Niliwahi kuachwa kisa kumtania mchumba

Niliwahi kuachwa kisa kumtania mchumba

zee_latown

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2026
Posts
562
Reaction score
1,024
kwema ndugu zangu? nilichokifahamu ni kuwa wanawake wanapenda sana utani na kutania, ila wao hawapendi kutaniwa... hawapendi kabisa.

enzi nikiwa kijana mdogo nakumbuka niliachwa na mchuchu ambaye tulipendana... sababu kuu ilikuwa si kubwa sana... bali siku hiyo nilimtania na nikamkazia sana kuwa amefanan na Hayati Mkapa kwa sura, yaani mpaka nikawa najua huenda ni baba yake mdogo...

na nikakazia huku nacheka sana... aisee alini mind na ukazuka ugomvi mkubwa sana uliopelekea kununiana na kuachana. nacheka sana nikikumbuka.

happy sunday
 
Hujua mindset ya mwanamke,hapo hukumtania ulimkejeli,haswa kama alikuwa ana karibia kufanana.

Katika kitu mwanamke anahangaika nacho hapa Duniani ni Uzuri wa Sura yake,wao wanaamini kwenye kitu chanya tu.

Mwanamke hata kama anajijua kuwa si mzuri kisura ,wee mwambie ni mrembo na ni mzuri mno,hapa atatabasamu na NAFSI yake itasuuzika.

Mwanamke hata avae nguo hazijampendeza wee mwambie amewaka na ametokelezea,hata akibisha basi mwambie umbo na shepu yake vimechangia mavazi yamkae,hata kama si kweli .
Kuna
Wanawake za watu wanaliwa si wote Wana njaa Bali Kwa kusifiwa na maneno madogo Sana.

Kwa mfano wanawake umri mkubwa
(Mishangazi) Ukitaka uwale kirahisi mno wee wasifie,waambie kuhusu Uzuri wao wee mwambie kuna wasichana umri mdogo wanazeeka lakini wao wako vilevile,hilo neno hasahau hata akiwa anaoga atakukukumbuka kila saa kete ya juu ya mwanamke ni kuhusu Uzuri wake.

Moja ya vitu vingi vinavyoua mahusiano tofauti na kipato ni wanaume kushindwa kucheza na maneno Kwa mwanamke.

Mwanamke ndiye mtu pekee ambaye haeleweki anataka nini sasa kama unadhani pesa zako pekee zitakupa wanawake si kweli,unaweza ukapata lakini usidumu nao.kila siku Una mwanamke mpya.

Tumeumbiwa kuwapenda wake zetu,halafu wao watuheshimu na si vinginevyo.

Unakumbuka siku umemiliki simu ya gharama Kwa mara ya Kwanza?

Vile ulivyoijali na kuipenda siku za mwanzo ndivyo siku zote ufanye hivyo Kwa mwanamke

Unakumbuka ulivyomiliki gari Kwa mara ya Kwanza? Ndivyo unapaswa kufanya hivyo Kwa mwanamke, mwanamke anakuacha kwasababu umezidiwa na Huyo jamaa mwingine.
 
Kwa mfano wanawake umri mkubwa
(Mishangazi) Ukitaka uwale kirahisi we msifie....


HAPA UKIWAFUNDISHA MADOGO WA UNDER 20 UTAUA KIZAZI MKUU. HII MBINU KWA MISHANGAZI UTAWALA MPAKA USIOWATEGEMEA KIFO TU KITAAMUA GEMU
 
Back
Top Bottom