Niliyo yaona katika safari yangu ya Cameroon

Niliyo yaona katika safari yangu ya Cameroon

1. Kuna vyakula vya kila aina vingi na ni bei rahisi kwasababu serikali ina control bei za bidhaa huwezi kukuta mtu anajipangia bei ovyo ovyo.
Kuna vyakula vya kila namna mfano ukinunua mkate utaulizwa uwekewe maharage, au chocolate, au samaki wa mchuzi au wa kubanikwa, au butter n.k
2. Ni wakarimu sana hasa kwa wageni hata polisi wakijua wewe ni mgeni wana kutreat kwa heshima siyo kama hapa wageni ni mtaji kwa polisi.
3. Ni wapenda mazoezi na ni magiant kuanzia wanawake mpaka wanaume kufanya mazoezi kwao ni kama culture.
4. Pesa yao ina thamani kuliko yetu na unaweza itumia kokote na ya west africa mfano 100USD kwao ni kama 50000 cefa.
Ila mzunguko wa pesa ni mdogo sana kupata pesa ni ngumu.
5. Kufungua biashara kuna vibari vingi na siyo kama huku eti unakuta mtu ana duka la nguo anauza karanga na vocha kwao hakuna. Kama ni duka la nguo la nguo tu.
6. Huduma za afya ni za kiwango cha juu sana yani sijawahi kuona Tanzania hata kwenye hospital kubwa. Ukienda hospital kule utaflshiwa mwili kabla ya kuwekewa dawa yoyoyote na kila mara wakibadirisha dawa wana kuflash kwanza mwili pia utazungumza na dr atakuuliza matatizo yako kuanzia unywele mpaka unyayo. Hakuna madawa fake wana dawa inafanana panadol ukiwa na kikihozi unameza kidonge kimoja tu kwisha habari yake.
7. Hakuna daladala wana vigari kama passo ndo taxi zao.
8. Wana socialize sana hata kwenye usafiri wa umma siyo kama huku mtu mmoja anaweza anzisha story wote wanachangia yani hakuna ile eti unakaa kimya ni makelele mwanzo mwisho. Hata ukiwa barabarani mtu anakuchangamkia kama anakujua ni wakarimu sana.
9. Miji yao haijajengwa kama huku watu hawana ela kama huku maana kupata ela kwao ni ngumu sana ila kula unakula sana.
10. Kuna baridi kama la mbeya na mvua kila mara.
11. Bado wanaheshimu sana mila zao na ni vigumu kukuta watoto wanafanya mapenzi halafu madada wa kule hawagawi uroda kama soda kugawa uroda kwao ni ngumu sana.
12. Kuna upungufu wa mabinti warembo maana mabinti wengi mabaunsa na wana sura kama za kaka zao.
13. Cameroon imegawanyika katika sehemu mbili, wanakozungumza kingereza na wanaozungumza kifaransa. Wanakozungumza kifaransa wamesoma sana na ndiyo wanajiona wajanja hata raisi wao ametoka katika jamii ya wafaransa.

Haya ni machache niliyo yashuhudia Cameroon bila kusahau kwamba wanakula panya na ngedere na wanajua kupika kweli kweli siyo kama sisi.
Asante kwa Uzi mzuri,naomba jina la Hospital kubwa hapo kwao yenye kila huduma,iwe private au government mkuu
 
Mleta mada hujasema hivi sasa Wakameroon waishio usuizi wanaandamana kufanya fujo hotel ya five stars aishio Rais Paul Biya wakimtaka arejee Nyumbani.
 
Uswiss wamemwambia aondoke alitaka kwenda Ufaransa nako kaambiwa asiende
Mleta mada hujasema hivi sasa Wakameroon waishio usuizi wanaandamana kufanya fujo hotel ya five stars aishio Rais Paul Biya wakimtaka arejee Nyumbani.
 
Kabisa. Ona kama hapa alivyoandika conclusion yake baada ya kuona ''kidonge'' cha kikohozi.
Kabisa. Ona kama hapa alivyoandika conclusion yake baada ya kuona ''kidonge'' cha kikohozi.
Nilichoandika sijaandika kwa kubahatisha. katika mambo ya huduma za afya wako vizuri ni vigumu au hakuna dawa fake kabisa maana wao siyo kama hapa huwezi kuingiza vitu ovyo ovyo mfano uamue kwenda India au china ukaleta vitu. ndiyo maana mzunguko wa ela kwao mdogo sana
 
Kuflash mwili? Sorry, sijakuelewa exactly wanaufanya nini mwili hapa!
Unaondoa takataka zilizopo ndani ya utumbo mdogo, mkubwa, mafuta yaliyobana kona zote za mwili yaliyojificha ndani ya utumbo aina zote.
 
Wanakuwekea drip kuondoa somo mwlini na madawa uliyotumia kabla
Wataalam wa afya hii imekaaje? Yaani kila mgonjwa akienda hospitali wana- kuflash sumu kwanza? Hizo gharama mbona itakuwa kubwa sana. Labda assume it's case by case. Hapo italeta maana.
 
Hiyo ya 12 upo sawaa kuna mmoja wao nilisoma nae elimu ya juu alikua na sura kavuu sanaa huwez tamn
 
Back
Top Bottom