Nimeachwa tena

Sidhani Kama hii ni habari kamili, kila mtu anafahamu ukweli nauhalisia nafsini mwake.
 
Kwani kulikua na ulazima sana wa wewe kula chakula cha sherehe?
 
Kwanini unapenda kutoka toka wakati mwenzawako hapendi kutoka toka? Na kwenye kutafuta mwenza lazima uangalie je mwenzangu anapenda kutoka toka usiku ili muendane sasa wewe unapenda kutoka kujichanganya yeye mwenzako yupo tofauti hapendi" lakini na wewe hutaki kucheza mfumo anao upenda tatizo linaanza hapo, Wanaume tupo tofauti wengine hawapendi mikusanyiko ya watu wengi na wengine wanapenda mikusanyiko.
 
Mtu akionyesha hakutaki kaa pembeni. Kujifanya king'ang'anizi utaonyeshwa dharau hadi ukome. Kama unaamini huna makosa piga kimya akikutaka atakufata.
Huyo hamuendani na kama unampenda sana jifanye boya maisha yasonge.
 
Hapo umenena. Unakuta yeye mtu wa club, bar, outings hafu wewe mtu wa ndani sana. Lazima mtapishana.
 
pole mtu akikuchoka hata sababu ya kijinga atakuacha,kitakacho kusaidia ni kukubali kuachika na kuendelea na maisha mengine,lakini kukuchoka pia inategemea eidha we ndo umesababisha akuchoke
Familia zina mengi jamani
 
Tatzo lenu mnataka 50/50 unaambiwa rud nyumban unakaid labda jamaa alikuwa anataka kuchakata ukamlaza wima km watchman unajua shida anayopata mwanaume ikiwa anataka kuchakata na akakosa mbususu tena kisa sherehe kwendraaa amna namna
maelezo ya upande mmoja huwezi kuyajua uwenda mwanamke naye ni mtu wa masherehe
 
Unailazimishia nfoa nini ... mbona wanaume ambao hawajaoa bado ni wengi!
 
Hajakuoa na hajakulipia mahari mnaishi wote....wazazi wamelifumbia tu macho ???
Hamjaanza kuzinguana leo....anafikia hatua ya kukulaza nje unaona sawa???
Na kuna sehemu umeandika ushawahi enda sherehe ukarudi saa moja jioni akakupiga.....
Kwa haraka haraka nadhani wewe ndio tatizo.
Kuna namna mtu wako anataka u behave na wewe una behave tofauti. Kwanini usifuate anachotaka? Ni lazima kwenda kwenye sherehe kama yeye hataki??
Nafikiri ishi nae vizuri msome tabia yake na ufanye vile anavyopenda kuna kitu kinaitwa ku compromise....kuna baadhi ya mambo huna budi kuyaacha kwa ajili ya afya ya mahusiano yako.Pia moja ya sifa ya mke ni kua submissive ( ila reasonably submissive usiwe mtumwa) Issue za ukatili zikizidi kama kupigwa , kulazwa nje etc chukua hatua hapaswi kukufanyia hayo.
Pole sana I hope mtayamaliza.
 
Usijali dada, hauko peke yako. Hii hapa ya kwangu ya leo leo. Nimeona taaabu hata kumjibu, nimefuta tu namba. Watu tupo billion 7 na sehemu hapa duniani, nahangaika na 1, kweli?

“Stokaa nkaja kwako wala kuonana na wewe ni sameh kwa hilo nilikwambia uninunulie cm ukakataa kabisa , na naonaga nakujaga kwako unanichukulia kama maraya tu pamoja na yote nakujituma kote kwenye mahusiano hujawah kuiona thamani yangu hata sk moja”
 
Pole kwa yote yaliyokupata.

Kosa mojawapo ulilofanya ni KUKOSA UTII kwa mumeo. Ulitakiwa utii agizo lake la kurudi nyumbani/kumpelekea ufunguo. Wewe ukathamini sherehe kuliko mahusiano.

Ukipendwa na mume, basi, rudisha utii kwa mumeo hiyo ni kwa mujibu wa Biblia. Wewe ulifanya ukaidi. Ukiwa mkaidi huwezi kufaidi mema ya nchi.

Kichwa cha habari kinasema umeachwa tena. Je, hii ni mara ya ngapi unaachwa? Je, hizo ulizoachwa ( kama zipo), uliachwa na wanaume wengine tofauti na huyu wa sasa na kwa sababu zipi?
Endapo umeachika mara kadhaa, basi itabi ujitathmini. Huwenda wewe ndiye tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…