Nilikopa Tigo Niwezeshe ila simu imeibwa na nimebadili laini, nitatafutwa?

finance2014

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
314
79
Habari Wakuu niliibiwa simu katikati ya mwezi huu nikafanya maamuzi ya kubadili line sasa nilikuwa na deni la tigo niwezeshe la 160,000 lilipaswa kulipwa mwezi ujao.

Nauliza, je Tigo watanitafuta au nijisalimishe kuclear jina langu, kuna yeyote aliyewahi kubadili line akiwa na deni na hakutafutwa na mamlaka husika, msaada kwenye tuta.
 
Mimi Wananidai 680k
Ilikuwa kila nikirudisha kwa muda wananiongezea, Kuna Mwezi ikafika nimekwama kurudisha ontime, kawaida yao ukichelewa tuu hata Masaa, unaanza Mwanzo.

Ile hela nikaipata kesho yake, nikawaza Awamu hii nikilipa nisitarajie tena kupata chochote, Hapo ndio uvivu ukanianza ila sasa wakawa wanakata hela yoyote itakoyoingia kwenye simu, ikawa wanatuma tuu msg kunikumbusha kulipa, baada ya kama miezi miwili nikapoteza simu na ile laini, nikawa sipo hewani kwa laini ile 3 months (sikua tayari kupotezea ile laini)

Mwezi huu mwanzoni nikairenew, Juzi ndio wakanitumia msg ya deni langu, Now limepungua sababu mara nyingi nimekuwa nikijisahau naweka hela kule au mtu mkipatana atume basi anatumia namba hio...

Kwa ufupi namba naitumia na nitaendelea kuitumia na deni lao nitalipa taratibu, nilichowapendea sio wasumbufu... Ila uhuru ninaoukosa ni suala la kuwa makini kutoingiza hela TIGOPESA, wakati nishaizoea, kuanza kuongeza salio kwa njia ya Vocha ambayo nilishaisahau na watu wa dharura wanaohitaji kutuma pesa au kutumiwa kwa njia ya TIGOPESA.

Nakushauri Renew laini yao, lipa taratibu, kuwalipa haihitaji mpaka watumie mamlaka, rudisha fadhila kama ulivyosaidiwa.. Mimi sikutafuta laini nyingne yoyote na isitoshe sikuwa tayari kupotezea laini yangu watu wanayoifahamu kwa Zaidi ya 12yrs kwa deni la 680k.

Wakiona umesajili laini mpya hio inatosha kuwaaminisha umedhamiria kutowalipa pesa yao, na kama wana mfumo wa kukudaka basi hawatashindwa..

Pia kumbuka suala la wewe kupoteza laini hawalijui kwa sasa, ila wanaamini umeitupa baada ya kudhamiria kutolipa kama wakopaji wengi walivyo...

Uaminifu ni mhimili mkubwa sana hasa kipindi hiki ambacho kuupata ni kazi kubwa.

NOTE: Mawazo ya wao kusahau hilo deni au kutokutambua hata usiyawaze.
 
Hawana muda wa kukufatulia mi ni deni la 170k toka 2017 hadi leo hii sijalipa na line yangu naweka pesa na kutoa kama kawaida hawakati wala nini na ukithubutu kulipa basi hawata kukopesha tena pesa nyingi wataanza na elfu 20
 
Habari Wakuu niliibiwa simu katikati ya mwezi huu nikafanya maamuzi ya kubadili line sasa nilikuwa na deni la tigo niwezeshe la 160,000 lilipaswa kulipwa mwezi ujao.

Nauliza, je Tigo watanitafuta au nijisalimishe kuclear jina langu, kuna yeyote aliyewahi kubadili line akiwa na deni na hakutafutwa na mamlaka husika, msaada kwenye tuta.
Aliyekuibia amekusikia atakulipia tu usihofu.
 
Back
Top Bottom