Nimeachana na mke wangu

Wanawake wakiwa kwenye kipindi cha ujauzito wanasumbua sana uamuzi wako ni mzuri wengine huwa wanawarudishaga nyumbani kwao mpaka watakapo jifungua

Nikweli lakini sikuhtaji iwe hivyo kwangu kuwa mkewangu aende kwao lakin ndoivo yametoka haya
 
Umefanya maamuzi ya kiume,lakini!,[emoji848] inaonekana una tabia za kike,huo muda wa kujibishana na mwanamke unapata wap?,si umuache aongeee akichoka atanyamaza

Mkuu anyway sawa
 
Akijifungua atatulia
 
Ungempa muda wa kupumzika kwa maana kama kwao ni karibu basi akajitazamie kwao au kama hivyo uko mbali mbali ungetafuta ndugu yake wa kukaa NAYE halafu wewe ukawa unaendesha mambo ukiwa huko...

Natumai inawezekana na
 
Wewe una roho mbaya!
Umemuonea dada wa watu tu
Ungesubiri ajifungue ndo uweze kumhukumu!
 
Kuna version hujaiandika.Kuhusu maisha yako huko Dodoma....Una mwanamke/wanawake
 
Mhh kwamaamuzi haya yko,kunamengi hujayasema kukuhusu pamoja na kipindi kigumu cha ujauzito anachopitia mwenzako naye anaziada inayomtesa juu ya tabia yako+ukombalinae kwa sasa hawezi kujua unafanya nini hapo ulipo.

Pili mbona unaongea kama umetake advantage ya maumivu yake juu yako,nikweli umemwacha au umeleta uzi tupotezee muda,ukweli sijaona juhudi hasa ulizofanya kumtuliza mwezio kama kweli unafwedha ungeagiza nae awepo huko ulipo japo usiku apoze moyowake kwamba uposalama na haibiwi maliyake,Ila kwakujinafasi kwamba umemwachia hela,umechukua apartment unaishi pekeyako mh.

Na pia nadhani utakuwa hujakomaa kifamilia ndugu yangu,ndiokwanza umejaribu kuoa ila ndoa imekushinda
Anyway pole yake mama k wa watu,upendowake wa kukuletea jina hapa duniani umemponza.
 
sema wajawazito wa siku hizi wamezidi jamani mbona kule kijijini kwetu hayo mambo hayakuwepo
 
Sawa mkuu nimekuelewa shukrani
Na siku nyingine usirudie tena kulitamka hilo neno kuachana kemea kabisa. maneno uumba. Kuwa mtu wa kurekebisha mambo na si kubomoa. huyo mtu ana kiumbe chako tumboni halafu unatamka kumuacha, hujui hata mtoto tumboni anawasikia mnavyochemka hapa duniani.

Wenzako watoto wakiwa tumboni uwa tunaiambia mimba na kuinenea mazuri na kumnenea mtoto mema pindi atakapozaliwa. Wewe kinyume chake unatangaza kuachana na mkeo, yaani mnampa stress mtoto toka mimba.

Umenikwaza sana. Rudi kamuombe radhi mkeo na umuombe radhi huyo mtoto aliyeko tumbani
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Ndo mtoto wao wa kwanza jamani ana mengi ya kujifunza msimlaumu sanaa..
 
Siku akijifungua utamkana mwenyew,utasema ni yeye kweli?,mbona kabadilika...Iliwahi kunitokea mimba hainitaki mimi,nilimrudisha fasta kwa Mother,hali ilitulia maana wazee wanajua jinsi ya kuhandle hali hizo.

Alipojifungua alikuwa anahadithia na kuishia kucheka tu....
 
Mungu ni mwaminifu sana. Nimefurahi wengi wenu hapa mmemcrush mleta mada na kumpa ushauri mzuri. knows kama una hekima na busara basi utafanyia kazi hizi shauri.

Madhaifu kwetu wanawake yapo na mwanadam bila udhaifu jiulize mara mbili..utakuwa unaish na kijini alichokiimba mbosso. Najua unao moyo mzuri na mpaka kuamua kumuoa ina maana alikidhi vigezo vyako.

Yumkin hiyo ndo ile 20% alioikosa katika zile 100% zako kwahyo mbebe aisee. Hata wewe deep down unafaham unao udhaifu. Kama unapenda kuwa mtu wa maana hapo baadae na kuwa baba bora katika jamii futa kuachana katika akili yako. Ndoa is a struggle for both parties. Work on your marriage. Mungu awasaidie kuitengeneza familia yenu. Be blessed
 
wewe ushafikishwa kileleni au umechangia ili kuharibu maudhui ya anayeomba ushauri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…