SEHEMU YA KWANZA: NILIVYO KUTANA NA JINI WA UTAJIRI WA MATESO
Hadithi ya Kweli ya Dogoli Kinyamkela – Mgeta, Morogoro
Yalipo nikuta Aya majanga.
Nilizaliwa katika kijiji kidogo cha Mgeta, kilichozungukwa na milima, misitu mikubwa na mito yenye maji baridi kama roho ya mtoto mchanga. Nikiwa kijana mdogo, nilikuwa maskini wa kutupwa yaan choka mbaya mno, nikiwa sina cha kutegemea zaidi ya kazi za mikono za wazazi wangu. Lakini tangu nikiwa na miaka 15, nilianza kuona ndoto za ajabu—ndoto zilizojaa mapicha ya miali ya moto, majumba ya dhahabu, na mwanamke mrembo asiye na kivuli. Nilijua haya hayakuwa ndoto za kawaida.
Miaka miwili baadaye, nikiwa na umri wa miaka 17, nilikwenda kutafuta kuni kwenye msitu wa Mgeta – sehemu ambayo wazee walituonya tusikaribie jioni. lakini hamu ya kuota moto jioni ilinivutia zaidi. Wakati nikikata mti wa mkaratusi, upepo ulianza kuvuma kwa nguvu isiyo ya kawaida. Miti ilianza kulia kama watu. Niliposimama kutazama, alitokea mwanamke mrembo zaidi ya wote niliowahi kuona (alikua pisi ya kwenda)– ngozi yake nyeusi yenye kung’aa kama samli ya usiku, macho mekundu kama makaa ya moto, na nywele ndefu zilizoshuka hadi miguuni.
Alinitazama kwa macho yaliyopenya ndani ya nafsi yangu. (Nilianza kuwaza jinsi nitakavyo ichakata mbususu yake 😂😂) Bila kuzungumza, nilihisi moyo wangu ukianza kudunda kwa kasi. Alijitambulisha kwa jina la Zubeda, akasema yeye si mwanamke wa kawaida, bali ni jini wa kizazi cha Mkinyonga. Alijua jina langu, ukoo wangu, na hata mawazo yangu ya ndani. Nilihisi hofu na mvuto kwa wakati mmoja. Sauti yake ilikuwa ya kuvutia, laini kama (kama mshangazi na cc muhando😂😂😂)
Zubeda aliniambia kuwa nimechaguliwa kuwa mpenzi wake wa kibinadamu. Aliniambia nitapewa utajiri mkubwa, lakini kwa masharti matatu:
1. Sitakiwi kumpenda mwanamke yeyote wa kibinadamu.
2. Kila mwezi wa mwisho, nitatoa sadaka ya damu ya mnyama.
3. Kamwe nisiulize yeye anatoka wapi au kifo chake kilikuaje.
Niliporudi kijijini usiku huo,nilishangaa sana, nilikuta nyumba yangu imejaa pesa. Vifurushi vya noti na dhahabu vilikuwa kila kona. Sikuamini. Nilikuwa tajiri wa ghafla, watu wote walinianza kuniita Dogoli Tajiri. Lakini kila kitu kilianza kubadilika taratibu. Kila nilipojaribu kutoka na mwanamke wa kawaida, usiku nilikuwa naota chululu yangu inaungua. Waliojaribu kuwa karibu nami walipata ajali, au walikufa kwa njia za ajabu. Zubeda alitawala kila kipengele cha maisha yangu – usiku aliniita kitandani, mchana alinitokea katika vioo, na alinichoma kwa mapenzi yake matamu japo ya maumivu.
SEHEMU YA PILI: MATESO YA MAPENZI NA UTUMWA WA KIROHO
Maisha yangu yaliendelea kubadilika kwa kasi. Ingawa nilikuwa tajiri, ndani ya moyo nilikuwa masikini. Zubeda alinipenda kwa njia ya kuumiza. Sikuweza kula vyakula vya kawaida tena – nilianza kula damu na nyama mbichi kwenye ritwali zetu. Kila mwezi, nililazimika kuchinja mnyama – mbuzi, kuku mweusi au paka mweupe – na kumwaga damu mlangoni mwangu. Usipofanya hivyo, usiku unakuja na ndoto za kifo, sauti za kulia, na viumbe wanakuandama hadi unatokwa na damu puani.
Nilipojaribu kumuacha, nilipata homa ya ajabu iliyonifanya nilale wiki tatu. Wataalamu wa hospitali hawakugundua tatizo lolote. Nilijua ni yeye. Nilipoamka, nilimkuta amelala pembeni yangu – si kwa mwili wa mwanamke tena, bali kwa umbo la kiumbe mwenye miguu ya mbuzi, macho manne, na mkia wa nyoka. Alinichoma alama kwenye kifua changu – alama ya umiliki.
Miaka ilipita. Nikawa tajiri sana – apa sasa nikahamia Jiji la starehe nikajenga nyumba Dar, magari ya kifahari, pesa zisizoisha. Lakini nilikuwa mpweke. Kila nikicheka, kulikuwa na kilio moyoni. Nilijaribu kutubu kwa waganga wengine, lakini hakuna aliyeweza kunitoa kwa Zubeda. Mmoja wao alijaribu, lakini alikufa usiku huohuo.
Ile Hali ilinichosha Siku moja nilipanga safari kurud kijijini kuongea na zubeda kipenzi, niliketi msituni Mgeta, mahali tulipokutana mara ya kwanza. Nikamwita. Alitokea tena. Nilimwambia sitaki tena utajiri wa mateso. Alinitazama kwa huzuni halafu akasema:
“Dogoli, uliniita mwenyewe kwa tamaa yako. Sasa umetaka kuondoka. Lakini kumbuka, damu iliingia mkataba. Hutaondoka hadi mtoto wa damu yako achukue nafasi yako.”
Nikashangaa. Mtoto wangu wa kwanza ambaye alikuwa na miaka 5 alianza kuumwa ghafla – akawa anaongea maneno ya ajabu, na usiku anaota ndoto kama zangu. Ndipo nikajua, mkataba wa jini hauishii kwa maneno tu, bali kwa kizazi.
Niliapa kumaliza hii laana. Nilianza safari ya kujitakasa( kujitoa Kwa zubeda), lakini iyo ni sehemu ya
tatu…..............
Usikose........