Nimeamini hanipendi huyu msichana

Bin Shaib

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,315
1,186
Wakuu mpo naamini mnaendelea kulijenga taifa letu pendwa Tanzania.

Nimekaa kwa muda bila kuwa kwenye mahusiano baada ya kuumizwa sana, nikiwa najiuliza kweli nitampata mwenye mapenzi ya kweli?

Daaaah! Sijui alinishauri nani?

Ok twende..

Hivi hawa wanawake ili wakupende kwa dhati inatakiwa uwape nini au uwafanyie nini?

Mpaka sasa nahisi mahusiano yangu hapa yalipofikia yanaelekea kufa maana nacho kiona kinanikatisha tamaa

Nipo kwenye mahusiano na msichana ambae niliamini kuwa ananipenda kwa dhati kutokana na jinsi matendo yake yalivyo kuwa na tulipo kuwa tukiongea pamoja katika kupiga story nilijiaminisha kweli huyu ndie.

Mahusiano yetu yameendelea kwa muda sana nahisi yapata mwaka 1, lakini hatujawahi kufanya sex.

Nimekuwa nikimwambia kuhusu sex ananiletea sababu mbalimbali, anasema au Mimi nataka kumchezea tu halafu nimuache, mara ataniambia siku akiwa tayari, hawezi kutoka pale home mida ya usiku.

Mpaka sasa simuelewi japo mie naheshimu hisia zake na mawazo yake sipendi kumlazimisha kuhusu sex.

Hadi sasa mawazo yangu yananituma au nitumie ule muda wa story mimi na yeye tukutanapo nimshawishi hata kwa romance ili anitunukie?

Kwa maana sitaki kumsariti kwa kwenda na wasichana wengine tofaut na yeye maana naheshimu hisia zake lakini mimi naona haziheshimu hisia zangu..

KANICHUKIA GHAFLA
Ni kweli ametumia pesa zangu pamoja na zawadi mbalimbali toka kwangu lakini nashangaa kabadilika kuna siku kaniomba pesa ya kununua viatu vya kike yaani ndala ,alidai alizo kuwa nazo zilikatika.

Namnavyo jua saa hizi hali si shwari mtaani basi nikamuahidi kuwa ntamchukulia siku yoyote, akasema poa
Mambo toka siku hiyo yaligoma kabisa kuhusu kupata mpunga, sasa kwa huyu msichana naona kakasirika na yale mazoea kama kipindi cha nyuma yamekata ghafla,

Kipindi cha nyuma alikuwa akiniona lazima asimame tupige hata story kidogo, saa hizi hata akiniona anabadili njia.

Toka siku nimempa ahadi ni siku ya tano sasa hata hana muda na mimi ,akija mtaani kwetu anahemea na kusepa.

Wakuu ushauri wenu je, nimfanye nini huyu msichana?

Au nijitoe mapema kabla sijaumia zaidi na stress za mapenzi?

Je, anamapenzi ya kweli au amenipendea pesa?

Kwanini nikimwambia sina hela anachukia na ananihoji kuwa hela zangu nazipelekaga wapi?

Cha mwisho haamini kuwa mimi nina mpenzi mmoja tu ambae ni yeye.

Daaaah! Sijui alinishauri nani?
Muwe na siku njema...

2020Bin Shaib Classic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
See i heard them say, heard them say
Boy you a player
You dey score like Messi, play like Kaka
Dribble like Wakaso
You dey like Barcelona, Real Madrid
Arsenal, Man U, Chelsea

I go give you my heart, give you body
Do anything for you
Sacrifice my life to be your wife
I'm gonna be there for you

But if you break my heart
I go date ur fada
You gonna be my son
You go call me your mother
Say if you break my heart
I go date ur fada
You gonna be my son
You go call me your mother

Sasa wewe badilisha Haya Maneno, Go and Date her Mom! Yasomeke hivi

I go give you my heart, give you body
Do anything for you
Sacrifice my life to be your Boyfriend
I'm gonna be there for you

But if you break my heart
I go date ur Mom
You gonna be my daughter
You go call me your Fada
Say if you break my heart
I go date ur Mom
You gonna be my daughter
You go call me your Fada

Nenda kafanye kweli at your own risk though



Kitochi Original
 
Mkuu mademu wa kibongo asilimia kubwa wanatengenezewa mazingira tu,ukisema uende kizungu utasubiri sana.
Unaweza panga kaa outing ka mbali,mkalala huko huko na kumtafuna,unaweza kufake ugonjwa akaja getto kukuona ukamaliza n.k
Hapo sasa ndo najiuliza kila nikimwambia napigwa za maradona, wakati yeye anatumia vyangu tu,
Naninavyo jua mapenzi yanaweza kufa bila kula tunda wakati wewe vyako visha liwa kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahusiano bila sex yanatoka wapi siku hiz?

Huyo dada kakuchomesha mahindi sana hlf ni mwaka mzima yan siku 365 kaninginiza ahadi tu bila kuishusha!

Kwa jinsi ulivyoelezea, huyo dada ana agenda ya kukufanya uwe mtaji wake wa maisha na kafanikiwa kwa mwaka mmoja...Wewe bado unangangania tu!

Akili yake inasema 'nina bwege langu lipo mahali, ni kulikamua tu na kujipimia nitakavyo'
 
Mkuu mademu wa kibongo asilimia kubwa wanatengenezewa mazingira tu,ukisema uende kizungu utasubiri sana.
Unaweza panga kaa outing ka mbali,mkalala huko huko na kumtafuna,unaweza kufake ugonjwa akaja getto kukuona ukamaliza n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesomeka mkuu....
Kuna mademu wengine bila wewe kumkontrol hawezi kukitamkia mbashara kuwa twende tukabanduane
Daah! Somo limeingia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tafuta hela nmeona tatizo kubwa huna hla

Sent using Jamii Forums mobile app

Hela anatokea kwenye betting na hali, kwa hali hii ni sahihi huyo demu kumzingua!
 
Bin Shaib, Unaliwa hadi chenchi hapo, shtuka na uchape lapa. Huyo hana nia na wewe na ameshajua umrkufa na kuoza kwake. Anatumia huo udhaifu wako, kama silaha na kama ukiendelea naye nakwambia utakuja kulazwa kwa presha kushuka.

Fanya hivi, mpotezee kimyakimya bila kumwambia lolote lile. Yaani usimtafute, wala kushughulika naye. Ukiona hajarudi, basi elewa nilichokwambia ni sahihi. Na kama akijileta jifanye si wa kumpapatikia kama mwanzo, jifanye upo busy sana na mishe zako na una muda mdogo.

Karudi ukaonesha una muda naye, atajua zoba lake bado lipo upande wake. Yaani hivyohivyo kaza kama kweli alikufanyia vile kisa upendo atajileta mwenyewe na akija piga na ukiona hakuna kizuizi jua ana mtu mwingine na wewe ulikuwa wa dharura tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom