Nilivyoona katika safari yangu mkoa wa Rukwa

CPA

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
809
354
Mkoa wa rukwa ni moja ya mikoa iliyosahulika kabisa nchin tanzania. Barabara mbaya, umeme wa taabu, Katika safar yangu nilifanikiwa kupita wilaya ya sumbawanga, nkasi na mpanda kwa pinda. Miongoni mwa wilaya iliyosahaulika na ambayo watu wengi hawaifahamu ni wilaya ya nkasi(namanyere) wilaya hii inazaidi ya miaka 30, lakini hadi leo haina umeme. Wanatumia generator ambao unasambaza umeme kwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi tu. Kule maisha bora wanasikia kwenye redio. Pamoja na kuwa na utajiri wa asili kama mbuga ya wanyama ya katavi, maporomoko ya maji ya karambo, ziwa rukwa, ziwa tanganyika nk bado mkoa wa rukwa ni maskini wa kutupwa. Kunakiwanda kikubwa kimoja tu cha nyama cha mh.mzindakaya. Mkoa huu ndiko anakotoka waziri mkuu(w.mpanda), mh.mzindakaya(sumbawanga mjini) na mmiliki wa kampuni kubwa ya mabasi ya sumry. mohamed sumry(laela-sumbawanga). Kunabaadhi ya sehemu katika nchi umeme, lami mpaka vijijini. Lakini mkoa huu lami ipo kilomita 7 tu mkoa mzima. Je hii ni haki. Wafanyakazi wengi wakipelekwa wanakimbia.
Maswali ninayojiuliza. Híi miaka 50 ya uhuru inamaanisha nini kwenye baadhi ya sehemu? Huu ni mtazamo wangu tu.
 
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika haina maana kwa mtu wa kawaida. Wengi wa wananchi wanaishi kwenye umasikini uliokithiri. Ni aibu kujivunia miaka 50 ya uhuru wakati wananchi wamekosa tumaini.
 
mi nashangaa watanzania hawaandaman na hali yetu ni mbaya,ila wenye hali nzur kama libya ndo wanaandamana.
 
Bora ndugu yangu nawe umejionea hali ya huku kwetu, hapo ulipoona ni nafuu zaidi kuliko miaka 10 iliyopita!
 
Back
Top Bottom