Nimchukulie Passo au Vits?

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,074
3,735
Wakuu, habari yenu wakuu,

Ninataka gari la haraka haraka ya kumchukulia wife kwani gari aliyokuwa anaitumia mwanzo ambayo ni Carina t.i nimeamua niiweke sehemu fulani iwe inatega, sasa nimekuwa na kibarua cha kumpeleka wife kazini na kumrudisha jambo ambalo naona linaanza kunishinda kwani ratiba zangu zinabana sana.

Hivyo nimeamua nijichange pesa za haraka haraka nimchukulie kibajaji chake awe anakimbia kimbia nacho hapa mjini, na kwa kuwa sikupanga kununua gari mwaka huu imetokea tu ghafla, bajeti yangu sio kubwa kwa maana ya m5- 5.5 na hii nataka kumvua mtu.

katika kupita pita kuangalia angalia mitandaoni nimeobserve kitu
Vits namba B unapata kwa 5.5 na Passo namba C unapata kwa 5.5. Sasa swali langu ni kuwa nimchukulie Vits au Passo?

Na kwanini Vits namba B ni bei sawa na Passo namba C?

Na kwanini watu wanaziuza Passo sana siku hizi? Au ni bomu linaloenda kulipuka??

Ipi gari nzuri hapa Passo au Vits?? Na advantage na disadvantage ya kila gari ni ipi??

Natanguliza shukrani

mshana jr Mparee2 RRONDO japokuwa juzi tulizinguana kwenye mambo ya majini ila hapa nakujitaji mkuu rafiki yangu Munawar ila usiniambia PASUA tu mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hizo gari mbili zinafanana sana kwenye vitu vya msingi kama engine size,space,fuel consumption. Ila nakushauri uchukue Vitz ni imara zaidi kuliko Passo. Kuhusu bei demand ndio inapandisha bei ya used cars,unajua sisi wabongo kwa mkumbo baada ya Passo kuingia kila mtu anataka Passo kwahio wauzaji wanatumia fursa. Na unaweza kupata gari namba B nzuri kuliko namba C
 
sawa mkuu shukrani sana...
 
Kuna wanunuzi wa magari wanapenda sana number,utasikia nitafutie Gari namba D na yenye km chache bila kujua Gari iliyochakazwa Zanzibar hata Miaka mitatu ikija hapa Dar inawekwa number D na hata ukitaka kilometer sifuri unawekewa....Ushauri nunua Gari iliyo na condition nzuri usiangalie number.
 
Hilo nalo neno
 
mimi sio mtaalam sana kusema nikupe adv na ds-adv za hayo magari, Lakini kwa uzoefu wa kimjinimjini vitz ni imara sana kuliko passo...
 
Mchukuloe vitz ni gari ya uhakika hizo baby walker achana nazo hazihimili safar na hata spare zake zina usumbufu sana na ni pasua kichwa sana chukua vitz ndo gari kati ya hizo ulotaja kutokana na pesa yako ingekua uko juu kidodo ngekushauri uchukue ist
 
Mbona hata vitz ni baby walker?
 
Maisha bwana kweli ni sawa na vidole.....wakati wengine wanakimbiana na wake zao kwa sababu ya hela ya kununulia dela.....wengine wanapiga hesabu za kuwanunulia wake zao magari kwa hiari yao......
 
Back
Top Bottom