malimingiii
JF-Expert Member
- Nov 20, 2013
- 968
- 1,343
Big up sana mzizi mkavu
Nice story, imemalizika vzuri tofaut na story kazaa nilizowahi kuzipitiaAsante mkuu
Nice story, imemalizika vzuri tofaut na story kazaa nilizowahi kuzipitia
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Niliuwa kwa kukusudia-36-
Sikuwa na wazo lingine muda huo, nilimchukua mwanangu nikidhamiria kuondoka haraka mahali hapo, lakini kabla sijafika mbali nilikiona chakula kikiwa mezani. Kwa jinsi kilivyokuwa kimewekwa nilitambua kwa vyovyote Elhakim alikuwa akijiandaa kula.
Akili yangu ilifanya kazi kwa kasi. Kwa kuwa sikuwa mgeni wa nyumba ile, haraka niliingia chumba cha stoo na kuchukua sumu ya panya katika moja ya masanduku ambayo niliyakumbuka vyema.
Kwa bahati nzuri niliiona, nikaichukua kisha nilienda moja kwa moja nakuichanganya sumu ile kwa wingi katika chai ya Elhakim. Sekunde chache baada ya kufanya hivyo nilimsikia Elhakim akizungumza na simu akitokea jikoni, nikaondoka haraka mezani hapo na kwenda kukaa kwenye sofa nikijifanya namnyonyesha mwanangu.
Bila kushtuka Elhakim aliketi mezani na kula chakula chake huku akishushia na ile chai niliyoijaza sumu. Sikumsumbua mpaka nilipohakikisha kuwa amemaliza kunywa ile chai.
Kama kawaida yake aliponiona tu aligeuka mbogo na kunifukuza nyumbani kwake kwa ukali tena kwa wakati huo alikimbilia ndani na kuichukua bastola yake akitishia kuniua.
Kwa kuwa niliogopa, niliamua kuondoka zangu na mlinzi wake aliniona nikitoka na bosi wake akirudi ndani salama salimini. Nilirudi baada ya dakika chache nikimsihi mlinzi wake aniruhusu niingie ndani lakini alinikatalia. Lengo langu wakati huo halikuwa kuingia ndani kweli, bali kuhakikisha kama nimeshammaliza.
Kwa macho ya uwongo nilimsihi sana mlinzi yule angalau aniitie Elhakim mwenyewe aje nje nizungumze naye. Baada ya kumuomba sana yule mlinzi alinionea huruma na kuamua kwenda kuniitia bosi wake.
Nakumbuka alinijibu kwamba, bosi wake alionekana amechoka sana kwani alimkuta amelala bila hata kumalizia chakula chake pale mezani, hivyo hawezi kumsumbua kwa ajili yangu.
Kwa maelezo hayo nilitambua kuwa tayari ile sumu ilikwishafanya kazi yake. Niliondoka zangu nikishangilia ushindi mkubwa. Sikujua nini kilichokuwa kikiendelea humo ndani, lakini nilikuwa na uhakika kuwa Elhakim ameshakufa muda mchache baada ya mimi kuondoka.
Siku mbili baadaye nilisikia kuwa kuna msichana amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua Elhakim. Hiyo ndiyo ikawa mara yangu ya kwanza kuingia mahakamani na kukutana na kesi hii. Kwa nilivyosikiliza niligundua kuwa mtu anayeshtakiwa yaani huyu dada hapa (huku akininyooshea mimi) aliipiga risasi maiti ya Elhakim lakini siyo Elhakim. Elhakim nilimuua mimi, alimaliza Jamila.
Kwa maelezo yale, miguu yangu iliisha nguvu nikajikuta nikikaa chini kama mzigo. Nilipopata nguvu nilijitahidi kuvuta kumbukumbu zangu vizuri. Kweli siku ile nilipofika nilimkuta Elhakim akiwa amelala sikumuangalia kama alikuwa mzima au la. Bila kuchelewa nikammiminia risasi papohapo, hivyo kwa maelezo yale ya Jamila huenda kweli Elhakim hakuwa kama nilivyofikiria awali, hakuwa amelala bali alikuwa amekufa.
Baadaye nilirudishwa gerezani huku wakili wangu aliyekuwa akinitembelea gerezani karibia kila siku, akinieleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu kesi yangu. Kwanza aliniambia kuwa mwili wa Elhakim ulikuwa umefukuliwa ili kufanyiwa uchunguzi tena. Matokeo yalionesha kuwa kweli Elhakim alikuwa amefariki dunia kutokana na sumu kabla hajapigwa risasi, hivyo niliambiwa ningeweza kuachiwa huru maramoja kuanzia siku hiyo.
***
Siku chache baada ya kutoka gerezani nilisikia kuwa Jamila amefungwa na anatumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuua kwa kukusudia, bila shaka hiyo ndiyo adhabu ambayo ingenikuta mimi.
Baada ya miaka miwili nikiwa katika matembezi yangu ya kawaida nilimuona Jamila akiingia ndani ya nyumba moja nzuri sana karibu kabisa na nyumba niliyokuwa nikiishi mimi.
Sikuamini kabisa kwa kuwa nilijua Jamila alikuwa gerezani, akitumikia kifungo cha maisha.
Nilijaribu kumfuata na kumuulizia ndani ya nyumba ile lakini walisema kuwa hakukuwa na mtu kama huyo.
Sijui kama waliniambia ukweli au waliniongopea, lakini nilikuwa na uhakika kuwa niliyemuona alikuwa ni Jamila kwa kuwa sikuweza kabisa kuisahau sura yake na haiba yake ya ujasiri.
Nikaamua kuyaacha mambo hayo kwa kuwa tayari nilikuwa nimeshaanza maisha mapya na kuhusu Elhakim, nilikuwa nimeshamsahau, au labda ningemkumbuka sana kama mwanangu angefanana naye, lakini namshukuru Mungu aliniepushia hilo, mwanangu alikuwa amefanana kila kitu na mimi.
MWISHO '' THE END''