Niliyoyashuhudia Leo usiku chuo cha CBE ni HATARI

Niliyoyashuhudia Leo usiku chuo cha CBE ni HATARI

Leo mida ya saa mbili usiku nilikuwa natembea hii njia ya CBE lakini niliyoyaona nilistaajabu,ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

Nimekuta masista du wa chuo cha CBE wakipanga foleni huku wakigombania mihogo saa mbili usiku.

Kwa jinsi walivyo utaona ni matawi ase kweli mwaka huu tunabana matumizi ase

Hadi masista du tunagombania nao mihogo siku hizi ,

Wakati tuliwazoea wakinywa juice wanaacha nusu kwenye glass wakila zege wanabakisha vichips robo kwenye sahani..

Lkn nawashauri mwanafunzi hapaswi kula vyakula vya wanga migumu kama mihogo mida ya usiku ,mwanafunzi yuwapaswa kula vyakula vyepesi usiku ili akiamka asubuhi akili iwe sharp ,kuwe na kiwango cha kuingiza wanga mwilini .
Picha tafadhali
 
Mihogo ya kukaanga ni mitamu sana iwe na kachumbari na pilipili kwa mbali[emoji39]
Nilikuwa nakula mihogo tajwa hapo juu kipindi hicho nasoma F1-6 mpaka baadaye chuo now job lazima siku nikikumbuka wife lazma apike

Kwa hiyo hayo ni mapenzi yao mihogo mitam asee
 
mm huku kila napotoka kufanya mazoezi sasa napishana na wadada tena first year wanatoka gengeni kununua matembele siku nyingine chainizi tena wanabeba mikononi bila hata ya mfuko hii ni wiki sasa kila siku.sasa first year mambo yameishabana hivo mara hii daahh yaani km wanaenda kulisha sungura kumbe wao.saaa kesho mmoja wapo nimepanga niendee nae buchani.kifuatacho ITV tupambe
Acha matusi wewe . Chainese au matembele sio mboga???
 
Mm nimeila sana tu na nimemaliza mwaka 2013 na GPA ya kweli sana, shida yako nn?
 
Ushasikia ile kitu wanaume wa Dar wanaita kifurushi?.... huko kwenye foleni huko jioni saa ya kwenda nyumbani... utasikia mtu dirishani anaita. .. we dada (dada muuza mihogo mibichi na matango kwenye beseni ) wee dada. .. nipe kifurushi..... heheheheheh ndo lala salama hiyo.

Ukiuliza sasa humo kwenye kifurushi kuna nini ....
We mtoto wa Masaki, kula kuku kwa mrija!
Endelea kushangaa hayo ndiyo maisha ya mtanzania wa kawaida.
Kwenu mnakula milo mitatu na kilichobaki anatunziwa mbwa bobi.

Halafu nyie ndo wa kwanza kupata mikopo, endeleeni tu.
 
mm huku kila napotoka kufanya mazoezi sasa napishana na wadada tena first year wanatoka gengeni kununua matembele siku nyingine chainizi tena wanabeba mikononi bila hata ya mfuko hii ni wiki sasa kila siku.sasa first year mambo yameishabana hivo mara hii daahh yaani km wanaenda kulisha sungura kumbe wao.saaa kesho mmoja wapo nimepanga niendee nae buchani.kifuatacho ITV tupambe

Jichagulie tusi
 
Mihogo mbona ni chakula kama vingine tu,
Najua sehemu ambayo watu wanapark magari yao wanasubiri mihogo na inauzika haswaa.
 
HIVI WAAFRIKA NANI KATUROGA?...Tunazarau vyakula vyetu wenyewe? Leo hii mwafrika kajazwa ujinga Wa kula vyakula Vya kizungu ndiyo aonekane mjanja!..yaan kula piza, baga n.k .
Watanzania tubadilike; mababu zetu walikula vyakula asili ya mizizi kama viazi na mihogo n.k, walionekana kuwa na nguvu sana. Sasa sahivi kula mihogo ni UKAPUKU!
Mzungu kafanikiwa sana kutuvuruga!
Kusema ukweli Mimi nakula chochote nikitakacho bila kumwogopa mtu, Ukitaka maisha yaende vizuri usitake kumfurahisha kila MTU!
 
Hao ni wanafunzi hawana kipato, hakuna cha kushangaa nwengine chuo wanatamani mihogo hawaioni.
kama hali ni hiyo Kuna amani kweli kwenye Maisha ya hawa? IQ zao tayari ziko tempered hata pefomens darasan itakuwa ndogo. Ni Mungu tu atusaidie
 
Bongo ikija ishu ya msos balanced diet tumeshindwa maintain kabisa hata middle class families. Ukifulululiza kula nyama kila siku utachukiwa nakuitwa freemason na hutaachwa tu hivihivi juju pia utapigwa
 
HIVI WAAFRIKA NANI KATUROGA?...Tunazarau vyakula vyetu wenyewe? Leo hii mwafrika kajazwa ujinga Wa kula vyakula Vya kizungu ndiyo aonekane mjanja!..yaan kula piza, baga n.k .
Watanzania tubadilike; mababu zetu walikula vyakula asili ya mizizi kama viazi na mihogo n.k, walionekana kuwa na nguvu sana. Sasa sahivi kula mihogo ni UKAPUKU!
Mzungu kafanikiwa sana kutuvuruga!
Kusema ukweli Mimi nakula chochote nikitakacho bila kumwogopa mtu, Ukitaka maisha yaende vizuri usitake kumfurahisha kila MTU!
vyakula vyetu vipi? Hivyo vyakula unavyosema ni vyetu tumeletewa na haohao wazungu akina Vasco. Ulitaka tushindie wadudu mizizi na matunda ya porin (weild berries)?
 
Ha ha haa!..mnashangaa kula mihogo mimi nimeila sana hiyo toka shule ya msingi nikitoka shule mpk chuoni hiyo ni kawaida kwa watoto wa wakulima hawana hela unataka wafanyaje?ni mwendo wa kujibana tu alafu badae ukitoka hapo anakuja b.wege anakuletea ushambenga.ni kupiga tu
 
Nakushangaa, hivi hujui hali ya mtanzania kwa sasa?
Mbona leo nimeshuhudia vigogo flan wakinunua mihogo ya kuchoma kwa wingi kwa ajili ya lunch.
Au mihogo ipi unamaanisha?
pale mirambo street kuna bimkubwa anauza mihogo ya ukweli balaa.. vigogo wengi sana huenda pale
 
Mkuu nimeogopa sana kuskia ni wanawake tu ndio wanakula mihogo...sijui hali ya wanaume ni gani maana hujasema kama umewaona
 
Leo mida ya saa mbili usiku nilikuwa natembea hii njia ya CBE lakini niliyoyaona nilistaajabu,ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

Nimekuta masista du wa chuo cha CBE wakipanga foleni huku wakigombania mihogo saa mbili usiku.

Kwa jinsi walivyo utaona ni matawi ase kweli mwaka huu tunabana matumizi ase

Hadi masista du tunagombania nao mihogo siku hizi ,

Wakati tuliwazoea wakinywa juice wanaacha nusu kwenye glass wakila zege wanabakisha vichips robo kwenye sahani..

Lkn nawashauri mwanafunzi hapaswi kula vyakula vya wanga migumu kama mihogo mida ya usiku ,mwanafunzi yuwapaswa kula vyakula vyepesi usiku ili akiamka asubuhi akili iwe sharp ,kuwe na kiwango cha kuingiza wanga mwilini .
CBE ya wapi mwanza , Dodoma au Dar?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom