Niliyoyashuhudia kwenye mkutano wa injili wa Mwamposa Moshi

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,491
8,721
Nilifanikiwa kuhudhuria mikutano miwili siku ya Ijumaa na Jumamosi. Kuna vitu nilivishuhudia ambavyo kwa kweli kama Wakristo tunapotoka sana.

1. Kwenye mkutano hakuna aliyekuwa amebeba Bible-Hiki ndo kitabu cha mwongozo kwa Wakristo ila pale sijaona mtu mwenye bible.

2. Mtumishi alivyo mkuwa anafika Jukwaani anaanza na watu watoe shuhuda. Nilishangaa sana kwa kweli badala watu wahubiriwe wokovu mtumishi anaanza na watu wenye shuhuda.

3. Watoa shuhuda wana utata sana. Baadhi ya miujiza ina utata kwa kweli. Mmoja wa mtoa ushuhuda alidai baada ya simu yake kuombewa na Nabii alitumiwa pesa laki 2 na baada ya kufika nyumbani akakuta na mume wake ametumiwa laki 3 kimiujiza.

Hakufafanua alitumiwa na nani hasa. Je ni alikuwa anadai mtu? Je kuna ndugu yake alimtumia? Je ni Vodacom walimtumia? Je ni pesa ilitumwa kimakosa kwake? Hapa kuna utata.

4. Watoa shuhuda wengi ni wanawake na hasa kwenye mambo ya uzazi.

5. Mtumishi anasisitiza sana watu watoe sadaka ile noti yenye thamani.

6. Mpaka naondoka siku ya pili sikusikia sehemu mtumishi anahubiri kuhusu watu waache dhambi, watu wawe wema, watu wajiandae na kurudi kwa yesu mara ya pili. Haya sikuyasikia kabisa.

7. Ni sehemu chache sana mtumishi alikuwa anatumia bible. Mahubiri yake mengi ni juu ya mikosi, kurogwa na kadhalika.

8. Mkutanoni mtumishi aliuza sana stika, mafuta ya upako, Jarida lake na Maji. Sijajua maji kama ni kampuni yake.

9. Mtumishi alikuwa anaingia na V8 tinted na hakuna cha kupungia hata waumini mkono.

Kwa kuhitimisha sasa.

Kwa kweli zile shuhuda nyingi ni za kupangwa watu wanapangwa watoe shuhuda.

Baada ya ule mkutano nimeapa.kutokwenda kwenye mikutano ya Manabiii.

Kwenye kukanyaga wese ya upako mimi niliwahi kukanyaga wa kwanza kwanza hivyo wakati majanga yanaanza tayari nilikuwa nje ya uwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Kwenye mkutano hakuna aliyekuwa amebeba Bible-Hiki ndo kitabu cha mwongozo kwa Wakristo ila pale sijaona mtu mwenye bible.

2. Mtumishi alivyo mkuwa anafika Jukwaani anaanza na watu watoe shuhuda. Nilishangaa sana kwa kweli badala watu wahubiriwe wokovu mtumishi anaanza na watu wenye shuhuda.
Huduma ya delivarance au kufungua waliofungwa ni tofauti na huduma ya mahubiri ya kawaida uliyozoea.UNAONA watu wa delivarance wengi huwa na walinzi hicho wewe hukushangaa? Wale walinzi kazi yao kubwa ni kumlinda mtumishi asije vamiwa na wapandisha mapepo au vichaa waliokuja kufunguliwa

Kwa nini huanza delivarance moja kwa moja na sio kuhubiri kwanza?
KUNA mhubiri toka Nigeria alienda marekani kuhubiri ni mhubiri mkubwa tu .Wenyewe wamarekani waliposikia ni mhubiri mkubwa mwenye jina kubwa wakasema njoo wakamlipia kila kitu .LAKINI KWA siri wakapanga kumpima kama kweli ana nguvu za kiroho na ufahamu wa kiroho

wakampeleka kwenye semina akakuta ukumbi umefurika watu wamekaa .Akakaribishwa aanze huduma yake akafungua Biblia akaanza kuhubiri akahubiri kama dakika kumi mwenyeji akasema inatosha.TUONDOKE akaambiwa live kuwa hawamtaki hayuko kiroho.
sababu nini ilikuwa?

wote waliokuwepo ukumbini walikuwa viziwi walichukuliwa sehemu mbali mbali wakaletwa kwenye semina wakamtegeshea wakasema huenda atalijua hilo awafungue kwanza ndipo aanze kuhubiri ,yeye kafika tu na BIBLIA yake kaanza kubwabwaja kwa viziwi

Na hawakumwambia akawauliza kwa nini mlinijaribu wakajibu neno la Mungu linaturuhusu kuzijaribu roho ndio maana tukakujaribu tukakuona huna uwezo wa kiroho kama unavyosifiwa

Watu wenye mapepo kuanza kuwahubiria kwa mtu wa delivarance huwa haaanzii huko

Ni kweli mikutano ya Mwamposya wengi huwa biblia hawana pia sababu wengi HUWA ni waislamu sio wakristo

yapo mengi tu ila cha msingi ujue kuna tofauti kubwa kati ya huduma ya deliverance na hii ya kuhubiri tu kwa kutumia Biblia
 
Watoa shuhuda wana utata sana. Baadhi ya miujiza ina utata kwa kweli. Mmoja wa mtoa ushuhuda alidai baada ya simu yake kuombewa na Nabii alitumiwa pesa laki 2 na baada ya kufika nyumbani akakuta na mume wake ametumiwa laki 3 kimiujiza.

Hakufafanua alitumiwa na nani hasa. Je ni alikuwa anadai mtu? Je kuna ndugu yake alimtumia? Je ni Vodacom walimtumia? Je ni pesa ilitumwa kimakosa kwake? Hapa kuna utata.
Unashanga nini pesa za miujiza zipo.Labda tufafanulie wewe zile pesa petro wakati wa Yesu alitoa kwenye tumbo la samaki na kulipa kodi .Zile hela ziliingiaje kwa samaki ,kutoka chanzo kipi?
 
..................Usijumlishe jamii yote kwa kusema “WAKRISTO TUNANAPOTOKA SANA” ukiwaweka na wale walio timamu vichwani mwao na wanaojua thamani ya Imani ya Kristo,sema “SISI TUNAOJIITA WAKRISTO HUKU HATUJUI TUNAABUDU NINI TUNAPOTOKA SANA”

Ni ujinga na wendawazimu kama mtu unaweza kwenda kuchomwa na jua kiwanjani kumsikiliza mjanja mjanja mmoja akinyofoa baadhi ya vifungu vya Biblia na kuwadanganya watu na kuwauzia baraka,eti anauza maji na mafuta ya baraka mikate ya baraka juzi sijui ni huyu niliona pic's za chvpí kwamba wale walio wagumba wazinunue wavae watajaaliwa uzao,hivi kweli nyie waumini mna akili sawasawa vichwani mwenu???

Kwa sababu anawaona mapoyoyo juzi akaona awape home work ya kufanya ili mjue thamani ya Imani zenu akawadanganya mkagombanie kukanyaga mafuta aliyomwaga chini mmeenda kama nyumbu akaondoka hapo na ishirini,ninini mnafanya ni njaa ama nini?shida zimezidi?Imani haba mnapenda miujiza na mnataka kufanikiwa kwa kuombewa na mtu,mkiambiwa fanyeni kazi hamtaki huku maisha mazuri mkiyataka mnatamani muendeshe magari na kujenga nyumba nzuri kwa kuitikia tu Aminaaa,Aminaaa huku mikono mmeiinua kwa juu.

Hiyo paragraph ya mwisho nashangaa kwanini upo hapa,hata wewe unayeaminika kusoma kwenye ukoo wako unaamini upuuzi wa kukanyaga mafuta?Mungu anisamehe ila ningekuwa Israel na wewe nisingekuacha lazima kingeeleweka siku ile,Mungu hafanyi kazi kibwege hivyo otherwise asingeweka kitu maarifa kwenye bongo za wanadamu amkeni.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom