Nimeachishwa kazi na sijalipwa posho stahiki; je, Tume ya Usuluhishi inaweza kunisaidia?

ulongo

Member
Jun 17, 2016
20
7
Wanajukwaa naomba ufafanuzi wa kitalaamu kwa wenye ufahamu kabla sijaenda TUME YA USULUHISHI WA AJIRA.

Niliajiriwa na kampuni moja hapa Dar nikapewa mkataba nitafanya hiyo kazi kama miezi 10 baada ya hapo wakanipeleka mikoani nkafanya kazi huko kwa miaka 2 sasa nikaachishwa kazi huko baada ya kuachishwa kazi kule nilikaa kama siku 17 bila wao kunirudisha Dar ambapo ndio niliajiriwa baada ya kunirudisha nikaenda kuwadai pesa zangu za posho kama sheria inavyosema kwamba ukimsitishia mtu ajira akiwa sehemu ambayo sio ulipomuajiria unatakiwa kumlipo posho kila siku toka siku ile ambae umesitisha ajira yake hadi siku utakaemsafirisha wa hawataki na kifungu cha sheria ni hiki hapa chini

43.-(1) Kama mkataba wa mfanyakazi umesitishwa katika mahali ambapo sipo mfanyakazi alipoajiriwa, mwajiri atatakiwa aidha, (a) kumsafirisha mfanyakazi na vitu vyake kwenda sehemu aliyoajiriwa; (b) kulipa gharama za usafirishaji wa mfanyakazi kwenda mahali alipoajiriwa; au (c) kumlipa mfanyakazi posho ya usafiri kwenda sehemu aliyoajiriwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na posho ya gharama kwa kila siku wakati wa kipindi, kama kipo, kati ya tarehe ya kusitishwa kwa mkataba na tarehe ya kumsafirisha mfanyakazi na familia yake kwenye sehemu aliyoajiriwa. (2) Posho iliyotajwa chini ya kifungu kidogo cha (1)(c) itakuwa sawasawa na angalau nauli ya basi kwenda kituo cha basi kilicho karibu na sehemu ya kuajiriwa.

JE, NIKIENDA TUME YA USURUHISHI WATANISAIDIA KUPATA PESA ZANGU AU MIMI NDIO SIJAKIELEWA KIFUNGU HICHO CHA SHERIA YA AJIRA

msaada wenu please
 
Waoneee wahusika ,ila inategemea kwa nini umeachishwa ...kama umeharibu kazini jipange
 
Waoneee wahusika ,ila inategemea kwa nini umeachishwa ...kama umeharibu kazini jipange
Sheria ya ajira inakutaka umrudishe mfanyakazi wako pale ulipomtoa bila kujali kwanini umemuachisha kazi mana kule sio kwake
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Sheria ya ajira inakutaka umrudishe mfanyakazi wako pale ulipomtoa bila kujali kwanini umemuachisha kazi mana kule sio kwake
Sina utaalamu sana wa sheria za kazi.
Naongea kwa uzoefu.

Ninachojua .
Inaangaliwa ni nani ame breach/misc-conduct the contract.

Kama ni ww ndio umezingua, na wao wakakuterminate, haki nyingi sana unakosa.

Maana kabla ya kukutema, watakuita displinary hearing na watashauriana wakufanye nn. Au pengine kuna makosa ni direct dismissal , haihitaji mashauriano.

Au Either kama ni wao tu wameamua kupunguza kwa sababu za kampuni.
Na hasa ukiwa ndan ya contract, kuna haki watakupa.

Au kama contract imeisha. Wanatakiwa wawe wamekuambia either 1 month prior notice, au zaidi. Na hawakupi haki nyingine maana sheria imefuatwa.

Sasa jitafakari uko kundi gan?.
 
Ishu sio fidia ila ile pesa ambayo sheria inataka upewe km umecheleweshwa kuhamishwa tu
Kama ni mambo madogo madogo malizana nao tu kiutu uzima. Kama mmemalizana vizuri unaweza ukapata future consideration.
 
Inaonekana hata kazin ulikua unawawekea vifungu vya sheria wakikupanga kaz ndo maana wameamua kuachana na we
 
Nenda CMA shauri lako lina uzito sana..

Fika Ofisi ya Kanda uliyopo..hao waajiri wako wababaishaji sana..
 
Back
Top Bottom