Nilivyokutana na Msukuma kwenye msitu wa Malangamilo

Kadagaa

Member
Jan 24, 2018
9
17
NILIVYO KUTANA NA MSUKUMA KWENYE MSITU WA MALANGAMILO

ILIKUWA JUZI TU yaani usiku wa kuamkia Jana Kabla ya hakujakucha.... Hakuja pambauzika, usiku wa siku hiyo, niliomba Dua kwa sir God aniamshe mapema sana kwani ratiba yangu Ilikuwa tight...

Kweli bwana Mungu yupo wazeee, na anajibu maombi. Huwezi amini akajibu ile Dua....Saa Kumi na Moja alfajiri imenikuta nipo macho...Sina hata lepe la usingizi.

Tofauti na Dar es salam Mikoani huku saa Kumi na Moja alfajiri Kuna giza la haja tena la kutosha tu...

Yule muhenga aliyeleta ule msemo Kwamba: Ukiona giza linazidi ujue mapambuzuko yamekaribia nadhani alifanya utafiti wa kutosha.... alfajiri yenye giza mkoa wa Mbeya ni giza kweli.

Hivyo nikaendelea kuvuta time kitandani Ili kupambazuke, tayari kwa safari ya kijiji Cha MALANGAMILO. Ndani ndani kabisa....

Ilipotimu saa Kumi na mbili asubuhi juu ya alama....

Nakwenda maliwato kwa ajili ya haja na kujiswafi kisha narudi chumbani....Navaa chap na haraka kisha naitoa 'chopa yangu' chopa bwana ni pikipiki fulani hivi bovu bovu huku tunayaita 'chopa'😆

Baada ya hapo napiga kiki, tayari kwa safari ya MALANGAMILO ajabu chopa inagoma kuwaka, napiga kiki kama tano za mfululizo chopa haioneshi dalili.

Pikipiki mbovu mbovu hizi miyeyusho sana, mwanaume nakandamiza kiki kama ishirini na usheee. Chombo kina goma kabisa kunitiii dereva.

Nachunguza plag kama iko vizuri, pia nacheki 'wese' labda pengine lilikwisha hata hivyo naona kila kitu kipo poa.

Tatizo ni nini sasa.????

Napandisha choki. Napiga kiki zaidi, ngoma inagoma kabisa.... Naghafirika, nasikitika, nahuzunika... Hii pikipiki inanichelewesha dili la hela huko MALANGAMILO.

Nacheki time, ni saa Kumi na mbili kama na nusu hivi...Muda unakwenda mbio sana.

Yanii kufumba na kufumbua nishapoteza kama nusu saa nzima, nifanyeje?? najiuliza.

Chap nampigia Simu George Mlewa, Mimi napenda kumwita Mkandawile, huyu dogo ni mtukutu sana, mtu wa gambe, hana baya na mtu, halafu ni boss wangu hamuwezi kuamini. 🤣🤣

"Katalambula," anapokea simu kwa mtindo huu.

"Chopa inazingua kuwaka nusu saa nzima. sijaondoka hadi sasa."

"Oooh shit hujaondoka tu, sasa itakuwaje?"

"Hapa lazma nisubiri hadi saa Moja nipeleke kwa fundi, pale kwa bonge."

"Nalichukia sana chopa lako. this time ukipata hela fanya ununue chombo kipya."

"Hahaha inshallah boss, I will do."

"Kaza na huo mnyororo ikibidi nunua spoket mpya."

"Haina kwere Mkandawile."

Nakata simu kisha nasukuma chombo kwenda gereji. Bahati nzuri gereji kwa bonge pale kituo Cha mafuta Cha Samora tayari Jamaa alishafika.

Ananipokea, anaichunguza pikipiki, anachokonoa hapa na pale, kisha bonge anapiga kiki Moja tu chopa inawaka kwa kishindo kama helkopta ya Chadema. 🤣

Nalipa malipo, kisha safari ya MALANGAMILO inaanza. Nakwenda kwa kasi kidogo, kwani niko nyuma ya muda. Pikipiki inapiga makelele kama dege la jeshi la JWTZ.

dakika tatu nikawa tayari nimeachana na barabara ya lami, sasa nipo kwenye njia ya vumbi. chombo kinapepea kama tiara. MALANGAMILO lift valley' ni mbali bwana weee bila kukimbia nitafika kesho🤭

Kama nusu kilometer naachana na barabara ya vumbi, nakunja kulia na kumshika kanjia kadogo, siwezi kwenda na barabara kubwa kwani mbele mita kama mia mbili huwa Kuna geti la polisi, wale Jamaa wako kazini wanaisaka pesa usiku na mchana na Mimi Sina pesa, hivyo naingia chocho.

Safari ya MALANGAMILO ndio kwanza imeanza.

itaendelea.

Bonyeza kiungo kusoma inayoendelea

Sehemu ya pili
 

Attachments

  • FB_IMG_1656875233288.jpg
    FB_IMG_1656875233288.jpg
    91.5 KB · Views: 25
Sawa tupo kuisubiri..chamsingi usituache njiani kama mpwanyungu.

#MaendeleoHayanaChama
 
jf inakuwa ya hovyo sana siku hizi.

mods nao ukiwaeleza kuhusu hizi kero wala hawana habari.
 
Back
Top Bottom