OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,206
- 103,778
Katika hali ya kusikitika sana mwanzoni mwa mwaka huu nilipata na mkasa huu kama changamoto ktk profession yangu. Nikiwa mbele ya jopo la usaili(serikalini) la watu 6, huku wakipitia CV, pamoja na vyeti vya ''ukweli'' walipenda kujua ''who is my role model''. Kwa haraka nikataja watu wa3 ie Nyerere, Mandela na Dr.Slaa, lakini nikawaomba nijikite zaidi kwa Dr. Slaa kwa sababu namshuhudia tofauti na Nyerere ambaye nimeishia kumsoma tu kwenye vitabu maana 1999 wakati ndo kwanza nilikuwa la 4. Nilimchambua mzee huyu ''Dr.Slaa'' vizuri hasa ktk nyanja ya uongozi imara kwa kuwapa vijana nafasi na hamasa kubwa ktk ushiriki wa kujenga taifa lao pamoja na kuleta mageuzi ya sector zote.
Wana jopo walishtuka, na mmoja aliniambia wazi kuwa pamoja G.P.A 4.2, material niliyo-deliver mbele yao, wanasikitika kusema kuwa ''JINA LA DR.SLAA LIMEHARIBU KILA KITU'', hivyo nisitegemee simu. Niliwashukuru na kuwaomba watambue mchango wa Dr. Slaa hata bila ya uwepo wangu ktk ofisi yao