GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,773
Wakuu,
Hii dunia ina mambo mengi sana, ndio maana tunatakiwa kufikiri kabla ya kutenda na hapa ndipo tunapotakiwa kukubali kuwa sio wote walioko magerezani wana makosa. Ni muda mrefu kiasi umepita lakini siwezi kulisahau tukio hili, Siku hiyo nilitoka nyumbani na kutembelea maeneo ya Buza Kanisani majira ya Saa 1.30, nilikuwa nimekusudia kwenda
kumuona mgonjwa maeneo hayo. Niliposhuka kwenye daladala nikavuka barabara nakuelekea Upande wa pili ambako kuna Baa na nyumba ya kulala wageni ambayo inaitwa Kilimanjaro.
Wakati nakatisha kwenye kichochoro cha ile Guest kuna mwanamke alikuwa anatoka mle guest, akafuata nyuma yangu kana kwamba tuko safari moja, mara nikasikia sauti nyuma yangu "Baba Moni hawa huku wanatoka" Ghafla yule mwanamke akachomoka kwa spidi kali na kunipita huku akifuatiwa na watu wawili ambao walitoka mbio kumfukuza mmoja
akaja kunishika mkono kwa nguvu huku akiporomosha matusi kuwa nitamtambua. Wakati huohuo wakaongezeka watu wengine watatu yule jamaa akasema mwangalieni huyo kwanza, kisha nae akakimbia kuelekea kule walikoenda wale wawili.Mwanzo nilikuwa sijaelewa nini kinatokea lakini Sekunde chache baadae nikafahamu kuwa niko kwenye Fumanizi.
Dakika chache baadae nikasikia yule mwanamke akilia hku kukiwa na hali ya wazi kuwa anaburuzwa au anapigwa.Wakuu sikuwa na lakufanya zaidi ya kujaribu bahati yangu, nilichomoka ghafla mikononi mwao na kuanza kukimbia kuelekea kichochoro ambacho kilikuwa kinaelekea upande wa kulia, sikujua naelekea wapi jamaa walijitahidi kunikimbiza huku wakipiga kelele, ninachoshukuru ni kuwa hawakuitisha mwizi. Namshukuru Mungu kwenye mbio niko vizuri, hivyo jamaa niliwaacha sana, nilipita njia nisizozifahamu nikakatisha kijimsitu fulani nikajikuta nimetokea Kitunda.Wakuu huu mkasa siwezi kuusahau maisha yangu yote, na toka hapo nimekuwa mwoga sana ninapopita kwenye vichochoro vya Guest.
Tuchukue tahadhari tunapopita maeneo hayo