Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Nimeachiwa mtoto ndani ya basi

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2012
Posts
5,352
Reaction score
7,662
Nilikuja dar kikazi kwa takribani siku 4, sasa jana nikawa narudi mkoani kwangu. Wkt nipo Ubungo nimekaa kwenye dar express akaja mama mmoja mtu mzima mweupe amebeba mtoto, akaketi pembeni yangu, nikamsalimia nikapiga kimya.


Akaniomba nimbebee mtoto akajisaidie, nikakubali. Muda ukawa unazidi kwenda yule mama harudi! hadi basi linajaa hajarudi, mara kakaja kadem kamoja kakaketi kwenye ile siti ya yule mama nikapigwa na butwaa! nikamueleza kwamba ile siti ina mtu, akanionyesha tiketi yake ikabidi nimuamini kwamba kweli ile ni siti yake

Wkt basi linataka kuondoka ikabidi nimpe taarifa konda, tukashuka na konda na baadhi ya abiria hadi kituo kdg cha polisi ubungo, polisi hawakuniamini sana, wakadhani nafanya usanii nilipotaka kumuacha pale mtoto, ikabidi nipige copy vitambulisho vyangu na niache mawasiliano yangu niondoke na mtoto.

Wamama ndani ya basi wakawa wanapokezana kukabeba na kukalisha, ni katoto ka kiume, ka-handsome, baba, mama na girlfriend wangu nao hawaniamini, wanadhani ni mwanangu! Dah!
 
jamani dunia sasa imisha kwa kweli, nakushauri ndugu yangu mlee mtoto huyo kwa upendo na Mungu atakubariki na kukuinua zaidi na zaidi kwa kufuata taratibu zinazotakiwa. au kama huna uwezo mpeleke kituo cha polisi au kitu cha kulelea watoto yatima
 
we lea tu utazipata baraka zako huko mbeleni wakati mwingine wanawake wanaokabili ugumu wa kuwaela watoto hutumia njia hii akiamni atakuwa amemwacha mwanaye katika mikono salama na atakua kuliko kumtupa na kumtelekeza,kuhusu mama baba na girlfrnd we endelea tu kuwaelewesha kilichojiri watakuelewa tu mwishowe.
 
umepunguziwa kazi Mpwa wangu, umevuna pasi kupanda. Unnataka ukatae mtoto? Soma Bible Mpwa kuna baraka nyingi sana sana, mimi niko kwenye kampeni ya kuwarudisha na kuwakusanya wanangu wote niliowapata nje ya ndoa. hadi sasa nimempata mmoja, msihana mkubwa tu sasa, halafu ana akili kama mimi mwenyewe aisee, usikubali kuacha hio kitu ati and GOD will Bless You
 
Mlee tu na Mungu atakulipa kheir.
Huyo girlfriend na wazazi wako nao baada ya muda wataelewa tu na kushiriki nawe katika kumlea.
Kumbe huu mchezo umerudi tena!!!
 
Mtunze mtoto , japo pale ulipotoa taarifa polisi naamin ulipewa RB. Chukua hiyo) nenda nayo kituo cha polisi karibu na unapoishi uwaonyeshe , kisha nenda serikali za mitaa ukatoe ripoti na kama kuna dawati la jinsia na watoto karibu pia toa taarifa na uonyeshe vidhibiti(RB). Hii itakusaidia siku za usoni
 
Au mkuu ulifanya tukio mahala umesahau? Si unajua mla ndizi?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sipati picha..ikute ndo huwa unafanya kazi mbali na familia yako halafu huwa unarudi nyumbani kila baada ya miez 2. Ghafla yanatokea hayo unafika nyumbani mke na watoto wamejiandaa kuja kukufungulia gate wanakukuta umebeba mtoto..... Mkuu ndo yashatokea mlee tu mtoto ni wako huyo
 
umepunguziwa kazi Mpwa wangu, umevuna pasi kupanda. Unnataka ukatae mtoto? Soma Bible Mpwa kuna baraka nyingi sana sana, mimi niko kwenye kampeni ya kuwarudisha na kuwakusanya wanangu wote niliowapata nje ya ndoa. hadi sasa nimempata mmoja, msihana mkubwa tu sasa, halafu ana akili kama mimi mwenyewe aisee, usikubali kuacha hio kitu ati and GOD will Bless You

Ulikumbuka kuwashukuru waliokulelea?
Kumbuka hukumkabidhi mama yake akiwa msichana mkubwa huyo!!!!
 
Aisee ! Pole sana.lea tu mwaya mtoto huyo huwezi jua mipango ya mungu.
 
Back
Top Bottom