Niliyoyaona Jijini Mwanza

Matapalei fursa zipi😂😂 kule kwenu mnakimbia vibaka.

Mkija huku Kuna jua kali msivae Makoti mnaonekana kama bodaboda na washamba.

Kumbe unajua kujitetea 😂
 
Mwanza wanawake wanakimbiza baiskeli kinoma, tena wanaendesha zile Phoenix alaf mrembo kuwazidi wenzake baiskeli yake inakua ina swaga flan hivi anaitolea kiti Cha nyuma anaweka na bendera ya Simba au yanga hapo mbele

Ww unaongelea Shinyanga
 
Tourism imefanya Arusha iwe na mchanganyiko mkubwa wa watu kutoka mataifa tofauti na hii ni ushahidi tosha A town ni cosmopolitan. Huwezi sema hii kuihusu Mwanza.

Chukua hii uchangamshe ubongo wako. Arusha inapokea maeflu ya wageni toka nchi nyingi duniani na wageni hawa baadhi, wanachagua kuishi Arusha.
 
Unadhani silijui hilo la tourism? Nalifajamu vizuri sana ila siliongei kijuujuu
 
Mkuu hilo wala halina mjadala, sijazaliwa Arusha ila nimesoma na kuishi hapo kwa nyakati kadhaa. Na hakuna mwaka unaisha sijakanyaga Arusha as kila ninapokuja kupumzika mwisho wa mwaka Moshi lazima pia nifike Arusha.

Vijana wa Arusha wana usela wa kizamani, mkuu hili wala usitake kilibishia. Majuzi tu hapa iletrend video vijana wakikimbia na mabodaboda ovyo ovyo kitu kilichosababisha ajali na kuua watu zaidi ya watano. Ukiacha hizo fujo bado hata mtaani kwa teenagers na vitoto vya chuo huwa kuna kuvimbiana sana, wakishajua wewe wa kuja utanyanyapaliwa na unaonekana mtoto wa mama kisa wao wanavuta bange na kuvaa minyonyo.
 
Hahahaha mkuu kule wanapaweza wenyewe na sie baadhi yetu. Napapenda Arusha sababu starehe ipo ya kutosha tu, ingawa binafsi yangu kwa starehe nitachagua Moshi maana hata bia unakunywa kwa amani. Arusha pasua kichwa sana ingawa pesa ipo!!
 
Sasa mkuu mtu umetinga zako jeans safi, T-shirt chini umekula Jordans unapita mitaa ya Sombetini umetoka labda msalimia msela mtu na mnyonyo wake anaanza kukutukana mara akuite bishoo huku anakufata na mawe hiyo ndio strong personality??

Mimi Arusha kwangu ni best kuliko hata Mwanza na Dar. Nikiwa Arusha nafeel some peace of mind lakini tabia za usela mavi ndio zinachafua huo mji. Hujiulizi kwanini kila mtu anaponda tabia hizo? Unafikiri kwanini hiyo unayoiita strong personality inaishia USA au pale njia panda ya KIA ambako Moshi wala hizi tabia hazipo??
 
hahahaaaa
Anasema alikua Mwanza,....afu Hasemi kama aliweza kufika na MBINGUNI.

Wakati wenzake wanaokwenda Brazil lazima wafike Reo De JENEIRO.

Mimi hata sijaamini alichokisema....story yake haina tofauti na zile story ambazo bodaboda wanazokuaga wakizipiga huku wakiwa wamelala juu ya pikipiki.
 
Wewe binafsi nani aliwahi kukurushia mawe kwasababu ulivaa raba nyeupe?

Au unajaribu kudanganya?
 
Kawaida sana.

Biker culture ni kawaida kwa vijana wengi kwenye majiji yote duniani.

Kwa watu wanaotokea places zisizopata watalii hawawezi fahamu hili.
 
Mkuu sihitaji kukulazimisha!!
Sasa wewe umefahamu vipi kwamba vijana wa A town wanarushia mawe watu kwasababu wamevaa raba nyeupe?

Hii haihusianani na wewe kunilazimisha mimi. Hili ni swali linalolenga kuhakiki madai uliyotoa.
 
Sasa wewe umefahamu vipi kwamba vijana wa A town wanarushia mawe watu kwasababu wamevaa raba nyeupe?

Hii haihusianani na wewe kunilazimisha mimi. Hili ni swali linalolenga kuhakiki madai uliyotoa.
Unataka kuhakiki kama nani? Wewe ni RC, RCO, RPC, DC, DCO, MB, Mayor, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya au Katibu wa CCM mpaka unilazimishe nikuaminishe madai yangu?

Na unataka nikuaminishe kwa njia gani hapa mtandaoni zaidi ya maneno ambayo wewe umeyakataa na mimi sijalazimisha uyaamini?? Sasa hapa tukisema vijana wa Arusha akili zenu mnazijuaga wenyewe utasemaje?
 
Nimekuuliza wewe umewahi rushiwa mawe kwasababu ulivaa raba nyeupe?

Au ulidhani madai yako kwamba vijana wa A town wanarushia mawe watu kisa wamevaa raba nyeupe yataachwa bila kutaka uthibitisho?

Kumbuka, huu ni mjadala na utawajibika kudhibitisha kila dai unalotoa.

Turudi kwenye swali la msingi.

Wewe binafsi uliwahi rushiwa mawe kisa ulichagua umevaa raba nyeupe?
 
Nilisharushiwa jiwe moja likanikosa akawa anakimbilia kuomota mengine anirushie huku anaporomosha matusi wenzake wakamkamata. Hii ilikuwa Sombetini mwaka 2009.. Unazijua Supra? Nilikua nimekula Supra ya 120k mguuni kijana kalewa mgundi huko anaona wivu anaanza poromosha mawe..
 
Wapita njia hawawezi kukulewa..
Wanywaji wa mrina na picnic hawawezi kukuelewa.
Watakuelewa watu walio set stds zao na maeneo yenye hadhi Arusha.

Anayeshinda matejoo, unga ltd na Ngarenaro hawezi kuelewa uyasemayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…