Nilisalitiwa miaka 12

Nilikuwa na mchumba niliyetarajia kufunga nae ndoa 2002 lakini ghafla alinikimbia.Sasa hivi ananipigia simu akitaka ni msamehe na turudiane na mimi sasa hivi nina mke na kila nikimwambia hanielewi nifanyeje?

Watu wengine mnashangaza sana. Kwani inalazimu wapi yeye akuelewe? Kwa hiyo anakuendesha au? Wakati anakuacha hiyo miaka 12 alikuaga na ww ukamuelewa au alienda tu na wewe ukalazimika kukubali?
 
kwa kipindi kile alikukimbia baada ya kuona uchumi wako mbovu,sasa hivi anakutaka sababu ya uchumi wako umeakaa sawa.
 
emu acha ubabaishaji,wewe umeoa unataka nini tena,hapa hamna deni inasemaaje,lazima uwe na mtazamo endelevu na ndoa,duh!
 
miaka 12 its long time bro! afu wewe kama una mke unatafuta nini? yeye kaachwa huko ndo maana anakutaka.
 
muambie mkeo akusaidie kumuelewesha, najua ataelewa tu.
 
humu duniani kuna watu wanajitafutia matatizo wenyewe halafu baadae wanatafuta sababu ya kumlaumu mungu.kwanza umeoa pili alikukimbia kama kwenzi lingekuwa linasafiri kwa bluetooth saa hizi lingeshatua utosini mwako,vitu vingine ni kutumia akili tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom