kelphin
JF-Expert Member
- Dec 24, 2019
- 10,387
- 17,095
Mshukuru Mungu kwa kumkosa
SIO kila unachokita ukakikosa unatakiwa kuumia, vingine ukivipata vitakuumiza
Ahsante .
Mshukuru Mungu kwa kumkosa
SIO kila unachokita ukakikosa unatakiwa kuumia, vingine ukivipata vitakuumiza
sana pia imani inaponza wengi...ni heri kuchukua tahadhari muda wote.Hii dunia yataka uwende nayo kwa akili San...
kabisa mkuu, maana wengine kuumwa kichwa tu ni shida je uambiwe umeze dawa maisha yote, Ile hali unafanya unakosa umaana wa maisha yani unalipua lipua kilakitu hujali chochoteKama hujawahi kupitia hiyo hali mtu anaweza asiamini. Binafsi niliwahi kuwa na mahusiano na mtu wa aina hiyo alikuwa tayari na maambukizi. Na niliingia kwenye mahusiano kwa kuhisi mimi pia si mzima maana nilipita sehemu zisizofaa. Lakini tulipoachana nilipata ujasiri wa kwenda kupima, kuanzia hapo maisha yangu yalibadilika sana.
Uhai na afya ni zawadi kubwa sana,toka hapo pamoja na muda mwingine kucheza rafu nyingi saana ila kupima na kujitambua ni muhimu sana.
akiwa hatumii dawa ni hatari ila kujaribu sio Sawa kabisa. Hongera kwa kuwa sawa, usawa ni maliKipindi fulani nilikuwa na mahusiano na mwanamke na nililala nae mara nyingi. Mara mwisho wa siku nilikuwa kituo cha ctc Kama prescriber mara paap mwanamke yule huyu hapa na faili lake la ctc. Kucheki viral load 'not detected' nikaenda kupima negative. Nikadharau kabisa kitu kinaitwa vvu.
Ah wee acha tuu kwanza kumwaga nje ni dhambi...wacha tuu tugegedane hayo mambo ya kujiapisha mie wala sijisumbuhi. Kugegedana raha bwana. Vipi wikend wajirusha wapiNi Mungu tu
Mtu anapima Leo anakuwa negative anajiapisha weee kwamba harudii tena lakini baada ya mwezi anauza mechi tena.
Sex iache tu iitwe sex
mzabzab
Asante kwa ushauri Mungu ni mwema sikuzote mkuu, anatusamehe hata pale tusipostahili msamaha. SitasahauSafi pale ulipoanguka pawe funzo maishani UKIMWI upo ningekuwa sio mvivu kuandika ningeuliza uma wa wanajf ila ndiyo hivyo tena kuandika ni mvivu na pia ni mtu wa hisia sana kiasi nikianza kuandika najihisi maumivu naquit
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa yani, kwa urembo wa yule dada sijui tu huko shule kama wamepona dah.Mshukuru Mungu kwa kumkosa
SIO kila unachokita ukakikosa unatakiwa kuumia, vingine ukivipata vitakuumiza
Sure tangu hapo muoga sana.Pole sana kile kihoro nilichopitia madhani ulipitia pia, tutulie sana mkuu, ukiumwa kidogo tu unajua tayari ukiamka usiku ukiwaza tu basi usingizi hauji hadi asubuhi.
Tuendelee kuombeana 🙏kabisa mkuu, maana wengine kuumwa kichwa tu ni shida je uambiwe umeze dawa maisha yote, Ile hali unafanya unakosa umaana wa maisha yani unalipua lipua kilakitu hujali chochote
Kama kweli unampenda nichek 0712505049 namtibu kabisa anapona bei laki tanoHabarini wakuu.
Nimekuja kutoa mrejesho wa thread yangu iliyopita.
Unaweza soma apa
Kwanza nitoe shukrani kwa kutiwa moyo kwani kipindi nilichopitia kilikuwa kigumu sana kwangu, pia nakiri hapa nitakwepesha na sitataja tarehe na mwez sahihi kuficha kujulikana.
Kipindi nimekuja kuomba msaada kuhusu yule binti, nilikuwa sina uhakika asilimia 100, kwani yeye hakutamka kwa kunywa chake ila alikwepa kupima. Miezi miwili iliyofuata nikaanza kutoka jasho usiku kichwani na mwili wote, yani nashtuka nakuta jasho jingi sana kichwani na mwilini. Sikutilia manani maana mchana niliendelea kuwa sawa kabisa.
Mwezi uliyofatia nilikutana tena kimwili na yule binti nimuite Catherine. Baada ya kukutana naye week 2 mbele nilianza umwa tena mafua na kichwa. Nikameza tu Panadol na Prednisolone vikatulia, ila homa za usiku zikarejea kwa kasi sana.
Japo nilikuwa naumwa ila niliendelea kwenda vibaruani kama kawaida. Kuna siku niliumwa sana usiku na asubuhi nilishindwa amka, nikapiga simu kibaruani, dereva wa ofisi akaja, akanipeleka hospitali yeye akaondoka zake.
Nikaingia kumuona daktari nikiwa hali mbaya sana, nikamuelekeza ninavyojisikia, akashtuka kidogo nilivyotaja ninavyojisikia hasa homa za usiku. Akaniuliza direct una mpenzi na mmewahi kupima pamoja? Hapo ndiyo nilipochanganyikiwa na kuhisi balaa lililopo mbele yangu, utulivu wote ulipotea.
Nikamjibu nina mpenzi na natarajia mwakani nianze kufanya taratibu za kujitambulisha rasmi nyumbani kwao. Pia nikamjibu sijawahi kupima naye na kiufupi nilimuamini sana Catherine.
Doctor akaniambia inabidi nipimwe ukimwi na magonjwa ya kuambukiza yote na TB pia. Nikapima nikijua tayari nimeathirika, lakini majibu yakatoka sina ukimwi, sina magonjwa yoyote ya kuambukiza ila nina TB.
Nikaanza kutumia dawa na hadithi za ukimwi nikazisahau, sasa baada ya mwezi binti alifiwa tukasafiri pamoja hadi Songea, usiku tukawa pamoja nikafanya tena ngono usiku ule bila kinga kwa kumuamini binti.
baadae tukarudi mjini na mambo mengine yakaendelea, ajabu mwezi uliofuata nikaumwa tena sana na siku niliyoamka vibaya nikagutuka labda binti ndie chanzo. Nikamuomba tukapime alikubali lakini baada ya dakika 5 mbele akauliza, "Hivi kwa mfano mpenzi wako ana HIV aliachiwa na mama yake lakini anatumia dawa, je, utamkubali?"
Nikashtuka sana na nikajua tayari nimeukwaa kwani nikavuta picha ya matukio fulani ya binti kutokuwa huru kujibu maswali fulani fulani nikaogopa sana. Mfano huyu binti ni mzuri sana ila kasoro yake 1 alama za vidonda miguuni japo vipo mbali sana, siku nimemuuliza alipataje akawa hayupo huru kujibu akahamisha mada.
Alivyoniuliza hivyo nilichanganyikiwa sana wakuu, nikajuta sana. Hapo nilikuwa naumwa na kichwa kinakizunguzungu kikali sana, lakini nikajikaza hadi hospitali kupima nikijiambia nikikutwa na HIV basi nitajitoa duniani kwani nisingeweza kuvumilia maumivu na shida zote za HIV.
Nilienda hospital siku hiyo ilikuwa ya 44 toka nilipokutana naye kimwili. Nikapima nikiwa na kizunguzungu na maumv ya mwili, majibu yakatoka negative. Nikaja hapa JF kuomba ushauri, nikatiwa moyo na wengine wakanitisha zaidi, ila niliendelea kupima na hali yangu ya kizunguzungu na maumivu ilizidi nikazidi changanyikiwa.
Nilipima tena siku ya 50, 60, 70 zote nikawa negative kabisa lakini bado hofu ilinishika na nikazidi teseka na kukonda ghafla. Nilisubiri hadi zikafika siku 91 nikaenda hospital nikapima kipimo kikubwa nikawa safi na nikarudi kupima kipimo kidogo cha bioline siku ya 95 nikawa safi.
Week tatu mbele binti nilimblock lakini alinitafuta kwa namba nyingine nikamwambia msimamo wangu ni aweke wazi hali yake au anipoteze daima, binti akaniambia ukweli alizaliwa nao lakini anatumia dawa na ni ngumu sana kuupata akaomba msamaha.
Nilimsamehe binti kwani niliona najiweka tu katika mateso, lakini sikurudiana naye na sitarudiana naye japo nimemuweka wazi kuwa awe huru na anapokwama ananiambia namsaidia. Baada ya siku 97 kupita hali yangu ikawa sawa na maumivu yakaisha na nikarudi kuwa sawa kabisa,
Ushauri wangu: Vijana tuwe makini sana, binti alizaliwa nao, wengi huwa wanakuwa vizuri na wanakuwa wazuri sana na shape nzuri sana huwezi mdhania, na hata akikupenda sana ni ngumu sana kukwambia kwa hofu kuwa utamtangaza au utamuacha.
Nimejifunza elimu ya jinsia nikiwa na miaka 34, sasa nimekuwa na nimejua thamani ya maisha na upendo wa Mungu. Mungu ni msamehevu sana, amenisamehe na kuniokoa mara 2 zote. Asanteni.
Sijui alikuwa anatafuta kugundua Nini!!?Kitendo Cha kufanya nae Tena tendo nimeishia palepale
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
