Niliyoyaona Jijini Mwanza

Hivi lile soko likilokuaga la nguo especially ile mitumba ilokua inamwagwa pale makoroboi lilihamishiwaga wapii??? 🤔
Siku ya kufungua yale ma baloo nilikuaga natingajee kusagula viwalo vya mtumba juzikati nilipita nikaambiwa lilihamishwa !!
Nafikiri waliamishiwa pale mlango mmoja kama sikosei(sina uhakika sana).

Lile soko lilikuwa linafurika watu balaa hasa watoto wakike.
 
nilifika mwanza mwaka jana june kwa mara ya kwanza nilishangaa ni mji mzuri na mkubwa tu na watu wengi Arusha haifikii mwanza.
 
Arusha isingekuwa usela mavi wa wale machalii clearly hii battle ya Arusha vs Mwanza wala isingekuwa ngumu. Tatizo la Arusha ni vijana wengi wana usela wa miaka ya 90 karne hii..

Arusha ipo mbele ya Mwanza kwa karibia kila kitu, kitu pekee kinachoichafua Arusha ni tabia za vijana wengi wenyeji wa hapo hawana lugha wala charisma ya kuwapokea na kukaa na wageni. Wao kwao mgeni wanamwona ni Mzungu tu.
 
Tatizo watu wanaotoka mikoa tofauti na A town (ukiondoa Kilimanjaro) wana inferiority complex wakikutana na vijana/wakazi kutoka A town.

Wengi wanakosa kujiamini na kudhani wanabaguliwa kumbe hakuna mtu mwenye time nao.

Unaweza gundua hili kwa urahisi tu hasahasa miongoni mwa vijana chini ya miaka 35. Kwa wazee hauwezi kuona hili. Hii naifananisha vile Watanzania wengi walivyo na inferiority complex wakikutana na waKenya.

Hapa Arusha tourism imesaidia pakubwa vijana wengi kuwa na self confidence kwasababu yamwingiliano na wageni.

Jambo la msingi na lakukumbuka, sisi Watanzania wote ni watu poa. Haina haja yakujiona dhaifu au kudhani wakazi wa Arusha wanawachukia wakazi wa maeneo mengine ya Tanzania.

Tanzania ni moja.
 
Kama unafuatilia na ulikaa nao watu wa Arusha mara nyingi wao ndo wanasifia mji wao na usela wao hakuna mtu ana wasifia ..


Ndo maana hata comedian wao wanahype sana mji wao mwisho wa siku wanaonekana kama matahira Yale mavazi hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvaa vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…