Nilikutana na mzungu asiye na hela kwenye "Dating app"

YE67NBE

JF-Expert Member
Nov 30, 2015
15,174
36,226
KUMEKUCHA KUMEKUCHA MWENZETU ANASHARE KISA CHAKE

TUIITE MPENZI MZUNGU NO 1
STORY TIME

Hekaheka za maisha kutafuta riziki za ndoa kwenye dating app miaka miwili ilopita niliweza kudownload tinder app kwajili ya kutafuta mchumba mzungu na marafiki tofauti wa kuchat nao

Hapo ekaheka likaanza nikawa sijui vigezo vya kuchagua watu wa maana nikajua mzungu akiwa mzungu tu basi pesa ipo hahahaha kumbe loh wapo njaa kali basi shoga enu nikamatch na huyo mzungu tukachat tinder baadae tukaamia watsapp tukapanga meeting yey akasema yupo kigamboni lkn nikajiuliza huyu mzungu wa kigamboni kweli mmmh

Lkn nikajitutumua siku tulopanga kukutana nikajiandaakisha nikamtxt narequest bolt atalipa akauliza how much? nikamjubu its cost 23 akajibu no just use public transport don't use bolt mmmh nikajipa doubt huyu mzungu mbona bahiri sana

Kipindi hicho naishi tegeta nyuki nikapanda daladala hadi kivukoni nikavuka na panton nkachukua daladala tena hadi nilipoelekezwa kuwa yupo barakuda beach nikashuka tena shoga enu walinioitiliza nikarud kwa mguu kufika hapo nikauliza mlango wa kuingilia balakuda beach nikaoneshwa nikazama ndani nikaakaa meza moja lengo langu nimuone huyo mzungu kisha nifanye maamuzi haraka

Nikampigia hlw nishaingia hapa uko wap akajibu nipo huku beach just come here around ocean lets chill here and walk behind the beach its nice place huku chini nikamjibu we njoo huku juu then will decide

Eeeeh bandugu after a while mzungu c akaja nikaona mtu wa ajabu akitokea baharin anapanda huku sehem ya kukaa watu kama counter jamani mliona mkanda wa yesu yule alotolewa mapepo na Yesu yakaamliwa yaende kwa nguruwe khaaaa sina la kuwaeleza lkn nadhani watakua ni mapacha

Nilianza kusali nikaweka sim mezani najifanya nachat siongei ili asinijue toba toba naona ananifuata uwiii akafika yani kwapani ni mzitu wa amazon,serengeti national park cjui national pack zote yey anazo jaman ile kufika na kukaa ni kama ilipita gari ya toka ama ni kama nimepita buguruni sokoni halafu mbaya kali ilipita puani mwangu

Nikamcheck kabeba mfuko ndani una yebo na vitu vitu siweza jua ni vitu gani kwa haraka lkn alikua kifua waz na shat aliweka ndani ya mfuko alotia yebo

So baada ya hapo nilipata msongo wa mawazo kisayansi wanaita sonona ambayo sikuwahi pata ni heli hata ningedaiwa vikoba waje na matarumbeta waniaibishe wabebe vitu vya ndani hiyo aibu ningeibeba lkn ile aibu ya mzungu yule ilikua nzito kwangu

Enewei akaomba tusimame tushuke chini tukae around beach tyongee aliposimama jaman jaman kwanza kakonda mnoooo mnooo suruali alivoaa mregezo ndan hajavaa chup matako yapo njee na sehem ya juu ya utupu wake inaonekana na nywele na nguo alovaa surual ilikua nyepes sana maumbile yake ya uume umejichola

Yan nilitoa macho kias sikuweza fanya maamuz haraka ikabid nisimame na nimuombe atangulie mbele twende sehem alosema tukakae bas nikamfuata jaman kila mtu anatutazama sisi bila kupiga kope

Najiuliza maswali mengi huku namfuata ama huyu ni chizi bas tulika baharin kuna viti mm nilikua nimenunua soda tayar wakaja wahudumu kuuliza kama tutakula mimi nikakataa maana nisingeweza kula mbele ya yule kaka ni kinyaa

Tukaaanza story za hapa na pale why yupo bongo kiukweli nilimuuliza mwaswali mazito sikuweza jizuia nilimuuliza mbona hujipend uko mchafu hivo na kucha zimelika mnoo za miguu akadai anashinda baharini sana

Inakuja part 2
 
Dating app

MPENZI MZUNGU NO 2


Kula chuma hicho

Basi shoga enu nilichagua kutokula sababu ya kinyaa kwanza napia binasfi kipindi hicho sikuweza kuwa na pesa nilikua na nauli tu sasa kwa muonekano wa yule mzungu tabu nikaona nisije kula nikaambiwa nideki bahari aka nikagoma zangu

Tukiwa pale jua likatuandama na tulipofikaniliwahi kiti cha mtu mmoja sikutakanikae nae lkn jua likazid akaomba tubadil mkao si ndo tukakaa kwenye kiti cha mtu 2 mwanzo nilijaribu kukeep distance time by time si akanisogelea toba roho yangu mara akainua mkono akashika upande wa pili wa bega langu yani kwapa lote akanisusia mtoto wa kiafrica nisie na hatia kabisa na lengo langu halikua baya hadi nifanyiwe hayo yote

Aisee nlipiga jicho la bombastick eyes yani lile kwapa nikama kaongezea kawigi kidogo lkn kumbe ni vuz tu za kwake utasema kabond halafu zinawekundu afu zina tumaji khaaa mwee mm sitaki kukumbuka

Mara akanibusu busu begani nyie nyie niliwaza nifike nyumbani ndo nioge au nioge tu kwanza baharini nitoe na nuski alizonipa ndo nikaoge nyumban

Nimshtua hey sory i need aspace plz alinitazama kisha akasmile toba ile smile inakuambia usile tena mwaka ufe kwa njaa maana yale meno last time kuona mswaki sijui lini na ninjao kuliko ile njano yenyewe

Yalinikuta mimi jaman soda ilikua shubir haipiti kooni niliwaachia tu nzi wacheze nayona ubahili wangu mm nishajilipia ila sonona ishanikumba no way
Tukiwa katika story nikamuuliza sasa vip hiyo mijivuz kwapani and you walk around people uko naked huoni aibu (bhna kinge mwenyewe nafosi mopaka nibane meno hapo nilimuuliza mbona haoni aibu anatembea uchi uchi kwa watu) jamaa akajibu hizo vuzi zake ni natural zinaota wa wingi

Aaah sasa kama zaota nyingi huwezi kukata kupunguza uchafu akajibu hawezi nikamwambia kama huwezi pls do it for me vaaa shati kwa sasa afu simama upandishe hiyo suruali tuendelee kuongea

Kweli akasimama akapandisha suruali ukweli niliona mifupa ikiwa ndani ya ngozi nyeupe jamaa kakonda yule kama mbwa mifupa tu unahesabu pale

Akachukua shati katika mfuko toba alipovaa nikagundua ni kaoshi yani still kwapa zinabaki njee njee sasa ngachoka mimi nikamuuliza kwa ukali wewe ss ndo nini hiv akajibu sina ya mikono mirefu woiiii mimi hakuna siku ilikua ndefu kama ile yan ilikua na masaa 365 akili ya kuondoka sina yan acheni

Basi nikamuuliza umetokea nchi gani akajibu from france ooh so huku upo kufanya nini na unaishije kwa kazi gani? maana seems your not okay afu nimezoea wazungu wengi wanatokea masaki,mikocheni,mbweni e.t vipi wewe

Akajibu mimi niliondoka kwetu sababu walikua wanaforce tuchanje chanjo ya corona na mm nilikua sipo tayar mke wangu kachoma na mtoto mm nimkuja huku mpaka hilo sakata liishe ntarud huko

MiMi:Sawa kwahiyo huku unaishije bila kazi na unakaa wapi
Mzungu pori:mimi nakaa guest na kuhusu pesa nyumbani wanitumia

Kwahiyo unakaa guest ya sh ngap nikamuuliza akajibu ya elfu 20 ila ameomba wampunguzie toba roho yangu nikamuuliza wew yan hadi 20k unaomba punguzo wewe huna hela

Na kigamboni umechagua kwanini mbona wewe ni mgeni kuna safe place na nzuri ulitakiwa ukae why huku vibaka kibao unashinda beach jua lako mvua yako hivi wew nashidani kama unanificha just tell me ukweli labda nawezakukusaidia

Kikajibu ok honestly mm nilianza kukaa zanzibar huko nilipata kuibiwa vitu zangu vyote nikamjibu ulikaa local place kama ulifanya hapa kigamboni akacheka tu lkn maswali nilokua nampiga alikosa nguvu akaanza kutetemeka

Akaendelea kunieleza kwamba baada ya kuibiwa aliingia mtandaoni na akaona kigamboni ndo sehem nzuri na salama yani hapa nilicheka kigamboni nan kakwambia ndo salama akajibu amesoma mtandaoni maoni ya watu nikaongea kwa kiswahili sio kosa lako huna tu hela

kikaniuliza sorry hapo sijaelewa umeongea kiswahili
Katika story kuchangamka akaniuliza napenda kula nin nikataja vyakula vya miziz kama viazi,mihogona ndizi

Nikaona yupo kafurahi mnoo anaiuliza kweli wapenda mihogo dear ninayo hapa ngoja nikupe ule shoga enu nilijionea mengi mimi khaaa baba yule akatoa mihogo na ndizi za kuchemsha zimefungwa na gazeti tena lilolowa mle ktk mfuko ambao mwanzo aliweka yebo na shati na takataka zingine macho yalinitoka yakatoka tena weeee why why yan nilikua kama kanumba mbona chakula humo jaman wew uko sawa kweli

Mzungu kwann nikajibu rudisha kwanza me napenda ila nimeshiba ndomana sijaagiza chakula sasa mbona umeweka humo akajibu niliweka nikija beach nile dah maskin

nilijipongeza kwa kutoagiza chakula basi story zikaendelea nikamwambia aseme shida yake ni nn akasema yey shida yake ni ndoa na mtoto maana visa yake imekaribia kuisha kwahiyo kama nipo tayari kesho tufunge ndoa mahakaman ili visa yake iongezwe muda

nikamwambia sasa kakahilo halina shida ila nina principle zangu ukiziweza namimi nitakutekelezea yote

Akauliza ni zipi basi nikamjibu moja mim nazaa kwa malengo kwahiyo jaza bank account yangu au npe mtaji tuzae ,pili mtafutie mtt wako nyumba nzuri nikizaa hata ukienda kwenu ukikaa kimya watu huku hztuteseki sasa naona muda unanitupa mkono nikuache utafakari kish utanijulisha kwenye simu kama unaweza kama huwezi plz usinitafute

Nikasimama nikamuuliza hakuna short way ya kutokea road akajibu ipo akasimama akatoa miwani mweusi akavaa kama yule jambazi chipaka wa kwenye saladini movie tukaongozana jaman watu walikua wanatuangalia mnoo nikona wazungu wazee mwanaume yupo na huyo dada mweusi yan huyo dada yupo kama mwehu anatukana hatar huyo mzng wake jaman waungu wakizeeka wanatsha mnoo

Nikaona na mmasai nae yupo na kibonge mzungu anahangaika nacho kila mtu anahangaika na riziki yzke

Tukwa tunatembea pembeni ya beach kufuata njia ya kwena road nikapande gar mzungu akasema nilikua naomba twend e nilipofikia ukapajue tu halafu kama ukipenda mimba ubebe leo kama upo danger mengine ntayafanya

Utapanga sehem nzuri na pesa ntakuwekea sasa angenijua nnavopenda pesa mimi ile kauli ilinikela kiasi nilitaka nimtzpikie usoni hasira ziishe maskini unaongea nin ww si utulie tu

Sikumjibu kitu alipoona nimekaa kimya kama sijasikia mzungu aliongeza speed ya kutembea ili aniache na tulawa tumefika chocho inamiti mingi huku nyuma anavopepea limgongo limeinama kama ngamia shenzi we li France

Itaendeleaaa......
 
Dating app

MPENZI MZUNGU NO 3

Kula chuma icho sehemu ya mwisho

Wacha tusonge na mzungu from france basi huyo mfranc aliongeza speed ya mwendo kama kafunga tairi kwa miguu nailikua kuna miti sasa nikapata uoga nikamwita hey why you walk so fast wait for me na unajua njia siijui bas akanisubir ilikua kapori karefu kidogo na miti

Mzungu anajua hadi chocho hii balaaaa hili hapo kabeba fuko lake na miwani mweusi kama kishoka wa j plus bongo movie nguo chafu chakavu

Yani nilipotokeza tu road naona magari hata sikumuangalia mara 2 nilisimama na vile yy alitembea kama kaka kuona hageuki nyuma me nikasimama wtu wasijue nipo nae anageuka anakuta nimesimama kule yy ashafika mbali nikavuka gar ikaja nikapanda huyo motoo

Yan nilikua najinusa kila dk maana wakati kanigemea nilikua najirudisha nyuma zile vuz zisiniguse na ile arufu yan niliposhuka nilitaka nichukue stiliwaya niogee nilihis kila mtu ananisikia nanuka nilijionea aibu kwa ujinga niloufanya na mkumbuke sikua na hela yan nauli yangu mm kama 4500 iliniuma mm nyiee nikama nilitumia laki 4

Nilifika hom nguo nikaloweka mim bafuni kuoga kisha nilikaa kutafakali kumbe si kila mzungu anapesa jaman khaaa kaka mchafu yule nikakumbuka na yule mzee wa kizungu muonekano wke afu ni watu hawaoni shida kukaa uchi wazungu wanatembea tu na chupi yan yule babu sijui nielezeje muelewe

Yule mzee wa kizungu ni kama kamwagiwa uji mzito ulopoa unapilomoka slowly yan mwili wake unatisha likitambi khaa yan mbaya mwili umedondoka umeshuka umelojoka lkn ana dem na anamvumilia na huyo dem ni ana smoke na matusi kibao ya kinge anwatukana wahudumu kaweka brichi sijui pink,kijan yan kidogo tu mother fucker yani kama kaweuka hiv nilirudisha matukio yote niloona mchana kigamboni

Nilisema hakika leo nimeona mengi kwa muda mfupi

Nilianza jiapiza sitki mzungu tena kama wazungu ndo hao sitaki mimi maisha yaliendelea baada ya siku mbili akaitafuta na kudai passport yake inaisha inabid aondoke vip mpango wetu

Nikajibu pesa ipo tuendelee na mpango eti kakajibu why you put money first dear bro you ask stupid question weka dau hapo twende bomani mimi sio mnyama wa majaribio

Akaaza jieleza nikampa brock mubashara nikakaa week naona no mpya hi nikajibu

Eti mim fulani kutoka tinder ulinipa no naishi posta nikasema tuma picha nikukumbuke kikatuma kinaonekana kituruki

Nikacheka nikasema mbona unaendana nawahindi wa kariakoo eti sorry

Kwahiyo unasemaje kikaomba tuonane shoga enu kilanga kishaisha nikajibu sikutani nastrangel akamua apige video call nikakata nikamtext why video call recharge me first

Kikasema why you put money first kikapiga kikaomba nipokee sekunde napokea eeeh jaman ni mfrance kakonda yani kwenye ile video call aliweka camela kwa chini uso nilikuanauona kama mbuni wa mikumi

Kikaanza jieleza nikisaidie passport inaisha nikamwambia rudi kwenu ww kajipange utakufa njaaa unang'ania huku ili iwaje ona unapukutika suruali zinadondoka bas kikaomba niki unbrock kimeazima sim kwa rafiki ake

Yan humo guest wanapokaa wapo wengi wachina,farnce,waturuki mixer kupo rafu na manet ya msaada Kama camp

Basi last time tupo beacha nilisahau kuwaambia mzungu aliomba tupige picha nikaataaa sasa muda ulipita kama week akanitxt kwa no mpya kapiga picha yupo kwao france mwenyewe kavaa nguo chakavu na yebo zake ananiambia mm niliondoka

Nikamuuliza jina lake akaniambia nikamcheck facebook jaman jman niliyoyakut huko duh kwanza anatoka familia maskin mnoo yan hata bongo sijui nitolee mfano wap yan nguo zao nyumba zao wanaishi kwenye madample kwa nilivoona zile picha afu nikakutapicha zawadada wengi sana wakibongo wengi amepiga nao pale pale barakuda beach shubamiti yule na hao wadada wamekenua meno kama ngiri natena wengine walienda nae hadi guest alipokua analala jamani sie wadada wa kibongo nimajasiri wallah Nyie wadada mlopiga picha na mfance yule mfuga vuzi pale barakuda 2021 aliwapost wote na mlienda guest na nyie kawapost mpo live afu mlikua mnamgusa kabisa bila shaka yupo alieliwa na kupigwa romance khaaaaa aibu kubwa jaman ndugu yenu kawapost huko kama kumbukumbu ya watu mlomonea huruma mmja baada ya mwingine na ukute hakuwapa kitu mm hata nauli sikomba nilipagawa niondoke kigamboni mpaka sasa naogopa kwenda ile beach nahisi watanikumbuka natania

Kwakweli picha yangu ndio ilikua iwe ya mwisho pale ila malaika wa zamu alikua upande wangu katika hilo shetani nilimshinda kwa nguvu zangu zote nikambrock kabisa
Nikagundua pia ndomana kila mtu alikua akitusindikiza kwa macho kumbe huwa wanamuona na manzi tofauti tofauti hapo beach sis wadada wa kibongo hatujui tunajichoresha tu

Mtandaoni mambo ni mengi jamani story time tucheke ntawapa vipengele vya kusisimua mcheke mkipenda naendelea vingine ilikula kwangu lkn dah this life no balance wallah nipo home likizo sina la kufanya wacha niwafurahishe my zangu

Kwenye dating site yan nayajua maronya yote hadi mabongo maswahili maongo na hivi ndo nacheza nayo tusipotezeane muda lengo ni kujifunza na kufulahi wala sipo kupoteza jamii warembo msinielewe vibaya humu wapo wanaotumia dating app kwa sababu zao binasfi lkn wapo watao anza kutumia chukueni tips hizo muaze nazo msije poteza muda kwa machoko

Kituo kinachofuata Mnigeria you dey like fine girls Ashawo nipeni ruksa niwape story ya mnigeria

Story time fanya kulike na kuccomment kwa sana nitupe kisanga cha mnigeria zikiwa like nying comment nying narud tenaaaaaa story time
 
Back
Top Bottom