Nilivyonusurika kwenye fumanizi

Nilivyonusurika kwenye fumanizi

Ahsante mkuu ni miaka minne sasa imepita dah!

Mkuu pole sana kwa tukio lililokukuta. Ninayahafahamu hayo maeneo so nimekuelewa vzr tena imebidi nicheke pia maana ni kama nilikuwa nakuona ukichanja mbuga. On a serious note, kumbe si mara zote tunatakiwa kujitetea maana kwa hapa ungeamua kujitetea pasipokukimbia, ukweli ungejulikana wakati una nundu tayari za kutosha tu kitu ambacho kisingesaidia.
 
duh! pole, maana ungedhalilishwa kwa makosa ya mwingine, ila usitamani mke wa mtu maana huenda ni tahadhari
 
Magazeti usikute ndiyo picha yenyewe hii manake nimeona inazunguka kwenye mitandao,hivi hawa wanaoandaa mitego ya kufumania wana akili sawasawa?


View attachment 251666

Hawa jamaa wabaya kweli .Hivi walitaka **** nanihi kweupe namna hiyo.
Mkubwa pole isijekuwa unatuzuga na mama msapti wako asije charuka kwa kuona hiyo picha?.

Ila mambo mengine hatari tupu?
Yaani sijui uso unauficha wapi kwa Watoto hapo nyumbani!
 
Duh pole sana, mimi niliwahi kufumaniwa aiseee, dah bahati nzuri aliyetufumania aliishia kuzimia! Sijui alikua mgonjwa au hasira hata sijui lakini tulisalimika.

Sawa wewe ulisalimika vipi mke wa jamaa hadi leo anaishi nae? Au jamaa alikufa moja kwa zote?
 
Sawa wewe ulisalimika vipi mke wa jamaa hadi leo anaishi nae? Au jamaa alikufa moja kwa zote?
oohhh sorry ukisoma post nyingine ndio nilikua nimeweka vizuri hili, yaani nilifumaniwa na Gf wangu mikiwa na rafiki yangu, aliezimia nii GF wangu back then, ila siku hizi nimezeeka.
 
Wacha kwanza ncheke..! Haaaaaaaah haaaaaaaaaah haaaaaaaah huuuuh..! Alafu nkupe pole sana Mkuu duuh soo ukiona guest ni kama umeona jani na ulikoswa na cobra..?
 
hahahahahahhahhahahhahahah!!! mbavu zangu nacheka kama mazur da! sijui atansemeje mana....? ivi unkulaga miguu ya kuk?
 
Inawezekana kabisa lilikuwa ni chezo hilo. Uswahilini wana tabia hiyo sana kutaka pesa, wala wasingekufanya kitu bali wangekutishia tu na kutaka pesa na wangekuacha ama kukuibia viatu, saa, n.k. Tabia hiyo ipo sana uswahilini, kuna ndugu yangu aliwahi kukaa Bar anamsubiria mwenzie, mara akatokea mdada na kuomba kukaa, ghafla akaanza kupaza sauti ya maneno kama haya 'utanilipa na leo nimekupata, ulidhani cha bure hiki na ulidhani sitakupata?!' Watu si wakaanza kujaa, jamaa akabahatika kukimbia, na ndiyo michezo yao. Ila Pole
 
Inawezekana kabisa lilikuwa ni chezo hilo. Uswahilini wana tabia hiyo sana kutaka pesa, wala wasingekufanya kitu bali wangekutishia tu na kutaka pesa na wangekuacha ama kukuibia viatu, saa, n.k. Tabia hiyo ipo sana uswahilini, kuna ndugu yangu aliwahi kukaa Bar anamsubiria mwenzie, mara akatokea mdada na kuomba kukaa, ghafla akaanza kupaza sauti ya maneno kama haya 'utanilipa na leo nimekupata, ulidhani cha bure hiki na ulidhani sitakupata?!' Watu si wakaanza kujaa, jamaa akabahatika kukimbia, na ndiyo michezo yao. Ila Pole
Duh inawezekana mkuu!
 
Pole mpwa sasa baada ya jamaa kuzimia ulikimbia au ulitoa msaada kwa aliyezimia.

Duh pole sana, mimi niliwahi kufumaniwa aiseee, dah bahati nzuri aliyetufumania aliishia kuzimia! Sijui alikua mgonjwa au hasira hata sijui lakini tulisalimika.
 
Wakuu,

Hii dunia ina mambo mengi sana, ndio maana tunatakiwa kufikiri kabla ya kutenda na hapa ndipo tunapotakiwa kukubali kuwa sio wote walioko magerezani wana makosa. Ni muda mrefu kiasi umepita lakini siwezi kulisahau tukio hili, Siku hiyo nilitoka nyumbani na kutembelea maeneo ya Buza Kanisani majira ya Saa 1.30, nilikuwa nimekusudia kwenda
kumuona mgonjwa maeneo hayo. Niliposhuka kwenye daladala nikavuka barabara nakuelekea Upande wa pili ambako kuna Baa na nyumba ya kulala wageni ambayo inaitwa Kilimanjaro.

Wakati nakatisha kwenye kichochoro cha ile Guest kuna mwanamke alikuwa anatoka mle guest, akafuata nyuma yangu kana kwamba tuko safari moja, mara nikasikia sauti nyuma yangu "Baba Moni hawa huku wanatoka" Ghafla yule mwanamke akachomoka kwa spidi kali na kunipita huku akifuatiwa na watu wawili ambao walitoka mbio kumfukuza mmoja
akaja kunishika mkono kwa nguvu huku akiporomosha matusi kuwa nitamtambua. Wakati huohuo wakaongezeka watu wengine watatu yule jamaa akasema mwangalieni huyo kwanza, kisha nae akakimbia kuelekea kule walikoenda wale wawili.Mwanzo nilikuwa sijaelewa nini kinatokea lakini Sekunde chache baadae nikafahamu kuwa niko kwenye Fumanizi.

Dakika chache baadae nikasikia yule mwanamke akilia hku kukiwa na hali ya wazi kuwa anaburuzwa au anapigwa.Wakuu sikuwa na lakufanya zaidi ya kujaribu bahati yangu, nilichomoka ghafla mikononi mwao na kuanza kukimbia kuelekea kichochoro ambacho kilikuwa kinaelekea upande wa kulia, sikujua naelekea wapi jamaa walijitahidi kunikimbiza huku wakipiga kelele, ninachoshukuru ni kuwa hawakuitisha mwizi. Namshukuru Mungu kwenye mbio niko vizuri, hivyo jamaa niliwaacha sana, nilipita njia nisizozifahamu nikakatisha kijimsitu fulani nikajikuta nimetokea Kitunda.Wakuu huu mkasa siwezi kuusahau maisha yangu yote, na toka hapo nimekuwa mwoga sana ninapopita kwenye vichochoro vya Guest.

Tuchukue tahadhari tunapopita maeneo hayo

Maskiniii!, pole sana mkuu hiyo ni kali mno. Yaelekea huyo mfumaniwa wa kike alikuwa anauza kwa kila mtu ndomana wale jamaa walikuhisi.
 
Hapana Mpwa, nilijitahidi kuyamaliza, uzuri ni kwamba nimefumaniwa na GF nikiwa na mwanamke mwingine, kwahio kile kiwewe ndio akazimika. Ila usiombe mtu azimike mbele yako....

Wewe vipi sasa uko nako unaita kufumaniwa!
 
Back
Top Bottom