Mliowahi kupata wanawake/wanaume Jamii Forums, mje kutoa ushuhuda hapa ili na sisi tunaotafuta tupate morali ya kutafuta zaidi

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
Toka nijiunge JF miaka kenda sijawahi kuona thread yoyote ya kutoa pongezi kuwa mwanamke/mwanaume kapata mchumba humu Jamii Forums.

Huko kwenye jukwaa la love connect kuna nyuzi nyingi sana za wadada /wakaka wakitafuta wenza wao, tena wengine wakilalamika kabisa kuwa wameshaandika mara nyingi bila mafanikio yoyote.

NALIA NGWENA aka afsa ubashiri kama wanavyoniita huko Jukwaa la Michezo, na mimi niliona niandike uzi wa kutafuta rafiki/mchumba ili aje kutuliza moyo wangu na mimi mgumu nisuuzike nafsi.

Lakini Mambo hayakuwa kama nilivyotegemea /juhudi zangu ziligonga mwamba sikuona chochote kule Private message (PM) kiufupi ni empty set tu.

Nilibadili gia nikaona labda wadada hawataki bado wanakula ujana, nikachenji gia nikaandika namtaka mama wa makamo lakini juhudi zangu hazijazaa matunda sijaona chochote Pm, zaidi ya kushambuliwa na vijana wa hovyo wakisema kuwa nataka kitonga/ mama wakunilea ili apunguze ukali wa maisha yangu.

Kama Kuna wadada/wakaka walishafanikiwa kupata wachumba humu waje hapa wanipe morali mgumu NALIA NGWENA na wenzangu tunaotafuta mbususu humu kwa udi na uvumba ili tutulize mioyo yetu swafi kabisa, waje kutoa ushuhuda hapa, au hakuna kinachoendelea humu nikucholana tu nakuchekana tuambiane tujue jamani.
 
Namma unaandika thread yako ni inajieleza wewe ni mtu wa aina gani.
Ingawa tumefichwa na fake names pamoja na avatar.
Lakini tone ya maandishi yako inaelezea kinaga ubaga u mtu wa aina gani.

Na wadada wengi kabla hawajaja PM lazima aangalie na thread zako zilipota u unachangia mada gani,unatumia maneno gani.
Unaonekana haupo serious ndo maana haupati mtu serious.

Mimi nilikutana na mkaka umu ndani,mkaka mtanashati,mastaharabu ana utani kidogo,namna thread yake ilivojieleza ndivyo alivyo kwa mara ya kwanza kuonana tukapendana na mpaka sasa tupo wote.Bado kula pilau tu.

Yangu ni ayo mkuu.
 
Back
Top Bottom