Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike – sehemu ya 1

Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike – sehemu ya 1

Hadithi nzuri ila unapaswa kutoa CREDIT kwa mtunzi maana tunamjua anaitwa NYEMO CHILONGANI ni mwandishi wa hadithi kutoka Global na hadithi hii ilikuwa ikitoka katika Gazeti la Uwazi. USIFANYE JASHO LA MTU LAKO! Najua hujawasiliana naye...
 
ILIPOISHIA
Nikasikia sauti ile ikiniambia
niende ndani ya mochwari ile,
maelekezo mengine angeniambia,
nikafanya hivyo na kuanza
kuingia humo ambapo kulikuwa
na masanduku mengi yaliyokuwa
na maiti nyingi. Nikaambiwa
nisubiri. Nakuja kutahamaki, eti
ilikuwa saa sita usiku. Nikabaki
nikitetemeka tu.
SONGA NAYO
Ulikuwa usiku mkubwa, nakiri
kwamba hakukuwa na sehemu
iliyokuwa inatisha kama ilivyokuwa
mochwari. Ndani ya mochwari ile,
kulikuwa na majeneza ya maiti
ambazo zililetwa humo ndani na
nyingine tayari kwa kuchukuliwa
lakini pia kulikuwa na masanduku
mengi ambayo ndani yake
kulikuwa na maiti, baridi lililokuwa
humo ndani, lilikuwa kubwa mno.
Humo kulikuwa na walinzi wawili,
walikuwa wakilinda, nilijiuliza
walipata wapi ujasiri wa kuwa
ndani ya chumba kile, tena usiku
mzima huku wakionekana
kutokuwa na hofu hata kidogo.
Mimi, sikuwa nikionekana, yaani
hata niliposogea karibu yao,
hawakuwa wakiniona zaidi ya
kufanya vitu vyangu. Humo, ndipo
nilipojifunza kwamba kulikuwa na
mambo mengi yaliyokuwa
yakitokea.
Niliwaona watu wakija usiku
huohuo, walikuwa wakizungumza
na walinzi hao na kuwaambia shida
zao, wengine walifika kwa kuwa
walihitaji baadhi ya viungo kutoka
kwa maiti ili waende kufanya
mambo yao ya kishirikina.
Nilimuona mlinzi mmoja akitoka na
kwenda kwenye sanduku moja,
akalivuta kisha kuanza kuitoa maiti
iliyokuwa ndani. Mwili wangu
ulisisimka mno, sikuamini
nilichokuwa nikikiona, hofu ilinijaa
moyoni mwangu.
Mlinzi yule akaivua nguo maiti ile,
sikujua alichokuwa akikihitaji, yale
mambo ambayo nilikuwa
nikiyasoma kwenye vitabu vya
kusisimua, siku hiyo nilikuwa
nikiyaona kwa macho yangu.
Akachukua kisu ambacho
alikihifadhi sehemu maalum,
nyuma ya mlango na kisha kuanza
kukata kifundo cha mguu cha maiti
ile kwani ndicho kilichokuwa
kikihitajika kwa hali na mali.
Ninayoyazungumza hapa,
niliyashuhudia kwa macho yangu.
Mapigo yangu ya moyo yalikuwa
juu mno, japokuwa kile kilikuwa
kikifanywa kwa maiti lakini
niliogopa na kuionea huruma,
niliona kama ilikuwa ikionewa.
Alipomaliza, mlinzi akakichukua
kifundo cha mguu ule kisha kumpa
mwanaume aliyekuwa amekifuata
na kuondoka nacho. Walinzi
waligongesheana mikono, kila
mmoja alionekana kuwa na furaha.
Wala haukupita muda mrefu,
nikaona mlinzi mmoja akitoka nje.
Sikutaka kubaki ndani, wakati
namsubiria yule mganga, nilitaka
kujua ni kitu gani kingine
kilichokuwa kikitokea.
Nilimfuata mlinzi, alikwenda moja
kwa moja kwenye gari la kifahari,
Range SUV nyeusi na kuongea na
mtu aliyekuwa humo ndani.
Nilisogea kwani nilitaka
kuyasikiliza mazungumzo yao.
“Nahitaji maji ya maiti,” alisema
mzee aliyekuwa humo ndani ya
gari.
“Laki mbili! Hela ipo?” aliuliza
mlinzi yule.
“Ipo! Naomba ukaniwekee humu!”
Yule mzee sikuweza kumfahamu
kwa kipindi kile lakini sauti yake,
hapo baadaye nilimfahamu kwani
nilikutana naye mara kwa mara.
Baada ya kuzungumza hivyo,
akatoa kidumu na kumpa mlinzi
yule ambaye akakichukua na
kuondoka nacho.
Sikutaka kubaki hapo nje,
nikamfuata mlinzi mle mochwari
alipokwenda. Nilipoingia, nikakuta
akimwambia mwenzake kwamba
kulikuwa na dili jingine, kuna mtu
alifuata maji ya maiti.
“Hakuna tatizo! Twende kule
kwenye maiti za wiki iliyopita!”
alisema mlinzi aliyeletewa taarifa.
Wakatoka na kuelekea kwenye
moja ya masanduku yaliyokuwa
mwisho kabisa ambayo yalikuwa na
maiti zilizokuwa na muda mrefu
humo mochwari. Wakafungua
sanduku moja, wakatoa maiti ya
msichana na kuiweka juu ya meza
moja kisha kuanza kuiosha huku
wakikinga maji na kuyaweka katika
sufuria kubwa kabla ya kuyaweka
katika kidumu kile.
“Mungu! Kumbe haya ndiyo
yanayotokea!” nilijikuta nikisema.
Waliendelea na zoezi lao mpaka
walipomaliza na kujaza kile
kidumu, yule mlinzi akaelekea nje
na kumpa yule mzee, gari
likawashwa na kuondoka mahali
hapo.
Wakati ikiwa imefika saa nane
usiku, hapo ndipo mganga yule
akatokea na kunifuata. Kabla ya
kuzungumza lolote, akaniangalia
machoni, aliiona hofu niliyokuwa
nayo.
“Upo sawa?” aliniuliza.
“Ndiyo! Nipo sawa na nipo tayari
kwa kazi,” nilimwambia.
Alichokifanya mganga yule ni
kuuchukua usinga wake, akaanza
kuimba wimbo ambao sikuwa
nikiuelewa. Aliimba kwa sauti
kubwa iliyonifanya nione kama
wale walinzi wangesikia lakini
haikuwa hivyo.
Waliendelea kupiga stori huku
mganga yule akiendelea na wimbo
wake. Alipomaliza, akalifuata
sanduku moja, akalitoa pale
lilipokuwa. Nilibaki nikiwa
nimeduwaa tu, sikuamini
kilichokuwa kikiendelea, sanduku
lilikuwa zito lakini yeye
alivyolishika ilikuwa ni kama mtu
aliyeshika kikaratasi.
Akaliweka chini, akalifungua na
kisha kuiangalia maiti ile.
Niliogopa, hata kusogea kule
sikuweza. Wakati nimesimama
huku nikiwa nimeduwaa, yule
mganga akachukua unga fulani na
kuipaka maiti ile kisha kuanza
kuzungumza maneno ambayo
sikuyaelewa, ghafla katika hali
iliyonishtua nikaiona maiti ile
ikiinua mkono wake.
“Mungu wangu!” nilisema kwa
mshtuko, sikuamini kile
nilichokiona. Mganga yule
hakunyamaza, aliendelea
kuzungumza maneno yale, mbali
na mkono, ile maiti ikainuka kisha
kukaa kitako mlemle kwenye
sanduku. Mpaka kufikia hatua hiyo,
nilitamani kukimbia. Jasho
lilinitoka.
 
View attachment 438141

KWA jina ninaitwa Zakia Ramadhani, ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto kumi, mama yangu aliyeitwa Zubeda Hassani na baba yetu aliyeitwa Saidi Ramadhani ambaye hapo tulipokuwa tukiishi alijulikana zaidi kwa jina la Mzee Mkude.

Familia yetu ilikuwa miongoni mwa familia masikini zilizokuwa zikiishi katika Kijiji cha Mbingu kilichokuwa katika Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro. Hatukuwa na fedha, baba alikuwa mkulima mzuri wa mpunga, mara kwa mara aliamka asubuhi sana na kuelekea shambani kulima huku mama akibaki nyumbani akiandaa uji, unapoiva, ninaondoka naye na kuelekea huko shambani.

Maisha yalikuwa magumu, yalituumiza lakini hatukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kupambana usiku na mchana ili tupate angalau fedha za kufanya mambo yetu mengine. Maisha hayo ya kimasikini, niliyachukia sana, nilitamani kuwa na fedha na kuyabadilisha maisha hayo, baba yangu atembelee gari, awe na nyumba nzuri na kufanya biashara zitakazomuingizia fedha nyingi.

Hizo zilikuwa ndoto nilizoota kila siku, ndoto za utajiri lakini kwenye maisha halisi, bado tulikuwa masikini wa kutupwa. Kula kwetu haikuwa ya uhakika, kidogo maisha yanakuwa na ahueni wakati wa mavuno, hapo, tutakula na kushiba, tutanunuliwa nguo na kufanya mambo mengine lakini kwenye kipindi cha upandaji mpunga, tulikuwa kwenye wakati mgumu sana.

Wazazi wetu hawakujua kitu chochote kuhusu uzazi wa mpango na ndiyo maana walizaa watoto wengi tena waliokuwa na utofauti wa umri mdogo, mimi ambaye ndiye nilikuwa mtoto wa kwanza, nilikuwa na miaka ishirini, aliyenifuata ambaye ni mvulana aliyeitwa Husseni alikuwa na miaka kumi na tisa, yaani watoto wote kumi tulipishana kwa mwaka mmojammoja.

Sikuwa na elimu, sikubahatika kuingia darasani, wazazi wetu hawakuwa wamesoma na hawakuamini kama elimu inaweza kumsaidia mtu kupata mafanikio. Kipindi cha nyuma waliambiwa sana watupeleke shule kujifunza lakini wakakataa kwa kuamini kwamba hata usipokuwa na elimu, ukitafuta fedha, utazipata tu, cha msingi uwe na moyo wa kutafuta.

“Unaweza kwenda shule, ukapoteza fedha kumbe Mungu amekwishakuandikia maisha ya kitajiri hapo baadaye, uje kuolewa na milionea au hata wewe kupata fedha kupitia biashara nyingine,” aliniambia baba, tena kwa ujasiri huku akiniangalia machoni.

Nilichokigundua ni kwamba baba hakuwa na fedha, hakuwa na uwezo wa kutulipia ada na ndiyo maana hata sababu alizozitoa hazikuwa na msingihata kidogo. Sikutaka kuingilia, niliendelea kubaki nyumbani mpaka nilipofikia umri huo, sikuwahi hata kuingia darasani kusoma.

Miaka ishirini lakini bado niliendelea kuishi kwa wazazi. Sijui kama nilirogwa au la lakini ukweli ni kwamba kila mwanaume niliyekuwa naye aliniacha siku chache kabla ya ndoa kisha kumuoa mwanamke mwingine.

Nakumbuka nilikuwa na mwanaume aliyeitwa Hamisi Sultan. Huyu mwanaume alinipenda sana, alikuwa mkulima mzuri, alijituma sana kijijini kiasi cha kumiliki mashamba yake ya mpunga, wazazi wangu walimpenda lakini kitu cha ajabu kabisa kilichotushangaza, wiki mbili kabla ya kufunga ndoa, akaniacha na kumuoa mwanamke mwingine.

Iliniumiza moyoni, sikuwa na jinsi, nililia sana na mwisho wa siku nikasahau na kuendelea na maisha yangu. Mwanaume wa pili aliyefuata aliitwa Abdul Maliki. Alikuwa mzuri wa sura, nilimpenda sana na wiki tatu kabla ya kufunga ndoa, akaniacha na kumuoa mwanamke mwingine.

Hayo yote yaliyotokea, yaliniumiza mno, sikuamini kama mimi ndiye niliyekuwa nikipitia maisha hayo. Hawakuishia wanaume hao tu, walikuja wengine kama watatu lakini matokeo yalikuwa yaleyale, kila aliyetaka kuniona, wiki chache kabla ya kufunga ndoa, aliniacha.

Sikutaka kukubali, nilichokifanya ni kufanya uchunguzi wa kujua tatizo lilikuwa nini, nilichogundua ni kwamba sababu kubwa ilikuwa ni umasikini na pia familia kuwa kubwa ilisababisha. Wanaume waliogopa kunioa kwa kuwa walijua kwamba sisi ni masikini, familia ya watoto kumi ilikuwa kubwa kiasi kwamba wakaona kama wangenioa, basi wangebebeshwa mzigo mkubwa wa kuitunza familia.

Nikakata tamaa ya kuolewa, sikuona kama kuna mwanaume mwingine angekuja na kunioa. Nililia usiku kucha, nilimlaumu Mungu lakini pamoja na kulia kote, lawama zote nilizozitoa, ukweli ukabaki palepale kwamba hakukuwa na mwanaume aliyetaka kunioa.

“Yaani sababu ya umasikini tu? Yaani sababu ya kuwa na familia kubwa tu?” nilijiuliza maswali mawili, majibu yake yalikuwa yenye kuumiza mno.

Maisha yaliendelea, hapo kijijini kulikuwa na familia nyingine zilizokuwa na uwezo kifedha, zilikuwa na nyumba zenye mabati, nyumba zao zilijengwa kwa matofali, hizohizo familia ndizo zilizotuletea dharau sisi masikini.

Kulikuwa na mambo mengi yaliyoniumiza, ila hili, lilikuwa la kwanza. Sikuona sababu ya kudharaulika kwa kuwa hatukuwa na fedha, sikuona sababu ya wazazi wangu kudharaulika kwa kuwa tu kila siku walivaa mavazi yaliyochakaa. Nilitaka na sisi tupewe heshima kama watu wengine, tupendwe na kuthaminiwa kama watu wengine ila hayo yote, yasingewezekana bila kuwa na fedha.

“Baba, hizi dharau zitakwisha lini?” nilimuuliza baba.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia kesho hapa kujua kitakachoendelea katika sehemu ya pili.

Haya Hadithi Mpya ya kusisimuwa ukiweka (Like) nitaendelea kuweka uhondo wa hadithi Mpya kazi kwenu wasomaji.
tarajia kufa
 
Mzizi mkavu vipi mwendelezo wa hadithi yetu pendwa
 
Back
Top Bottom