Nimeachana na mke wangu

Siku ukienda kumcheck mtoto akishazaliwa, na vile ni first born, naamini hizo tofauti zenu mtazizika, labda kama ni irreconcilable

Nikweli mkuu naamini hivyo
 

Daah sawa mkuu nimekuelewa sana nita fanya hivyo
 
Kama hapo awali hakua na wivu uliopitiliza na maugomvi vumilia mpaka ajifungue ila kama ni tabia yake hiyo toka awali. Piga chini hata usiwaze mara mbili mbili

Sawa mkuu nimekuelewa
 
KOSA LINGINE HILI, HAKUNA MSINGI WA TALAKA HAPO. KUGOMBANA SIO MSINGI WA TALAKA

wewe mwanetu unapotea nakwambia lazima sometimes tuambiane ukweli

Sawa nipemuelekeo sasa mkuu nini cha kufanya
 
Asantee mkuu
Nibaada ya kuamishwa ndo mambo yalipo badilika
Basi usimuache mkeo kwani kinachomfanya awe hivyo ni wivu tu na hiyo mimba inampa kisirani kwani anahisi kwamba wakati yupo kwenye situation hiyo pengine wewe upo na side chicks na hivyo upo mbali ndo kabisa unampa wakati mgumu maana kila muda anakuwazia wewe tu.

Usimuache mwanamke kwa sababu mnagombana tena kwa sababu za wivu tu, bali muache kama ni muasherati.

Kuwa proud na wivu anaokuonea mkeo maana siku wivu ukimuondoka hutompata tena.
 

Mbona Umeamua Vizuri TU? Ushauri Gani na wa Nini Tena Unataka? Ulioa upate Mtu wa kukuliwaza Ukiwa na Mawazo.

Sasa inapotokea uliemchagua ndio anakusababishia Mawazo zaidi, wa nini Tena huyo? Ndio maana nikasema Umeamua Vizuri kujtenga mbali naye. Move on. Utaumia kiasi lakini Utazoea TU.

Na utakuwa na AMANI...!
 
Bahna eh hutulipi fupisha maelezo hata wewe inaonesha unakera waih
Sikia pambana na hali Yako .
Kwanza siye tunashida zetu wenyewe napia kama umuacha haituhusu
 
USIMWACHE HATA KIDOGO !!

Wewe bado hujapata maarifa ya kuishi na mwanamke. Ukiona mwanamke ni mja mzito halafu ana ugomvi hivyo, jua tu ni HIYO MIMBA INAMSUMBUA !! Hujuilizi ni kwa nini baadhi ya wanawake waja wazito wana hamu kubwa kula udongo? Lakini akishajifungua hamu inaisha !!

Wacha nikwambie. Huyu wa kwako sio anakuchukia. Ni hiyo mimba tu ! Kuna mwingine akiwa mja mzito ANAKUPENDA KUPITA KIASI - yaani inafikia hataki utoke uende kazini!! Anakuwa KERO ! Lakini mwanaume mwenye akili unamchukilia tu kama mtoto uliyemnyima pipi halafu anakuwa na hasira mbaya hadi eti kutaka kukupiga!!

Nakushauri tena !! Usimwache. Ugomvi wake kwako unasababishwa na ukweli kwamba ANAKUPENDA SANA !! Anaona WIVU MKALI kwa vile anajua ni mja mzito na huwezi "kupiga mechi ya kiuhakika na yeye", hivyo anaamini kama uko mbali lazima unabanjua "samsing" ya pembeni !!

Zaidi ya hapo, wewe mwenyewe unampenda sana mkeo!!I MIMI SIKUJUI lakini DONT EVER MAKE THE MISTAKE OF LEAVING HER !!

Wanawake wote ni "kiungulia" tu. Kamwe hutakaa umpate ambaye hana mambo ya ajabu. Ukimwacha huyu unaweza ukampata unayedhani ni mpole kumbe ni malaya wa kutupwa! Au mwingine anataka umnunulie kila nguo inayokuja mpya, kila kitenge, kila kanga, na ukimwambia pesa hakuna anakununia na hata kufikia kukunyima "haki yako"

Mwingine atakugombanisha na ndugu na marafiki na hata wafanyakazi wenzako au wateja.

BAKI NA HUYO ! Waswahili husema:-
"Awali ni awali tu hata ikiwa ngada" (karata)
 
Kusema kweli hili mi binafsi japo wanawake wenzangu watanipopoa ila tuseme tu ukweli.
Mbonq kama mimba zinatofautiana kulingana na status ya mtu?

Maana kuna watu wa matabaka flani wakiwaga na mimba hujui Wadada wa kazi, mtu ambae bwana kaikataa mimba au hana hela unakua zako normal tu!

Ila hawa zake za wenyewe hawa eeeeweh!!!! Ni hatari niko hapa na mke wa mtu naishi nae ananinyanyasa kama hakai kwangu kwanza unamfulia, anajifanya akivaa nguo dakika 0 imechafuka, mara unanuka mara niketee sijui upupu gani!!! Hapo hajaanza kulalamika oooh mimba kazi ooooh mimba fyoko yani mambo ya hovyo tu

Kusema kweli mi Mleta mada namuelewa sana! Hapa msijifanye mnajua sana kuishi na mimba ila hawa so called Wifes wenye mimba wanakera mno MNOOOOO! hata mimi ningeondoka manake maisha yenyewe ya saivi ni mimba tosha bado na mmama wa mtu akuvuruge aaah
Braza ajichimbie uko akijifungua akamwone amuulize kaacha utoto ?? Kama kaaacha waendelee na maisha.
 
Hizo mimba ni kisingizio tu hamna kitu hapo, yaanii mimba haiwezi sababisha mtunga mimba akachukiwa, unaweza Kuta hata mimba sio ya jamaa
 
Hizo mimba ni kisingizio tu hamna kitu hapo, yaanii mimba haiwezi sababisha mtunga mimba akachukiwa, unaweza Kuta hata mimba sio ya jamaa
Mimba imekua kama sehemu ya kujiendekezea ili kutimiza mambo ambayo wazazi hawajakufanyia kwenu [emoji23]eti homoni

Homoni gani bwanaa homoni zina react mwilini sio zinatuma udongo sijui pweza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…