Naomba kufahamishwa kuhusu Nabii Dkt Elia Mahela

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,486
2,739
Wakuu habari za Wikiend?

Nipo Mkoani Kigoma sasa kwa muda wa zaidi ya Miezi minne, mimi ni mfuatiliaji sana wa Vipindi vya maombi au mahubiri radion au kwenye Runinga.

Hivi karibuni wakati nasikiliza radio moja hivi sijui inaitwaje(ila nafikiri ni radio yake) ila Nilimsikia mtumishi mmoja anajiita Dr nabii Elia mahela nikasikiliza shuhuda zake, maombin.k lakini kubwa alikuwa akialika watu ibadani.

Nilisikiliza sana inaoneka kwa Kigoma ndiye ameshikilia hatamu kama ilivyo Dar kwa Mwamposa NA cOMPANY YAKE(Suguye, kuhani Mussa, mwingira nk).

Nimejaribu kumfuatilia nimesikia story zake nyingi sana nyingine za kumsifu na mbaya kama ilivyo kawaida hasa kupenda hela nasikia Mtumishi ukienda kwake kipaumbele ni wewe utoe hela kwanza.

Naomba anayemfahamu vizuri anipe ABC zake nataka nifike hapo siku moja kwa ajili ya uchunguzi wangu sio kwa ajili ya maombi. maana hata mimi niko na kilinge changu

N.B mimi ni mgeni Hapa Kigoma nimetokea Tanga
 
Una shida na wokovu au unataka kutapeliwa?

Hao nawaita matapeli manabii wa zamani hawakuomba cho chote zaidi ya kutoa maagizo na utabiri wa waliyoagizwa na Mungu hawa wa sasa ni hela mbele na uongo mwingi.

Hata ukimjua haitokusaidia kitu.
 
inaweza kusaidia kumjua mtu kwanza Mkuu. mimi sina shida na wokovu unaotolewa kanisani
 
Una shida na wokovu au unataka kutapeliwa?

Hao nawaita matapeli manabii wa zamani hawakuomba cho chote zaidi ya kutoa maagizo na utabiri wa waliyoagizwa na Mungu hawa wa sasa ni hela mbele na uongo mwingi.
Hata ukimjua haitokusaidia kitu.
Mkuu kabla ya mapinduzi ya viwanda, njia kuu ya uchumi ilikua feudalism na mmiliki wa ardhi lilikua kanisa.
Madhani haya tunayoyaona ni echoes za waliotangulia
 
Mahela sio huyo alikuwa hapo Kinondoni Chama mkabala na headquarter ya Tanesco Kinondoni?!
Ndio huyo ila anayemsema anaitwaElia samwel mahela, kwahiyo yule wa Kinondoni Chama ni baba yake mzazi nafikiri dogo baada ya kuzingua ndio akampeleka Kigoma akatest zali. nasikia anakimbiza sana Kigoma ameishika kigoma kisawa sawa
 
Kama kweli ni babayake mzazi Basi watakuwa wanafanana tabia!

Waingereza husema "like father like son"
Alivyo baba ndivyo alivyo mtoto!

Na waswahili wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka!

Mpaka hapo nadhani nimeeleweka kidogo!
 
Hii ni maajabu wokovu huna shida nao!
Sasa kumjua mtu itakusaidia nini?
kama unaamini wokovu unatolewakanisani wewe ni zaidi ya Mpumbavu. kumjua mtu inasaidia Yesu mwenyewe alosema tusiziamini kila Roho,bali tuzichunguze kwanza. hii ni hatua ya kwanza katika uchunguzi wangu
 
Kama kweli ni babayake mzazi Basi watakuwa wanafanana tabia!

Waingereza husema "like father like son"
Alivyo baba ndivyo alivyo mtoto!

Na waswahili wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka!

Mpaka hapo nadhani nimeeleweka kidogo!
hebu ongeza nyama mkuu unamaanisha nini
 
Wakuu habari za Wikiend?

Nipo Mkoani Kigoma sasa kwa muda wa zaidi ya Miezi minne, mimi ni mfuatiliaji sana wa Vipindi vya maombi au mahubiri radion au kwenye Runinga.

Hivi karibuni wakati nasikiliza radio moja hivi sijui inaitwaje(ila nafikiri ni radio yake) ila Nilimsikia mtumishi mmoja anajiita Dr nabii Elia mahela nikasikiliza shuhuda zake, maombin.k lakini kubwa alikuwa akialika watu ibadani.

Nilisikiliza sana inaoneka kwa Kigoma ndiye ameshikilia hatamu kama ilivyo Dar kwa Mwamposa NA cOMPANY YAKE(Suguye, kuhani Mussa, mwingira nk).

Nimejaribu kumfuatilia nimesikia story zake nyingi sana nyingine za kumsifu na mbaya kama ilivyo kawaida hasa kupenda hela nasikia Mtumishi ukienda kwake kipaumbele ni wewe utoe hela kwanza.

Naomba anayemfahamu vizuri anipe ABC zake nataka nifike hapo siku moja kwa ajili ya uchunguzi wangu sio kwa ajili ya maombi. maana hata mimi niko na kilinge changu

N.B mimi ni mgeni Hapa Kigoma nimetokea Tanga
Tapeli 1 alikuwa kinondoni, akaenda kahama kumbe now yupo kigoma???
 
Back
Top Bottom