Nilikuwa nikitamani kupima UKIMWI kila siku ila nilikuwa nikiogopa sana. Kila nikijitutumua kwenda kupima, weeee! joto la mwili hupanda na kichwa kinauma sababu ya wasiwasi! Basi siku ya siku iliwadia ambayo nilipata ujasiri wa kwenda kupima! nilienda kituo cha afya na kuelekezwa chumba muafaka.
Nilikutana na mtoa huduma na kumuelezea dhamira yangu ya kutaka kupima lakini nikashangaa ile hali ya kuogopa ikanijia tena. Nilimwambia mtoa huduma naogopa sana sijua itakuaje! Jamaa akaniuliza mara ya mwisho kuchepuka ilikuwa lini! Nikamjibu kama mwaka mmoja uliopita. Akaniuliza tena kwa nini unaogopa kupima!
Nikamwambia huwa najiuliza nikikutwa na ugonjwa nitakuwa naishi maisha ya kumeza vidonge kila siku ndicho kinachoniumiza. Dah jamaa akaniambia mbona kila siku unakunywa chai ya moto.
Pia akaniambia mbona kila siku ninakula matonge kama ya wali na ugali iweje uogope kumeza vidongo! Kwa kweli haya maneno yalinipa nguvu na imani ya kupima na majibu niliyapa.