Habari zenu wandugu,
Poleni kwa majukumu ya hapa na pale.
Ijumaa ya tarehe 13 mwezi huu niliamua kwenda kupima Afya yangu hususani VVU kwani nilikuwa na wasi wasi uliosababishwa na ndoto iliyojirudia kama mara 3.Nilifika katika Zahanati 1 hapa jijini ambayo ina huduma ya vijana ya kupima na ushauri nasaha.
Kipimo cha kwanza kilitoa majibu ambayo hayakueleweka. Kile kimstari kinachoonesha kama mtu kaathirika hutoa rangi fulani endapo uko Positive.Kile kimstari kilikuwa kimefifia, hali iliyopelekea kuchukuliwa Kipimo cha aina nyingine.Kipimo hiki cha pili kikaonesha niko Negative.Daktari akashauri nirudi baada ya wiki mbili kwani majibu yanapishana,inabidi waangalie mgongano wa vifaa hivyo.
Cha kwanza hakijatoa jibu, cha pili kimetoa jibu.Hizi wiki mbili tu nimekata kilo nyingi kwa mawazo, nilijikuta nafikiria majibu yale ya kipimo cha kwanza yasiyoeleweka. Nikafikiri vipi kama baada ya wiki mbili ikawa confirmed ni Positive nitaishije mie.
Leo nimeenda ikiwa ni wiki mbili tayari.Dokta kaniambia ingia maabara,akatoa maelezo kwa mtu wa maabara juu ya kilichotokea mwanzo.Nikatolewa damu,baada ya hapo nikaambiwa nisubiri nje. Jasho kila mahali, mapigo ya moyo yakiwa juu, Usiombe hali hii ikukute, unaweza dondoka kwa pressure.
Baadae nikaitiwa majibu yangu, Dokta kaanza kwa kunipa Hongera na pole kwa kilichotokea wiki mbili ilizopita kwani majibu yanaonesha nipo Negative. Nilijihisi kuongezeka kilo kadhaa hapohapo.Njia nzima nilikuwa nikiimba sifa na ukuu wa Mungu.
Zipu haishushwi tena hadi siku iliyokusudiwa.
Namshukuru Mungu hata sasa.
UKIMWI upo na unauwa, usiombe hii hali ya sintofahamu ikutokee.