Winner80
Member
- Feb 9, 2021
- 20
- 19
Baada ya msiba wa baba ndugu wote waliondoka na kuitelekeza kabisa familia yetu. Hakuna hata ndugu mmoja aliyeonyesha moyo wa kuendelea kujihusisha kwa namna yoyote na maisha yetu.
Mbaya zaidi ni kwamba, walimnyang’anya mama karibia mali zote alizoziacha baba, pamoja na chakula ambacho kingeweza kutusaidia kusogeza sogeza maisha angalau kwa siku chache.
Ukweli ni kwamba, siku zote Mungu huwa na namna ya kutusaidia tuwapo katika nyakati ngumu. Tukiwa katika mazingira hayo magumu, Babu yetu mzaa mama alihusika sana katika kutusaidia.
Pamoja na mambo mengine, alitusaidia chakula cha kutusaidia kusongesha maisha mbele. Hakika ulikuwa ni muujiza, kwa sababu kama isingelikuwa yeye kutusaidia, pengine tungekufa kwa njaa.
Hii ni kwa sababu, zaidi yake, hakuna ndugu yetu mwingine aliyethubutu hata hutaka kujua tunaendeleaje mara baada ya kifo cha baba.
Katika umri wangu mdogo, nilipitia mambo mengi ambayo kwa umri wangu ilikuwa ni vigumu sana kuyabeba.
Baada ya matukio haya yote kupita, moyo wangu ulijaa na uchungu mwingi sana. Jambo hili lilinifanya niwachukie sana ndugu zangu wote.
Mpenzi msomaji, wakati mwingine unakutana na watoto wa aina mbalimbali
Huko mitaani.
Kuna baadhi ya watu hudhani kwamba watoto hao ni wakorofi, watukutu na waliotoroka majumbani kwa kwa sababu ya kiburi chao.
Binafsi, mambo niliyopitia yananifanya niwe na jicho la tofauti sana ninapowatazama watu wa aina hiyo.
Ninaamini kwamba, kadiri unavyoendelea kusoma kitabu hiki utaanza kuwa na mtazamo wa tofauti kuhusu kundi hili la watu katika jamii. Ninamuomba Mungu kupitia ushuhuda wangu, ainue watu watakaokuwa na moyo wa huruma na kujitoa kusaidia jamii hii ya watu.
Wengi wao ni wahanga tu wa mambo mbalimbali waliyopitia katika familia zao na mazingira tofauti tofauti waliyokulia
Itaendelea..............
Pastor Winner
Ukonga 0659-409447
February 22,2021