Nilipita uwanja wa ndege dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilipita uwanja wa ndege dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anfaal, Feb 18, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu, vituko haviishi. Kila sehem kuna mambo yake. Na watu wake huamini kuwa ni mambo ya kawaida na ndio nchi inatakiwa iende hivyo. Licha ya kwamba mengi katika yanayotokea tuhuma huelekezwa kwa serikali lakini sisi wananchi tunanafasi kubwa ya ukombozi wa nchi yetu.
  Pale uwanjani wakati wa kucheck in, wakaniambia mzigo wangu umezidi kama kilo 8. Nilishtuka kwa sababu huwa ninakawaida ya kucheck uzito wa mzigo kabla ya kusafari. Mara hii nikapatwa na hofu maana ni jambo ambalo huwa sipendi kamwe linitokee. Wale wahudumu wa pale, (hasa dada mmoja mjamzito), akawa wa kwanza kunirukia kila kilo dollar 30 kwahiyo inabidi ulipe dollar 240. Akaitwa mtu kwa haraka wewe toa beki lake weka pale. Aliyetoa begi akaniambia wewe ongea nao uwape chochote. Bahati mbaya hili la chochote huwa si katika mfumo wangu wa maisha niliojiwekea. Nikaanza kutoa baadhi ya vitu lengo hasa likiwa vibaki. Wale wahudumu pale wakaendelea kuninasihi niongee na wale watu pale watakubali. Wakati ninafanya hayo, akapita mzungu mwingine naye nikaangalia mzani wake ukawa umezidi wakamuacha aende. Sikujali lile kwa kuwa sikuwa muhusika wa ule mzigo, mara ghafla dada yule akarudi alivyoona kuwa kweli natoa mizigo akasema nakupa allowance ya 5kg, nikabaki ninaduwaa, kumbe anauwezo huu. Nikapack tena vitu vyangu, kupima mzigo haujazidi. Sikuelewa hasa tatizo lipo wapi. Lakini pia kauli za pale zilikuwa ni zenye kukera mno na zimejaa dharau ya hali ya juu. Kuna haja ya sisi Watanzania kujifunza kufanya kazi. Ubabaishaji hautatufaa kamwe. Naamini hii inaweza kuwasaidia watoa huduma wengine lakini pia nitawaandikia na wenye ndege maana wanahangaika na competition lakini kuna watu wanawaangusha.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pole sana !

  Mara nyingi kama unaondoka watakufanyia hayo. Kama haitoshi watakuomba chenji. Ninachokifanya huwa ninakuwa na USD 1 moja moja nyingi. Kupunguza shuruba zao huwa nawapa USD 3 - 5 maana huwa hawahebabu na mimi naishia zangu. Kuna siku ofisa wa uhamiaji aliniuliza kijana mbona unasafiri sana kazi yako ni nini? Nikamjibu pamoja na kusafiri afande ni sehemu ya kazi yangu. Akaniangalia na kuniambia sasa utaniachaje? hahahahahah nikamlambisha dolla 2 nikaendelea zangu.

  Wakati wa Kurudi baada ya kumalizana na Immigration, unasubiri mizigo ambayo mara nyingi hubebwa kwa mikono maana ile mashine ya kuzungusha mizigo huwa ni Mbovu, ukitoka kuna wale jamaa wa TRA wanafungua mizigo kukagua....Mara nyingi mimi huweka chupi juu wakifungua wanaboreka na kuniambia Mchungaji endelea nitoe basi nisikague mizigo yote najua umechoka....nao huwapa USD moja moja.

  Hii ni Made in Tanzania
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ndo maana kurudi Tanzania inabidi ufikiri mara mbili. its a f*en sh*hole. kila mtu mwenye mamlaka kidogo lazima aya-abuse. Hata msimamizi wa choo stand anaweza kukunyanyasa katika kutumia hicho choo. pumbafu kabisa.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Juzi nimeangalia documentary ya mtu alienda kutalii Tz. Kafika sokoni kununua nazi, wakakubaliana bei ni Tsh1,000. Mtalii katoa Tsh5,000. Mbona mama wa watu akagoma kutoa chenji! Nilikuwa naangalia na wazungu kadhaa. Ilikuwa aibu tosha. Inabidi niwaeleze ukienda sokoni inabidi uende na chenji ya kutosha. Hicho kitu huwezi fanya huku kabisa. It appears in Tanzania there is no sense of obligation at all.
   
 5. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hali hii ni hadi lini? We need to put a stop to this corrupt-like undertakings. Ni vyema kupendekeza namna ya kuzima mambo rather than kuyabariki iwe kama sheria.
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu I can bet hiyo ni SWISSAIR. Nilisafiri na hiyo ndege kama wiki kama tatu zilizopita na mimi nilikutana na hivyo vituko vya huyo dada mjamzito!!! Aliniambia mzigo wangu umezidi kilo 3 na hivyo inabidi nilipe dola 90, kwa maana ya dola 30 kwa kilo. Ukweli ni kwamba zilikuwa zimezidi kilo mbili tu wala sio tatu. Nilimweleza kwamba sina tatizo na kulipia hizo kilo tatu ila ningependa nilipe kwa kutumia credit card kwa kuwa sikuwa na cash. Aliniangalia mara mbili mbili na kuamua kuniachia.

  Ukweli huyu dada atawaharibia biashara SWISSAIR kama hatajirekebisha!!!!

  Tiba
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Nimejifunza kitu hapa kumbe credit card unamalizana nao lol! Thank u
   
 8. 2my

  2my JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe waoga kukagua vyupi eeeh
   
 9. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nimejifunza mbinu mbili vyupi na credit card watanikoma
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu si uwalipue tu kama wakikuletea upuuzi :A S 13: !!!
   
 11. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  sasa kama unajiamini na unajua uzito haukuzidi kwanini uliupunguza? by the way hiyo hiyo CCM unayoilamba miguu ndio imekuletea hizo kero. au akili zako hazijangamua?
   
 12. L

  Leornado JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Matukio ya hizi airport zetu yanasikitisha sana, hasa ukiwa mweusi unasafiri.

  Pale Arusha KIA wao wana tabia ya kukagua visa, wakiona ni lugha wasioielewa imekula kwako. Hata kama wakitafsiriwa wanakataa. Hasa jamaa mmoja mnene, anachukua hiyo pasipoti na kuingia nayo kule ndani kwenye mizigo. Utasubiri hadi miguu iingie ndani.

  Nashukuru muda wa kutua KIA ni asubuhi sana saa kumi na moja kiasi kwamba wakagua miigo wanakuwa hawajaamka.
   
 13. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  nilifikilia inanitokea pekee yangu kumbe na nyie pia!lol jamaa wa pale watia aibu walinidai dollar nikawambia kama imezidi nitawachia haya makatasi nione mtayapeleka wapi..wakatazama,kuonyesha vitambulisho wakaona aibu..kilichobaki wakadai mzee tuachie maji jua kali bongo,lol
   
 14. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hiyo tabia ya kuomba change nami nilikutana nayo... nilishangaa! Jamaa anakagua passport, then anakuambia vipi mama hakuna change iliyobaki...???!!!
  watu wanajishushia heshima zao wenywe kwa kuomba omba!... ndo umaskini hauishi..maana uko vichwani mwa watu!
   
 15. Rural Swagga

  Rural Swagga JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Poor customer service
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  uwalipue kwa nani, system imeoza toka chini mpaka juu.
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kama kichwa cha nyumba kimesuka na kuvaa heleni, watoto unategemea watakuaje? Changanya na zako
   
 18. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hizi mbinu 2 ya chupi na credit card nimezipenda nakwavile hawa wa tra ndio lazima nitahakikisha chupi zote cfui zote nakusanya cku ya kurudi nazipanga zote juu alafu nimezigeuza nje ndani chini naweka mizigo
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Hukumfahamu Babu lao, alitoa rai ya utani...aliona jina la AK-47. na ndio akasema hivyo.
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  nakumbuka wakati narejea nchini jamaa wakakomaa eti sijachoma chanjo wakati naondoka hivyo niwape 30000/= waniachie au nikachome chanjo kwa 100000/= mimi nikawaambia kama wakotayari kunipa kopi ya vitambulisho vyao na risiti nitawapa 30000/= la sivyo niko tayari kuchoma hiyochanjo kwa 10000/= kwa sharti la wao kunipeleka hospitali na hospitali nitalipa kwa bima ya afya jamaa kuona hivyo wakaniachia kwa kuniambia next time niwe nachoma
   
Loading...