Nilipona kupata UKIMWI nikapata TB

Kandambili1

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
425
1,122
Habarini wakuu.

Nimekuja kutoa mrejesho wa thread yangu iliyopita.
Unaweza soma apa

Kwanza nitoe shukrani kwa kutiwa moyo kwani kipindi nilichopitia kilikuwa kigumu sana kwangu, pia nakiri hapa nitakwepesha na sitataja tarehe na mwez sahihi kuficha kujulikana.

Kipindi nimekuja kuomba msaada kuhusu yule binti, nilikuwa sina uhakika asilimia 100, kwani yeye hakutamka kwa kunywa chake ila alikwepa kupima. Miezi miwili iliyofuata nikaanza kutoka jasho usiku kichwani na mwili wote, yani nashtuka nakuta jasho jingi sana kichwani na mwilini. Sikutilia manani maana mchana niliendelea kuwa sawa kabisa.

Mwezi uliyofatia nilikutana tena kimwili na yule binti nimuite Catherine. Baada ya kukutana naye week 2 mbele nilianza umwa tena mafua na kichwa. Nikameza tu Panadol na Prednisolone vikatulia, ila homa za usiku zikarejea kwa kasi sana.

Japo nilikuwa naumwa ila niliendelea kwenda vibaruani kama kawaida. Kuna siku niliumwa sana usiku na asubuhi nilishindwa amka, nikapiga simu kibaruani, dereva wa ofisi akaja, akanipeleka hospitali yeye akaondoka zake.

Nikaingia kumuona daktari nikiwa hali mbaya sana, nikamuelekeza ninavyojisikia, akashtuka kidogo nilivyotaja ninavyojisikia hasa homa za usiku. Akaniuliza direct una mpenzi na mmewahi kupima pamoja? Hapo ndiyo nilipochanganyikiwa na kuhisi balaa lililopo mbele yangu, utulivu wote ulipotea.

Nikamjibu nina mpenzi na natarajia mwakani nianze kufanya taratibu za kujitambulisha rasmi nyumbani kwao. Pia nikamjibu sijawahi kupima naye na kiufupi nilimuamini sana Catherine.

Doctor akaniambia inabidi nipimwe ukimwi na magonjwa ya kuambukiza yote na TB pia. Nikapima nikijua tayari nimeathirika, lakini majibu yakatoka sina ukimwi, sina magonjwa yoyote ya kuambukiza ila nina TB.

Nikaanza kutumia dawa na hadithi za ukimwi nikazisahau, sasa baada ya mwezi binti alifiwa tukasafiri pamoja hadi Songea, usiku tukawa pamoja nikafanya tena ngono usiku ule bila kinga kwa kumuamini binti.

baadae tukarudi mjini na mambo mengine yakaendelea, ajabu mwezi uliofuata nikaumwa tena sana na siku niliyoamka vibaya nikagutuka labda binti ndie chanzo. Nikamuomba tukapime alikubali lakini baada ya dakika 5 mbele akauliza, "Hivi kwa mfano mpenzi wako ana HIV aliachiwa na mama yake lakini anatumia dawa, je, utamkubali?"

Nikashtuka sana na nikajua tayari nimeukwaa kwani nikavuta picha ya matukio fulani ya binti kutokuwa huru kujibu maswali fulani fulani nikaogopa sana. Mfano huyu binti ni mzuri sana ila kasoro yake 1 alama za vidonda miguuni japo vipo mbali sana, siku nimemuuliza alipataje akawa hayupo huru kujibu akahamisha mada.

Alivyoniuliza hivyo nilichanganyikiwa sana wakuu, nikajuta sana. Hapo nilikuwa naumwa na kichwa kinakizunguzungu kikali sana, lakini nikajikaza hadi hospitali kupima nikijiambia nikikutwa na HIV basi nitajitoa duniani kwani nisingeweza kuvumilia maumivu na shida zote za HIV.

Nilienda hospital siku hiyo ilikuwa ya 44 toka nilipokutana naye kimwili. Nikapima nikiwa na kizunguzungu na maumv ya mwili, majibu yakatoka negative. Nikaja hapa JF kuomba ushauri, nikatiwa moyo na wengine wakanitisha zaidi, ila niliendelea kupima na hali yangu ya kizunguzungu na maumivu ilizidi nikazidi changanyikiwa.

Nilipima tena siku ya 50, 60, 70 zote nikawa negative kabisa lakini bado hofu ilinishika na nikazidi teseka na kukonda ghafla. Nilisubiri hadi zikafika siku 91 nikaenda hospital nikapima kipimo kikubwa nikawa safi na nikarudi kupima kipimo kidogo cha bioline siku ya 95 nikawa safi.

Week tatu mbele binti nilimblock lakini alinitafuta kwa namba nyingine nikamwambia msimamo wangu ni aweke wazi hali yake au anipoteze daima, binti akaniambia ukweli alizaliwa nao lakini anatumia dawa na ni ngumu sana kuupata akaomba msamaha.

Nilimsamehe binti kwani niliona najiweka tu katika mateso, lakini sikurudiana naye na sitarudiana naye japo nimemuweka wazi kuwa awe huru na anapokwama ananiambia namsaidia. Baada ya siku 97 kupita hali yangu ikawa sawa na maumivu yakaisha na nikarudi kuwa sawa kabisa,

Ushauri wangu: Vijana tuwe makini sana, binti alizaliwa nao, wengi huwa wanakuwa vizuri na wanakuwa wazuri sana na shape nzuri sana huwezi mdhania, na hata akikupenda sana ni ngumu sana kukwambia kwa hofu kuwa utamtangaza au utamuacha.

Nimejifunza elimu ya jinsia nikiwa na miaka 34, sasa nimekuwa na nimejua thamani ya maisha na upendo wa Mungu. Mungu ni msamehevu sana, amenisamehe na kuniokoa mara 2 zote. Asanteni.
 

Thread yangu iliyopita na baadhi ya picha za mawasiliano na binti, vipimo vya ukimwi na dawa za TB
 

Attachments

  • IMG_20221008_093239.jpg
    IMG_20221008_093239.jpg
    43.1 KB · Views: 73
  • IMG_20221008_093223.jpg
    IMG_20221008_093223.jpg
    36.9 KB · Views: 84
  • IMG_20221008_092915.jpg
    IMG_20221008_092915.jpg
    14 KB · Views: 69
  • IMG_20220721_111049.jpg
    IMG_20220721_111049.jpg
    44.5 KB · Views: 71
  • IMG_20220923_153948.jpg
    IMG_20220923_153948.jpg
    73.4 KB · Views: 65
kama unamtoto,kama unandugu kama unamdogo wako, usiache kuongea nae.

Kipindi naumwa mabinti wadogo tu niliona wanatumia dawa na mtaani mabinti wadogo tu hawakuacha kusogea kwangu, bila kujua napitia nini.

Asanteni sana Sky Eclat rikiboy Kunguru wa Manzese na wengine wengi sana mbarikiwe sana Kwa ushauri na kunitia moyo

Pia nimejifunza tusitenge na kunyanyapaa maana wengi wamepata kwa bahati mbaya, masikini mimi mahusiano nimejua ukubwani na sio muhuni lakini nimenusurika padogo sana.
 
Habarini wakuu.

Nimekuja kutoa mrejesho wa thread yangu iliyopita
Unaweza soma apa

Kwanza nitoe shukrani kwa kutiwa moyo kwani kipindi nilichopitia kilikuwa kigumu sana kwangu, pia nakiri hapa nitakwepesha na sitataja tarehe na mwez sahihi kuficha kujulikana.

Kipindi nimekuja kuomba msaada kuhusu yule binti, nilikuwa sina uhakika asilimia 100 kwani, yeye hakutamia Kwa kunywa chake ila alikwepa kupima,

miezi miwili inayofuata nikaanza kutoka jasho usiku kichwani na mwili wote, yani nashtuka nakuta jasho jingi sana kichwani na mwilini, sikutilia manani maana mchana niliendelea kuwa sawa kabisa.

mwezi unafatia nilikutana tena kimwili na yule binti nimuite Catherine,

Baada ya kukutana nae week 2 mbele nilianza umwa tena mafua, na kichwa. Nikameza tu panadol na prednisolone vikatulia, Ila homa za usiku zikarejea kwa kasi sana,

japo nilikuwa naumwa Ila niliendelea kwenda vibaruani kama kawaida, kuna siku niliumwa sana usiku na asubuhi nilishindwa amka, nikapita simu kibaruani, dereva wa office akaja, akanipeleka hospital yeye akaondoka zake

nikaingia kumuona doctor nikiwa hali mbaya sana, nikamuelekeza ninavyojisikia, akashtuka kidogo nilivyotaja ninavyojisikia hasa homa za usiku.

akaniuliza direct unampenzi na mmewahi Pima pamoja, hapo ndio nipichanganyikiwa na kuhisi balaa lililopo mbele yangu,utulivu wote ulipotea.

Nikamjibu ninae mpenzi na natarajia mwakani nianze fanya taratibu za kujitambulisha rasmi nyumbani kwao. Pia nikamjibu sijawahi pima nae na kiufupi nilimuamini sana Catherine.

Doctor akaniambia inabidi nipimwe ukimwi na magonjwa ya kuambukiza yote na TB pia

nikapima nikijua tayari nimeathirika, lakini majibu yakatoka sina ukimwi, sina magonjwa yoyote ya kuambukiza ila nina TB.

Nikaanza kutumia dawa na hadithi za ukimwi nikazisahau, sasa baada ya mwezi binti alifiwa tukasafiri pamoja hadi Songea, usiku tukawa pamoja nkafanya tena ngono usiku ule bila kinga kwa kumuamini binti.

baadae tukarudi mjini na mambo mengine yakaendelea, ajabu mwez uliofuata nikaumwa tena sana na siku niliyoamka vibaya, nikagutuka labda binti ndie chanzo, nimakuomba tukapime alikubali lakini baada ya dakika 5 mbele akauliza

"hivi kwamfano mpenzi wako anaHIV aliachiwa na mama lakini anatumia dawa, je utamkubali?".

Nikashtuka sana na nikajua tayari nimeukwaa kwani nikavuta picha ya matukio fulani ya binti kutokuwa huru kujibu maswali fulani fulani nikaogopa sana,

Mfano huyu binti ni nzuri sana ila kasoro yake 1 alama za vidonda miguuni japo vipo mbali sana, siku nimemuupiza alipataje akawa hayupo comfortable kujibu akahamisha mada.

alivyoniuliza hivyo nilichanganyikiwa sana wakuu nikajuta sana, hapo nilikuwa naumwa na kchwa kinakizunguzungu kikali sana, lakini nikajikaza hadi hospital kupima nikijiambia nikikutwa na HIV basi nitajitoa dunian kwani nisingeweza kuvumilia maumivu na shida zote za HIV.

Nilienda hospital siku hiyo ilikuwa ya 44 toka nilipokutana nae kimwili.
Nikapima nikiwa na kizunguzungu na maumv ya mwili, majibu yakatoka negative.

nikaja hapa JF kuomba ushauri, nikatiwa moyo na wengine wakqnitisha zaidi, ila niliendelea kupima na hali yangu ya kizunguzungu na maumivu ilizidi nikazidi changanyikiwa.

Nilipima tena siku ya 50, 60, 70 zote nikawa negative kabisa lakini bado hofu ilinishika na nikazidi teseka na kukonda ghafla.

Nilisubiri hadi zikafika siku 91 nikaenda hospital nikapima kipimo kikubwa nikawa safi na nikarudi pima kipimo kidogo cha bioline siku ya 95 nikawa safi.

Week tatu mbele binti nilimblock lakini alinitafuta kwa namba nyingine nikamwambia msimamo wangu ni aweke wazi hali yake au anipoteze daima, binti akaniambia ukweli alizaliwa nao lakini anatumia dawa na ni ngumu sana kuupata akaomba msamaha.

Nilimsamehe binti kwani niliona najiweka tu katika mateso, lakini sikurudiana nae na sitarudiana nae japo nimemuweka wazi kuwa awe huru na anapokwama ananiambia namsaidia.

Baada ya siku 97 kupita hali yangu ikawa sawa na maumivu yakaisha na nikarudi kuwa sawa kabisa,

Ushauri wangu: vijana tuwe makini sana binti alizaliwa nao wengi huwa wanakua vizuri na wanakuwa wazuri sana na shape nzuri sana huwezi mdhania, na hata akikupenda sana ni ngumu sana kukwambia kwa hofu kuwa utamtangaza au utamuacha.

Nimejifunza elimu ya jinsia nikiwa na miaka 34 sasa nimekua na nimejua thamani ya maisha na upendo wa Mungu...Mungu ni msamehevu sana amenisamehe na kuniokoa mara 2 zote. Asanteni.
Sasa yeye anao na maisha yanaenda ww kumgusa tu hofu kiasi hicho ? Acha kumnyanyapaa mwenzio
 
Kuuza mechi kumepitwa na wakati kijana.

Magonjwa hatari yanayoambukizwa kwa ngono yapo mengi sana.. Kuna HIV , homa ya ini, kansa ya kizazi etc..

Kuna wajinga wana tabia ya kununua vipimo vya hiv na kukaa navyo gheto. Demu akija gheto anampima HIV, akiona negative anakula mzigo kavu kavu bila kujua afya ya huyo demu kwenye magonjwa mengine... mwishoe anaambukizwa magonjwa mengine anakufa fasta
 
Back
Top Bottom