Niliyoyashuhudia kwenye mkutano wa injili wa Mwamposa Moshi

Zote za mtoa mada, na hasa hiyo ya kutohubiri kwa habari ya toba na msamaha wa dhambi.
sikuwepo siwezi jibu hilo atuwekee clip za mkutano wote siku hizo mbili tuangalie hapa tujadili kwa pamoja kwa uwazi.MLETA MADA TUWEKEE CLIP ZA MKUTANO ZA SIKU ZOTE MBILI HAPA
 
2. Mtumishi alivyo mkuwa anafika Jukwaani anaanza na watu watoe shuhuda. Nilishangaa sana kwa kweli badala watu wahubiriwe wokovu mtumishi anaanza na watu wenye shuhuda.
huduma ya delivarance ni tofauti na huduma zingine nikueleze kwa nini huanza na shuhuda.UNAPOTAKA kumtandika adui unaanza na shuhuda.BIBLIA inasema wakamshinda kwa shuhuda zao soma
UFU. 12:11

Daudi kabla ya kumpiga Goliathi alianza kwanza kwa shuhuda akasema alikuja dubu nikampiga na kuua,akaja simba nikamrarua na wewe mfilisti leo hii kichwa chako nikakikatilia mbali

Zile shuhuda zina kazi yake kubwa sana kwenye ulimwengu wa roho kabla ya vita kuu ya delivarance haijaanza.Zile shuhuda hazilengi hasa waliokusanyika zinamlenga Goliath kwenye ulimwengu wa roho kuwa kama ulivyoshindwa kwenye haya yanayoshuhudiwa jiandae kukiona cha mtema kuni na leo

Tatizo makanisani huduma za delivarance hazimo ndio maana ukabaki unashanga shangaa tu .Zile ni kukusanya nguvu kupasha misuli tayari kwa vita ya uhakika ya kufungua watu waliofungwa
 
Unashanga nini pesa za miujiza zipo.Labda tufafanulie wewe zile pesa petro wakati wa Yesu alitoa kwenye tumbo la samaki na kulipa kodi .Zile hela ziliingiaje kwa samaki ,kutoka chanzo kipi?
Mkuu samahani naomba unisaidie kifungu cha maandiko ya biblia kinacho husu hili tukio.
 
Mkuu samahani naomba unisaidie kifungu cha maandiko ya biblia kinacho husu hili tukio.
Mathayo 17:24-27
Yesu Na Petro Watoa Kodi Ya Hekalu
24 Yesu na wanafunzi wake walipofika Kapernaumu, wakusanyaji kodi ya Hekalu walimjia Petro wakamwuliza, “Je, mwalimu wako hulipa kodi ya Hekalu?” 25 Petro akajibu, “Ndio, analipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kusema, akamwuli za, “Unaonaje Simoni’ wafalme wa ulimwengu hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Unadhani kutoka kwa jamaa zao au kutoka kwa wageni?” 26 Petro akamjibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Kwa hiyo jamaa zao wamesamehewa. 27 Lakini ili tusiwaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemkamata; mfungue kinywa chake nawe utakuta fedha zinazo tosha kulipia kodi yangu na yako; ichukue ukawalipe.”
 
Yesu mwenyewe alikuwa na mabaunsa 12 mitume wake.POPOTE alipoenda alienda nao
kuna siku alivamiwa baunsa wake petro akatoa kisu chake akamkata sikio mtu
Yesu hakuwa na mabaunsa usipotoshe, tena yeye alimkanya mwanafunzi wake asipambane na watesi wake.
Mabaunsa gani waoga kama Petro kiasi cha kumkana Yesu alivyochukuliwa na watesi wake?
 
YEHODAYA post yako #15 umeandika as if kichwa umekifungia kabatini au umekisahau kwenye seat ya daladala,unasema mikutano yake wanajaa Waislam hivi unadhani mimi ambaye ni Mkristo na namuona tapeli haitakuwa zaidi kwa asiye Mkristo kumuona ni mwizi kabisa?

Hao wanaojazana kumsikiliza mtu kama yule ni wale wavivu wa kusoma Bible wakiamini kila kitu atakimaliza nabii sijui mtume,kusali hawasali wanasubiri mtume asali kubariki walivyopewa mamlaka wavibariki hawataki wamemuachia mtume abariki mwisho kawaambia wakachote baraka kwa miguu.

Pathetic!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Zamani magari ya mafuta yakipata ajali, watu walikuwa wakiyakimbilia na kwenda kuvua kisicho kuwa chao. Utamaduni ulishamiri na kustawi kiasi mengine yaliangushwa makusudi.
Baada ya tukio takatifu la Morogoro, huu utamaduni umepitwa na wakati. siku hizi gari la mafuta likianguka unalikimbia na si kukimbilia!

Kwamba watu wanajifunza zaidi kwa kuona kuliko kusikia! Kwamba tukio kama lile la Moshi liwe la mwanzo na lije kubwa zaidi ili watu waamke! Luka 9:60
 
5. Mtumishi anasisitiza sana watu watoe sadaka ile noti yenye thamani.
Noti pekee ndio imeandikwa FEDHA HALALI KWA MALIPO

AMBAZO SIO NOTI HAZIJAANDIKWA HAYO MANENO

MUNGU MPELEKEE HELA AMBAYO IMEANDIKWA KABISA FEDHA HALALI

NI JAMBO La kiimani ukitaka usiwe unapata mashilingi shilingi uwe unapata noti uwe unapenda kutoa noti sadaka vinginevyo umaskini wa kushika hela ndogo ndogo hauji kukutoka ni njia ya kukusaidia kukua kiimani sababu mtu apandavyo ndivyo atakavyovuna toa noti uvune noti
 
YEHODAYA

Hao wanaojazana kumsikiliza mtu kama yule ni wale wavivu wa kusoma Bible wakiamini kila kitu atakimaliza nabii sijui mtume,kusali hawasali wanasubiri mtume asali kubariki walivyopewa mamlaka wavibariki hawataki wamemuachia mtume abariki mwisho kawaambia wakachote baraka kwa miguu.
Musa kama yupo mwisrael ana haja gani ya kuomba Mungu? Akihitaji kware anamwambia Musa .akihitaji maji anamwambia Musa NA ANAVIPATA

Kuna watumishi wanabeba mizigo ya watu wengine KAMA AKINA MWAMPOSYA na kuna watumishi wengine wanasema muumini jibebe mwenyewe.Hawafungi hawaombei waumini wao wala nini wao kazi yao kula sadaka na mafungu ya kumi na kukoroma madhabahuni ndio aina ya mtu kama wewe.

Kwa nini nihangaike kufunga na kuomba wakati kuna baba yangu awezaye kubeba mizigo yangu na ana mzigo na mimi?
 
Back
Top Bottom