Majina Nikazitafute, Uongo Mbaya Huyu Dada Katushika Mpaka Wapagani.
 
jamani sikilizeni hizi nyimbo zake kwanza ndo mje humu: mzee tupa tupa, maamuzi yako ni matokeo ya kesho, dunia haina huruma
 
hao kina bukuku zilipendwa sasa hivi wapo vijana wanaimba injili balaa hebu tafuta album za NEEMA JEKONIA CHAVALA na ENOCK JONAS halafu njoo utupe ripoti.
 
hao kina bukuku zilipendwa sasa hivi wapo vijana wanaimba injili balaa hebu tafuta album za NEEMA JEKONIA CHAVALA na ENOCK JONAS halafu njoo utupe ripoti.

Huyo Enock Jonas siyo siri hata mimi amenishika.
 
Bukuku yuko juu tangia anaanza hii kazi ya kuhuburi kupitia nyimbo. Album zake zote ninazo, namkubali sana huyu mwanadada
 
jamani sikilizeni hizi nyimbo zake kwanza ndo mje humu: mzee tupa tupa, maamuzi yako ni matokeo ya kesho, dunia haina huruma

Ni Kweli Mkuu Nilichokipenda Ni Kwamba Ujumbe Wake Unawahusu Watu Wa Itikadi Zote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom