Nilivyoshawishika kupima virusi vya UKIMWI

Nilivyoshawishika kupima virusi vya UKIMWI

Nilikuwa nikitamani kupima UKIMWI kila siku ila nilikuwa nikiogopa sana. Kila nikijitutumua kwenda kupima, weeee! joto la mwili hupanda na kichwa kinauma sababu ya wasiwasi! Basi siku ya siku iliwadia ambayo nilipata ujasiri wa kwenda kupima! nilienda kituo cha afya na kuelekezwa chumba muafaka.

Nilikutana na mtoa huduma na kumuelezea dhamira yangu ya kutaka kupima lakini nikashangaa ile hali ya kuogopa ikanijia tena. Nilimwambia mtoa huduma naogopa sana sijua itakuaje! Jamaa akaniuliza mara ya mwisho kuchepuka ilikuwa lini! Nikamjibu kama mwaka mmoja uliopita. Akaniuliza tena kwa nini unaogopa kupima!

Nikamwambia huwa najiuliza nikikutwa na ugonjwa nitakuwa naishi maisha ya kumeza vidonge kila siku ndicho kinachoniumiza. Dah jamaa akaniambia mbona kila siku unakunywa chai ya moto.

Pia akaniambia mbona kila siku ninakula matonge kama ya wali na ugali iweje uogope kumeza vidongo! Kwa kweli haya maneno yalinipa nguvu na imani ya kupima na majibu niliyapa.

Eeeeeh. mbona kawaida tuu kama kupima malaria? mie kila mwisho wa mwaka napma na nafrahya hivyooo maana ndio napata uhakika wa ntaishije.
 
Kwakuwa sipendi kutumia Condom, kila mpenzi wangu mpya lazima tukapime ngoma ndo nianze kusex nae. Na sijawahi kucheat, kwahyo najiamini sana.
Unahatari zaid ya kuambukizwa ukimwi kuliko kuambukiza!Wewe usipocheat mwenzio anaweza akazcheat.................
 
Kansa na malaria inaua kuliko ukimwi, tatizo Ukimwi ni ugonjwa wa aibu.
 
Umetuacha kwenye cliffhanger....labda kuna episode nyingine utatuletea sio?
 
Hapo kuna vitu viwili tofauti.msiba usikie kwa mwezio
 
ukimwi mara ya mwisho nilipimwa tena bila kujijua nilipoenda kufatilia vipimo kwa sababu ya kujiunga na masomo baada ya hapo sijawah kupima. maana nilicheza game nying peku ikawa navizia mwenzamgu anaenda kupima ananipa majibu yuko poa nami najifariji. maana watu kama
 
Unahatari zaid ya kuambukizwa ukimwi kuliko kuambukiza!Wewe usipocheat mwenzio anaweza akazcheat.................

Nafahamu hilo mkuu, ila ndo jinsi ilivyo hakuna njia nyingine.
 
Hujasema wakati unasubiri majibu ilikuwaje, maana hapo ndipo wengi husepa mazima
 
Back
Top Bottom