Niliponea Chupu Chupu ku-ukwaa

Niliponea Chupu Chupu ku-ukwaa

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Mwezi uliopita nilipata ugeni hapa kwangu, alikuja dada mmoja kwa sasa anamalizia masomo yake ya Nursing katika chuo kimoja kilichopo Mkoani Shinyanga.

Dada huyu ni mzuri balaa na ukizingatia ana asili ya watu wa Singida, nilifahamiana naye kama miezi mitatu iliyopita nikiwa Shinyanga kikazi, nilimpenda na nilichukua mawasiliano yake, tuliendelea kuwasiliana hadi mwishoni mwa mwezi wa saba alipokuja kwangu kunisalimia.

Kama kawaida nilimpokea, tuliongea mengi sana na lengo langu kwake lilikuwa kumuoa muda si mrefu, binti huyu alinieleza kuwa ameathirika na virusi vya ukimwi na kama siamini twende muda huo tukapime, nikamwanbia twende, baada ya wote kupima ni kweli damu yake ili-react kuashiria kuwa alikuwa na vvu, alinionyesha hadi vidonge vyake vile ARV anavyotumia.

Moyo wangu ulienda mbio sana kwa sababu sikuamini macho yangu kama kweli duniani bado kuna watu wachache kama huyu atakayekueleza ukweli,
tuliporudi nyumbani alinieleza kuwa yeye yupo tayari kuolewa na mimi ila lazima nimkubali na ndugu zangu vile vile wamkubali kwa hali aliyonayo.

Alinieleza kuwa yeye ni bikira na alipokuwa na umri wa miaka 7 mama yake mzazi alimpeleka kwa Bibi yake huko Singida, Bibi yake alimkeketa, inahisiwa kuwa kitendo hicho ndicho kilimsababishia maambukizi.

Alianza kuugua tezi akapelekwa hospitali. akapewa dawa lakini haikumsaidia ndipo ilipoamriwa apimwe kipimo kikubwa, akagundulika kuwa tayari ameathirika.

Kiukweli nilimchezea sana kitandani tena sana ila niliogopa sana ku-do naye japo nilimshukuru sana kwa kuniambia ukweli.
 
Polee na Hongera at the same time..sasa umeamuaje? Unaoa au unamuacha maana kama stori imeishia kati hivii...
 
Kwanj moyo unasemaje juu ya huyo binti?
 
Kama kweli unampenda.. unampenda kiukweli.. endelea nae.
 
Hapana, siwezi muoa unless at my own risk

Huoni kama utakuwa umemuweka kwenye reli then unamtupia huko.....anyways,ni kweli at your own risk. Ni bora ingekuwa na wewe umeathirika.
 
Ni kweli nampenda saaana, ila moyo unasita sita coz nahofia naweza kuupata na mm.

Kuoa watu kama hawa ni at your own risk, kubali kuwa lolote litakalotokea utakubaliana nalo.
 
Una mambo ya ajabu sana wewe. Sema tu kuwa ulimchapa but kistaarabu.
 
Huoni kama utakuwa umemuweka kwenye reli then unamtupia huko.....anyways,ni kweli at your own risk. Ni bora ingekuwa na wewe umeathirika.


Ni kweli kabisa, hata ku-do naye naogopa sana japokuwa kondom zipo.
 
Great risk ----> Great achievement. Am sure unaijua hiyo theory

Mmmmh. una maana panapokuwa na great risk ndipo mtu unapata mafanikio? hivi kupata VVV ni mafanikio!!
Hii theory hapa hai-apply.
 
Kama kweli unampenda.. unampenda kiukweli.. endelea nae.

Nampenda kweli ila mmh. yeye anasema tukitaka kuzaa tutakuwa tunaandaana vya kutosha ili nisipate michubuko! dah!! lkn bado hajanishawishi kbs.
 
Una mambo ya ajabu sana wewe. Sema tu kuwa ulimchapa but kistaarabu.

Mkuu hapana, sikumchapa kabisa, kwanza utakuwa na raha gani wakati wa tendo? coz muda wote utakuwa unawaza UKIMWI tu! na unavyojua sisi wanaume baada ya ku*do huwa tunajuta tena!!!
 
Mwezi uliopita nilipata ugeni hapa kwangu, alikuja dada mmoja kwa sasa anamalizia masomo yake ya Nursing ktk chuo kimoja kilichopo Mkoani Shinyanga.

Dada huyu ni mzuri balaa na ukizingatia ana asili ya watu wa singida, nilifahamiana naye kama miezi mitatu iliyopita nikiwa SHY kikazi, nilimpenda na nilichukua mawasiliano yake, tuliendelea kuwasiliana hadi mwishoni mwa mwezi wa saba alipokuja kwangu kunisalimia.

Kama kawaida nilimpokea, tuliongea mengi sana na lengo langu kwake lilikuwa kumuoa muda si mrefu, binti huyu alinieleza kuwa ameathirika na virusi vya ukimwi na kama siamini twende muda huo tukapime, nikamwanbia twende, baada ya wote kupima ni kweli damu yake ili-react kuashiria kuwa alikuwa na vvu, alinionyesha hadi vidonge vyake vile ARV anavyotumia.

Moyo wangu ulienda mbio sana kwa sababu sikuamini macho yangu kama kweli duniani bado kuna watu wachache kama huyu atakayekueleza ukweli,

tuliporudi nyumbani alinieleza kuwa yy yupo tayari kuolewa na mm ila lazima nimkubali na ndugu zangu vile vile wamkubali kwa hali aliyonayo.

Alinieleza kuwa yeye ni bikira na alipokuwa na umri wa miaka 7 mama yake mzazi alimpeleka kwa bibi yake huko singida, bibi yake alimkeketa, inahisiwa kuwa kitendo hicho ndicho kilimsababishia maambukizi.

Alianza kuugua tezi akapelekwa hosp. akapewa dawa lkn haikumsaidia ndipo ilipoamriwa apimwe kipimo kikubwa, akagundulika kuwa tyr ameathirika.

Kwel huyo bidada ni mfano wa kuigwa
 
Back
Top Bottom