Nimeachana na hawara nachanganyikiwa

jamani hivi m.me mzinzi huwa anabadilika?mimi siamini hicho kitu,kama kubadilika mpaka yamkute ndio hubadilika.ila hata umuwekee vikao ni ngumu au labda aamue mwenyewe tu.kikubwa utaambiwa vumilia,muombe mungu kuna mawili uvumilie uletewe ukimwi ndani ya nyumba,au uvumilie uishi maisha ya huzuni kila siku.tangu sister wangu,tulimzika kwa ukimwi kwa kuambiwa neno la vumilia,muombe mungu.{kwa upande wangu simvumilii m.me mzinzi}bora niwe sina mtu niwe lonely maisha kuliko kuvumilia.sister jitahidi kujikomboa kimaisha.wewe ndio unaishi nae,unajua mazuri na mabaya yake.unavyoamua,amua kwa ajili ya mtoto wako na usiamue kwa kuiridhisha jamii.kwa miaka yako,bado mdogo,

tatizo unaweza kuishi na mume mzinzi miaka na miaka na usigundue!!!!!!!
pole kisukari...
 
Sasa kama mume humpendi wala humtaki wa nini unabaki nae?!Kama umeona hamna kitakachobadilika kaanze maisha yako upya mlee kila mmoja akiwa kwake!


Watu wengi wanaishi kwenye ndoa za kitumwa ilimradi waonekane ni wanandoa lakini ni bora kuivunja ndoa inapodhihiri kuwa wanandoa hawana amani wala furaha kutokana na tabia na matendo ya wenziwao sijui maana dini nazo zinadai tubebe misalaba ,hata kama ni ya cuma na inawaka moto,
Mtazamo wangu ni either kujitahidi kuijadili kwa wema hiyo ndoa yenu na kama mtaona kuwa hamuwezi kabisa kuendelea kuishi ni bora pia kuachana kwa wema kila mmoja anaweza pata mwingine mkaishi vizuri na kusahau yaliyopita
 
vidumu oyeeeeeeeeeeeeee,kwani huwezi kuwakeeep wote wawili?mbona wengine wanaweza?lol:confused2::whistle:

Na hii ndo dawa ya wanaume wazinifu! kumuacha huwezi as jamii zetu bado talaka inaonekana ni kitu cha aibu! so kidumu chako kimya! Heshima ya uongo ndani n big love kwa watoto maisha yanaenda, yaani kuwa na kidumu kunapunguza hizi stress na kushuka sukari sababu ya ndoa,
 
Mi naona tatizo ulikimbilia kutafuta suluhisho nje ya ndoa(the so called kidumu) kabla hujashirikisha wahusika wa familia as advised b4, mbaya zaidi huwajui wanaume hata kidogo!Mtoto tulia,tena nakwambia utakuja juta wewee,shauri yako.Utahesabu wanaume weeeee at last utakuta umri umeenda,hakuna anayekutamani tena,unaishi as single mother(maisha ambayo ukiwa kijana utaona ni matamu,si uko free) ila ukishazeeka utajikuta kwenye TATIZO la UPWEKE usioelezeke.

Tatizo unataka UKALE UJANA ndani ya NDOA.Kama wewe ni islam ruksa kudai talaka,naona wenzetu hawa ndoa IN/OUT ni kawaida kama kupanda daladala na kushuka,tena waume nao kibao,unaachwa leo kesho anakuoa ?(????????????NIDHAMU NA SAIKOLOJIA YA WATOTO JE)


Mimi sijaona tatizo serious kwa mumeo hapa,ninachoona ni wewe kupagawishwa nje ya ndoa.Binadamu wote hukosea,ulichukua hatua gani?

Si ulishamkuta kaacha mara2,sasa ulidhani wewe ni malaika na wenzio waliotangulia walikuwa mashetani?Huyo kidumu chako ushaishi naye ukajua mapungufu yake,nakuhurumia sana mdogo wangu.
 
...... nakumbuka ni kama miezi 2 imepita kuna kijana alionyesha kunipenda sana, huyo kijana ni mwanafunz wa chuo kikuu kimoja na yupo mwaka wa 3, na alikuwa anaishi jirani na nyumbani kwangu. kweli nikatokea kumpenda sana na tukaanzisha mahusiano bila yy kujua kwamba me ni mke wa mtu......

Hizi sentensi huwa zinaniacha njia panda. Miezi miwili tuu unatokea kumpenda mtu hivyo? Maana kuna thread nyingine hapa, mwanamke aliishia kukopesha mwanaume milioni sita baada ya kuwa kwenye mahusiano naye kwa miezi mitatu tuu. Wanawake kwa nini mnapenda ghafla hivyo?
 
You said it all. Two wrongs does not make it right. Sasa wewe wasema mumeo hajatulia, na wewe umetafuta kidumu; yaani kwa kuwa yeye kamwaga mboga na wewe wamwaga ugali. Mimi naona huo ni ubinafsi!

Kuna watu wawili ambao hauwajali. Mwanao na huyo kijana.

Kama mumeo ni mzinzi (japo kwa sasa na wewe ni mzinzi mwenzie) hauoni kuwa ulikuwa unahatarisha maisha ya kijana unayezini nae. Tena masikini ya Mungu kijana alikuwa hajuhi kuwa wewe ni mke wa mtu? Je una uhakika gani kuwa wewe na mumeo hamna maradhi hadi kwenda kutembea na kijana "unayempenda" kama kweli unampenda au unataka kumuua?

Pili unaposema mumeo kapokea simu ya huyo kijana na akamfokea unanifanya niwe na mashaka kama kweli mumeo ni mzinzi. Tabia za wanaume wazinzi ni wakali kuliko maelezo kwangu mimi mumeo kumfokea tu mwizi wake inanifanya nihisi unamsingizia kuwa ni mzinzi, mzinzi ni wewe mumeo unamuhisi tu.

Mimi pia ni mwanamke na najua wanawake ni wavumilivu, inapofikia mwanamke kutojali familia na kuanza kushindana na mumewe lazima nikemee hata ungekuwa ni ndugu yangu.

Kama ndoa imekushinda chapa lapa sio kuchanganya wanume.

Sorry kwa kuwa too critical
Lizzy, ni ushauri mzuri, lakini huyu dada yupo kwenye ndoa, na sio vizuri ku-solve tatizo kwa kukimbia, kwani hadi wanaoana alikuwa hajui kuwa anampenda?



Hapo kwenye RED ndio ukweli..

Dada, Mama K, asante kwa kutuomba na sisi tukushauri ufanye nini...

Kikubwa ninachokiona mapenzi na huyo mwanafunzi yajengwa katika misingi ya ngono..na mara nyingi ngono ya uwizi inaonekana ni tamu, lakini madhara yake ni makubwa.
Tayari umefanya vyema kumshauri huyo kijana atafute maisha mengine; na sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa naye wakati umeshajua nini kinaendelea.

Nakushauri utafute muda ukae na mumeo muongee yanayowasibu..Kama umekuwa na ushahidi wa kutosha kwa mumeo kuwa anatoka nje ya ndoa, kwanini usiyapeleke kwa wazazi au washenga wenu?

Hapa unasema;



Umefanya kosa, ndo maana hata moyo wako unakusuta..na huwezi kulipiza baya juu ya baya, na ikanonekana ulifanya haki. Kosa ni kosa tu.

Mie ninaona wewe bado ni msichana mdogo, 24, na maamuzi unayoyafanya ni ya kitoto. Angalia sana, usije ukapoteza ndoa yako kwa sababu tu ya huyo mwanafunzi. Hapa unasema mume wako yuko busy,ni mtu wa safari, una hakika gani kwamba amekuwa ni mtu kutoka nje??..

Hakuna ndoa iliyokamilika dada, zote zina shida kuliko..na unayofurahia mapenzi ya huyo kijana kwa sababu tu hakuna majukumu mengine mazito kama huyo kijana kutafuta chakula, kulea mtoto, yaani kwa kifupi, kinachowakutanisha nyie ni ngono tu..

Sasa kama unataka kuona maisha machungu, achana na huyo mume wako, na ukaishi na huyo kijana, halafu ndo utajua nini maana ya majukumu.. Inaonesha wewe ni mama ya nyumbani, sidhani kama mumeo hakupi matunzo mengine. Sina mengi, ila achana na huyo kijana kama ulivyoamua na uanze kujenga ndoa yako upya. Simama mwanamke..simamia ndoa yako.
 
Back
Top Bottom