Nilivyonusurika kuambukizwa UKIMWI

Nilivyonusurika kuambukizwa UKIMWI

Baada
sijataka unitukane wala sihitaji maoni yako, wala ukinitukana hainisaidii wala kupunguza chochote. kikumbwa nimejitambua na Mungu ameninusulu dats all.
Baada ya kufanya ujinga ndo ukagundua tatizo lako,ama kweli kama wadada mpo hivi mbona mnakatisha tamaa sana maana,mna tamaa mno za fedha daaah umefanya niumie Moyo,kwa kweli Mungu tusaidie
 
Wewe unauogopa ukimwi wa karne ya 21 ambao hata mtu akiupata anadunda tu mtaani huku akimeza dawa zake za ARVs kama hapendi vile na kuishi miaka chungu nzima! Ukimwi ni ule wa miaka ya 80's na 90's ambao haukuwa na dawa wala tiba.

Usisherehekee ushindi mapema kabla ya kuondoka hapa duniani. Kuna njia nyingi za kuupata ikiwemo ile ya kupitia kwa huyo mume wako mtarajiwa! Jambo la msingi ni kumuomba tu Mungu akupe maisha marefu.
 
Hatar Sana
tapatalk_1564845577269.jpeg
 
Sijasema about money maana hata mimi nimezaliwa katika familia ya waziri, sikuwahi kuijua shida ni kitu gani ila kilichonisumbua ni ujana ( Otherwise haya yalishapita) au unataka nikuwekee na cv yangu hapa? siyo kila mtu anadate na mtu just for money?
CV yako mimi siihitaji, kumbe mtoto wa getkali kitambo..duh! Wanawake bana
 
kwhyo ARv ndio anafata ulaya?

au kuna matibabu mengine ya HIV ambayo sijui
any way isitoshe risk ya kupata HiV through sexual intercourse haizid 0.5% lakin rate ya maambukizi mapya inaongezeka exponentially

hapo ndio namkubali deception kuwa hakuna HiV/AIDS na HiV haiambukizwi kwa njia ya sex
 
AMINA
Wewe unauogopa ukimwi wa karne ya 21 ambao hata mtu akiupata anadunda tu mtaani huku akimeza dawa zake za ARVs kama hapendi vile na kuishi miaka chungu nzima! Ukimwi ni ule wa miaka ya 80's na 90's ambao haukuwa na dawa wala tiba.

Usisherehekee ushindi mapema kabla ya kuondoka hapa duniani. Kuna njia nyingi za kuupata ikiwemo ile ya kupitia kwa huyo mume wako mtarajiwa! Jambo la msingi ni kumuomba tu Mungu akupe maisha marefu.
AMINA UMESEMA VYEMA
 
Aisee haupo peke yako mimi pia nimenusurika kuungua kama mara 2 hivi. Ipo hivi demu wa kwanza alinisumbua sana, siku alipojilegeza kuja geto, mzee baba nikaondoa kifuniko kwanguvu(kyupi) nikapiga kimoja takatifu kavu kavu.Baada ya siku nikamuomba game irudiwe, hapo mzee nikaandaa vipimo, alipokuja nikampima majibu HIV+.Daah!! Akili ziliniruka sana ila ikapita miezi 3 nikaenda pima nikajikuta nipo pw yaani HIV-.


Ya pili sasa, huyu ni demu wng wa muda, mwanzoni tulikuwa tunatumia kinga ila mwishowe mazoea yakazidi, mjomba nikaanza kupita naye kavu kavu yaani nyama nyama.Aisee kumbe yule dada ni victim muda tu anatumia dawa sema alikuwa ananificha, nilikuja kujua baada ya watu kumzungumza kwamba kaungua muda tu.Daah!! Ila nayo baada ya miezi 3, nkapima nmekutwa HIV-

namshukuru mungu sana kwa upendo!!
 
Asante sana, Kwa sasa sihitaji mwanaume bado nafurahia miujiza alonifanyia Mwenyezi mungu
Pole na hongera. Hata hivyo taratibu za upimaji wa HIV zinataka upime angalau mara tatu kila baada ya miezi mitatu. Hapo ndipo unaweza kusema kwa uhakika kuwa umenusurika.

Vv
 
Natamaniii nitukaneeeeeeeee ma.ma........eeeeee khaa we ni m.a.l.y.a ,n.I.a.n.g.u.s.a.ge
 
Pole na hongera. Hata hivyo taratibu za upimaji wa HIV zinataka upime angalau mara tatu kila baada ya miezi mitatu. Hapo ndipo unaweza kusema kwa uhakika kuwa umenusurika.

Vv
hiyo miezi mitatu kama sishiriki ngono zozote nitaupata kwa njia gani zingine?
 
polepole dada, so ulikuwa na mchumba wako na bado ukagawa mwili wako kwa mheshimiwa? hiyo tabia ninakokaa tunaita umalaya sijui kwenu wanaitaje..... Pili huyo mchumba wako ndiyo amefaidika na huo uamuzi wako, maana alikuwa anamahusiano na mtu asie jielewa kabisa wakuitwa chawote.....mwisho unakazi ila unatamaa sana ya maisha ambayo sio kiwango chako, ndo maana ulitembea na mheshimiwa hiyo tabia mtaani kwetu pia tunaita umalaya sijui kwenu wanaitaje..... Kama wanawake wote wapo hivi basi kuoa ni jambo la kipumbavu sana......
Yupo cheap sana..! Hata huku kwetu tunawaita hivyo hivyo mkuu
 
Unblock hiyo number,mzee hawezi kukuambukiza maana anakunywa dawa,pili kuna condom za kike unajivalia zako unaenjoy pesa za awamu ya tano.
 
Muheshimiwa bado yupo bungeni????mpaka sasa
Hi guys
I hope mko vizuli,
Mimi siyo mgeni huku kama ambavyo mmeniona ila hii id ni ngeni, nimeamua kuficha jina halisi ili niwe huru kushare hili jambo langu ambalo nimekuwa nikitamani niseme ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniokoa na janga hili.
Awali mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 27 nipo kwenye ajira Wizara flani huu mwaka wa 2.
Ilikuwa mwaka jana December ambapo nilipata ka semina Fulani nje, nikiwa safarini nikutana na Waziri mmoja mtu mzima kidogo ( tukasalimiana, of course yeye hakujitembulisha maana ni maarufu ila mimi nilijitambulisha baada ya kusalimiana) tukabadilishana mawasiliano.
Baada ya kuludi nchini tuliendelea kuwasiliana. Siku moja akiwa kikazi Dodoma aliniomba anikatie ticketi ya ndege nifike Dodoma mara moja tukaongee jambo. Siku hiyo nilikuwa bored kiaina nikakubali wito.
Niliondoka kesho yake nikafika Dodoma dereva wake akawa amekuja kunichukua akanipeleka katika makazi yake pale Dodoma. Baada ya kufika kwake nilikaa kidogo nae mwenyeji wangu akawa amefika.
Tuliongea mambo mengi na mvinjo kidogo jamaa akaniambia amenipenda sana ( japo anayo familia) akaniahidi mambo mengi ( sikumbuki ilikuwaje lakini nilijikuta nikifanya mapenzi na huyu mheshimiwa) bao 2 taam sana.
Tukaagana yeye alipata dharula akaondoka kwenda mkoa wa jirani ila akanicha hapo kwake nikalala kesho yake nikachukuliwa na dereva airport nikarudi zangu dar.
Tuliendelea kuwasiliana hapa jamaa ilikuwa kama kakolea maana alionesha kunijali sana. Baada ya siku mbili alisafiri akaenda nje ya nchi. Tukawa bado tunawasiliana vizuri tu
Nakumbuka nilichukua namba ya simu ya dereva wake na siku moja akawa amenipigia tukapiga stori mbili tatu basi ikawa tunasalimia tu. Nakumbuka siku moja huyu kijana aliniambia ( Mheshimiwa anakupenda sana lakini kuwa makini linda afya yako)Mzee huwa anaenda nje ya nchi kutibiwa ( na hii ni siri kubwa ila mimi naijua nimekuambia maana nakupenda) Nikaamua nichunguze maana maneno hayatoshi kujiridhisha.
Nikaendelea kumchunguza huyu jamaa na picha alikuwa ananitumia lakini niligundua kitu kwamba ana ugonjwa ila sikujua ni ugonjwa gani maana kisukari wala presha hakuwa navyo ( Nikagundua ni mwathirika wa H.I.V) nilichanganyikiwa sana nikapunguza mawasiliano nae, mwishowe nikaamua nimblock kila sehemu.

Baada ya miezi minne kuisha nikaanza kupatwa na homa za ajabu ajabu hapa nikajua teyari nimeshaanza kuumwa. Nililia, nikapauka hata kazi zangu za ofisini nikawa sifanyi kiufasaha.

Niliwaza sana hatimaye siku moja nikaamua niende kupima alafu nianze kutumia hizo dawa.
Kufika maabara nikapima, lahaulaaaaaaa, nikawa nipo safi, nililia mbele ya Yule daktari machozi ya kutosha, nikamuomba anipime mara ya pili akapima, nikawa nipo mweupe kabisaaa .
Hii siku sintaisahau katika maisha yangu, ilikuwa siku ambayo nilirudisha matumaini ya kuishi

Kuanzia siku hiyo nikapona vihoma homa nikawa mtu mpya kabisa. ( Hata mchumba wangu ambaye nilikuwa nae nikaamua kuachana nae hadi pale Mungu atakaponipa mume) nilimwambia tu kama unanihitaji fanya unioe full stop.), niliahidi kutokufanya mapenzi tena hadi nikiwa kwenye ndoa ndivyo nilivyomwahidi Mungu.

Lengo la huu uzi ni kukumbushana tu kuwa Ukimwi upo, lakini kwa hili Mungu ameniokoa
Jina la Bwana libarikiwe!
 
hiyo miezi mitatu kama sishiriki ngono zozote nitaupata kwa njia gani zingine?
Hii ni kwa kuwa mara nyingine virusi huchukua muda sana hadi kuja kuonekana. Kama hujawahi kushiriki ngono baada ya lile tukio, baada ya miezi mitatu ndio muda mwafaka kujua kwa uhakika kama unalo tatizo au umenusurika.

Vv
 
Back
Top Bottom