Nilimshauri hivi rafiki yangu kuhusu mchumba, je nilikosea?

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Kama unatafuta mchumba vigezo na asilimia zake ziwe hivi. Uzuri uwe 60% Tabia 35% mambo mengine kama elimu, n.k 5%. Sababu kuu ni kuwa 60% za uzuri maana ndio chanzo kikuu cha kusisimua mapenzi hatimaye tendo la ndoa. Na kwa sheria ya ndoa TZ kama tendo la ndoa halifanyiki kwa usahihi, ndoa hiyo inaweza kuvunjwa. Pili uzuri ni permanent, huwezi kuubadilisha, zaidi unaweza kuuboresha kwa urembo, lakini uzuri kwa maana ya body morphology huwezi kuubadili tofauti na tabia au elimu ambayo unaweza kuibadili kwa mambo kama mazingira, elimu, exposure, na kuonya. Tabia nimeipa 35% nikiwa na maana awe na reasonable tabia ambayo hataonekana kituko katika jamii japo anaweza akawa na mapungufu kadhaa yanayovumilika na ambayo yanaweza kurekebishika. 5% ya mengineyo ni ziada tu wala hayatakiwi kiwe kikwazo kwa mtu ambaye amepata score ya 95%. Je ndugu zangu mnaonaje ushauri niliompa rafiki yangu? Kumbuka sijataja Jinsia hapa maana ushauri huu kwangu ni any gender. Karibu tujadili . . .
 
ulikosea sana sana, ungekuja kuuliza kabla ya ushauri. Dah ushampotosha mwenzio sasa
 
hujui nani kakwambia uzuri ndio ngao wewe inaonekana hujaoa
nakushauri uoe mzuri ili uje na majibu sahihi
 
Simple, ni uzuri wa umbo na sura. Hapa inategemeana na mtu na mtu ilimradi wewe mtafuta mchumba uridhike kuwa kwa sura hiyo na umbo hilo, huyu mchumba ni mzuri angalau kwa 60% anakuvutia.
uzuri gani unaoongelea hapa....................ko hao wazuri
ndio wana uwezo wa kusisimua PENZI wengine hawawezi!!!!!!!!
 
Yeees uzuri ni ngao tosha kabisa, mtu unayetegemea kulala naye kitanda kimoja for the rest of your life lazima awe anakuvutia vya kutosha Ndo maana nkatoa 60%. Usijifariji ukaja kupata shida na kukodoa macho mtaani.
hujui nani kakwambia uzuri ndio ngao wewe inaonekana hujaoa
nakushauri uoe mzuri ili uje na majibu sahihi
 
Kwani vigezo vya mke mwema ni vipi achilia mbali mambo yenu haya ya gelofrendi sijui boyfrendi?
 
Simple, ni uzuri wa umbo na sura. Hapa inategemeana na mtu na mtu ilimradi wewe mtafuta mchumba uridhike kuwa kwa sura hiyo na umbo hilo, huyu mchumba ni mzuri angalau kwa 60% anakuvutia.

Well initially... its the look that MAY attract you.......
but it's the personality that keeps the love thriving, evolving,

kwa mfano mimi kama H.O.E huwa siangalii uzuri wa mwanaume..nahisi na kama naangalia haizid 5%...
sura yake nitatembea nayo!!!!!!!!sura yake will it pay the BILLS NO!!!!...ukute mtu HB lakin hana
vision ya maisha wa kazi gani huyo........
 
Yeees uzuri ni ngao tosha kabisa, mtu unayetegemea kulala naye kitanda kimoja for the rest of your life lazima awe anakuvutia vya kutosha Ndo maana nkatoa 60%. Usijifariji ukaja kupata shida na kukodoa macho mtaani.

Unaposema uzuri unaulinganisha na nini..? Labda tuangalie cha kwanza kabisa ulivutiwa na nini kwake..? Au how do u define huo uzuri..? Ina maana when u fall in love unakuwa na choice kwamba hapa ni-fall na hapo nici-fall..?
 
Nilishajibu huko nyuma!! Uzuri ni "case dependent" kila mtu kuna jinsi anavyodefine uzuri wa mtu. Siwezi kuwajibia watu ila la msingi, kama tunakubaliana kuwa factor ya uzuri katika mahusiano ipo basi ipewe asilimia kubwa, for whatever definition. Kwa sababu uzuri ndio kitu pekee ambacho hakibadiliki na huna option ya kuubadili. Vitu vingine kuna room ya kuvifanyia kazi na kuvibadilisha that why kwa kuanzia nimevipa alama za wastani kwani unaweza kuvifanyia kazi na kupata alama za juu hata baada ya kuwa umeshaoa/olewa. Mfano kigezo cha tabia, unaweza kukitoa kutoka 35% mpaka 75%. Na sasa niwajibu wanaouliza kuhusu %. Hizo ni alama za ufaulu. Mfano kila mtu angempenda mtu mwenye tabia nzuri sana (100%), lakini hata kama tabia yake ni ya kawaida say 45-50% huyo bado amepass kwani mambo mengine yanarekebishika, through exposure, elimu n.k. Yule ambaye yuko below 35% ( tabia hafifu) anaweza kuwa na matatizo ambayo ni magumu kurekebisha, au yanaweza kuchukua muda mrefu sana kuyabadili hivyo kuwa haina maana tena kuendeleana naye.

Back
Top Bottom