Nilimuacha kimasihara, sasa hivi najuta

Nilimuacha kimasihara, sasa hivi najuta

Ngoja nikupe kisa kimoja.
Kabla sijaanza A level mtaani kwetu alikuja msichana mrembo mithili ya Malaika yule msanii na kila mtu alikua anamtamani hadi kaka yangu.Bahati nzuri nikashinda zabuni ya kuumiliki moyo wake.Sikufanya nae chochote na kule mtaani kwetu aliondoka ikabaki legacy yake tu kua kuna mrembo alipitaga hapa.Mimi nilovoanza A level nikawa na mambo mengi na ukizingitia mawasiliano kati yetu hayakuepo.Ila alikua ananitafuta mimi nilikua sina habar nae,Mpaka nafika chuo akawa anaendelea kunitafuta.Anaweza akawa ananitext mwez mzima ila mm sijibu na yeye hakati tamaa.Alikua ana upendo wa dhati.Chuo nikakuta warembo wengi hivyo nikamuona hana thamami ukizingitia hajasoma hadi chuo.Sasa bwana mwaka jana akafanikiwa kufika Jiji nililosoma chuo kwa anti yake.Akanitafuta tukaonana,aisee ile siku nilipagaqa mtoto kawa mzuri mara 100 ya zamani yani sijaona mfano.Nilimpeleka kwa rafiki yangu nilimaliza nae Mlimani akaniita pembeni akasema usipooa hiki chuma Mungu atakulaani kwani hutopata tena kisu kama hiki.Toka pale nikajiona mpumbavu na nikawa naanza mtafuta mm mpaka leo hii na mwakani Mungu akipenda natangaza nia.Hajawahi niomba pesa kama wasichana wengine,anaakili ya maisha na anaupendo kwa ndugu zangu..Kwahiyo mkuu ukifanikiwa kupata msichana mwenye kariba hiyo usijaribu kumdharau na kumtoa thamani kwani wamebaki wachache sana hapa duniani unaweza juta maisha yako yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama nitakuja kumpata kama yeye
 
Sasa hivi ni miaka mitatu imepita tangu nimuache kiutani utani mwanamke alienipenda kwa dhati.
Naomi mwanamke ambae aliweka malengo ya milenia kwangu ni vile mimi nikajivimbisha kichwa na kujiona mimi ndio mimi ,star sana .

Nakumbuka kila asubuhi before hajaenda chuo , alikuwa anapitia ghetto ananipikia chai ,na kunipa show kisha anaenda shule..
Alihakikisha napendeza muda wote maana alinifuria nguo, ghetto liling'aa muda wote.kipindi hicho yuko kachuo fulani anasomea kozi ya nursing,alisema akimaliza chuo tutaoana,

Ikafika kipindi amemaliza chuo yupo anasikilizia apate kazi,akaja kwangu kukaa huku anafanya harakati za kutafuta kazi, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo nilivyozidi kumuona wa kawaida.

Ilipita miezi kama mitatu hivi naishi naye sasa nikawa nimemchoka.nikaenda kwa jamaa yangu nikamuelezea, kwamba yule demu nimemchoka nitumie mbinu gani kumtoa.
Jamaa yangu akaniambia mbona mwanamke mzuri sana,anaheshima,kwanini unataka ufanye hivyo,
Nikamwambia nimemchoka,pili sihitaji,kuoa kwa wakati huu.

Jamaa yangu alisikitika sana,akasema wenzako wanaombea wapate mwanamke kama wako, wamebakia wachache sana.

Siku hiyo naomi alipigiwa simu na kaka yake, anahitajika aende alishafayiwa mpango wa kazi.
Akaniaga vizuri na kusema atanipa updates za kila kinachoendelea huko,
N
Asubuhi yake nikiwa nampeleka stand kwaajili ya safari,nilionekana nafurahi sana,hADI akaniuliza mbona nina furaha sana, inaonekana nafurahi kuondoka kwake, nikamwambia Mimi nafurahi kupata kwake kazi,

Basi kilichofuata ni kabadirisha namba,akawa akija namkimbia kimbia,kumficha na kumkwepa kidizaini.

Baada ya kukimbia kimbia sana aliandika barua,akamuchia yule jamaa yangu.

Kwenye barua akasema,,"najua unaninifichama kama umeamua kuniacha si uniambie tu ili nielewe nifanye mambo mengine kuliko kujipotezea muda"

Ilipita miaka miwili hatujawasiliana ila mimi nilisikiaga kuwa anafanya kazi huko irembura hospitali..wala sikuwahi kumtafuta.

Bwana mwaka huu nimeonana naye mtoto ameng'aa kapendeza kawaka sana.ameniambia kashaolewa tena kwa ndoa na ana mtoto wa miezi kama mitatu hivi.nilitetemeka na kuondoka haraka sana.

Wadau nilimuacha kimasihara sasa hivi najuta sana haipiti sekunde sijamfikiria yeye,naumia wanawake wengine wapo kimaslahi zaidi,ila naomi ame change sana kawa mzuri sana, tofauti na alivyokuwa zamani,,

Nifanye nini niache kumuwaza kila saa [emoji86][emoji86][emoji86][emoji86][emoji86][emoji354][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mzee baba, wewe unapitia wakati mgumu kama mimi pia. Niliowaacha kwa upuuzi wangu kipindi sina mpango wa kuoa ndiyo ninaowawaza sasa!

Ninapojaribu kuulizia habari zao, tayari wameshaolewa. Nabaki najutia tu, maana ninaokutana nao ni balaa tupu.
Komaa na hali yako..vizuri mnavidharau
Hii comment yako inauma sana, japokuwa ndiyo ukweli wenyewe uliojificha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom