Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike – sehemu ya 1

Nilifanya Mapenzi Na Maiti 20 Nitajirike – sehemu ya 1

ILIPOISHIA
Nikasikia sauti ile ikiniambia
niende ndani ya mochwari ile,
maelekezo mengine angeniambia,
nikafanya hivyo na kuanza
kuingia humo ambapo kulikuwa
na masanduku mengi yaliyokuwa
na maiti nyingi. Nikaambiwa
nisubiri. Nakuja kutahamaki, eti
ilikuwa saa sita usiku. Nikabaki
nikitetemeka tu.
SONGA NAYO
Ulikuwa usiku mkubwa, nakiri
kwamba hakukuwa na sehemu
iliyokuwa inatisha kama ilivyokuwa
mochwari. Ndani ya mochwari ile,
kulikuwa na majeneza ya maiti
ambazo zililetwa humo ndani na
nyingine tayari kwa kuchukuliwa
lakini pia kulikuwa na masanduku
mengi ambayo ndani yake
kulikuwa na maiti, baridi lililokuwa
humo ndani, lilikuwa kubwa mno.
Humo kulikuwa na walinzi wawili,
walikuwa wakilinda, nilijiuliza
walipata wapi ujasiri wa kuwa
ndani ya chumba kile, tena usiku
mzima huku wakionekana
kutokuwa na hofu hata kidogo.
Mimi, sikuwa nikionekana, yaani
hata niliposogea karibu yao,
hawakuwa wakiniona zaidi ya
kufanya vitu vyangu. Humo, ndipo
nilipojifunza kwamba kulikuwa na
mambo mengi yaliyokuwa
yakitokea.
Niliwaona watu wakija usiku
huohuo, walikuwa wakizungumza
na walinzi hao na kuwaambia shida
zao, wengine walifika kwa kuwa
walihitaji baadhi ya viungo kutoka
kwa maiti ili waende kufanya
mambo yao ya kishirikina.
Nilimuona mlinzi mmoja akitoka na
kwenda kwenye sanduku moja,
akalivuta kisha kuanza kuitoa maiti
iliyokuwa ndani. Mwili wangu
ulisisimka mno, sikuamini
nilichokuwa nikikiona, hofu ilinijaa
moyoni mwangu.
Mlinzi yule akaivua nguo maiti ile,
sikujua alichokuwa akikihitaji, yale
mambo ambayo nilikuwa
nikiyasoma kwenye vitabu vya
kusisimua, siku hiyo nilikuwa
nikiyaona kwa macho yangu.
Akachukua kisu ambacho
alikihifadhi sehemu maalum,
nyuma ya mlango na kisha kuanza
kukata kifundo cha mguu cha maiti
ile kwani ndicho kilichokuwa
kikihitajika kwa hali na mali.
Ninayoyazungumza hapa,
niliyashuhudia kwa macho yangu.
Mapigo yangu ya moyo yalikuwa
juu mno, japokuwa kile kilikuwa
kikifanywa kwa maiti lakini
niliogopa na kuionea huruma,
niliona kama ilikuwa ikionewa.
Alipomaliza, mlinzi akakichukua
kifundo cha mguu ule kisha kumpa
mwanaume aliyekuwa amekifuata
na kuondoka nacho. Walinzi
waligongesheana mikono, kila
mmoja alionekana kuwa na furaha.
Wala haukupita muda mrefu,
nikaona mlinzi mmoja akitoka nje.
Sikutaka kubaki ndani, wakati
namsubiria yule mganga, nilitaka
kujua ni kitu gani kingine
kilichokuwa kikitokea.
Nilimfuata mlinzi, alikwenda moja
kwa moja kwenye gari la kifahari,
Range SUV nyeusi na kuongea na
mtu aliyekuwa humo ndani.
Nilisogea kwani nilitaka
kuyasikiliza mazungumzo yao.
“Nahitaji maji ya maiti,” alisema
mzee aliyekuwa humo ndani ya
gari.
“Laki mbili! Hela ipo?” aliuliza
mlinzi yule.
“Ipo! Naomba ukaniwekee humu!”
Yule mzee sikuweza kumfahamu
kwa kipindi kile lakini sauti yake,
hapo baadaye nilimfahamu kwani
nilikutana naye mara kwa mara.
Baada ya kuzungumza hivyo,
akatoa kidumu na kumpa mlinzi
yule ambaye akakichukua na
kuondoka nacho.
Sikutaka kubaki hapo nje,
nikamfuata mlinzi mle mochwari
alipokwenda. Nilipoingia, nikakuta
akimwambia mwenzake kwamba
kulikuwa na dili jingine, kuna mtu
alifuata maji ya maiti.
“Hakuna tatizo! Twende kule
kwenye maiti za wiki iliyopita!”
alisema mlinzi aliyeletewa taarifa.
Wakatoka na kuelekea kwenye
moja ya masanduku yaliyokuwa
mwisho kabisa ambayo yalikuwa na
maiti zilizokuwa na muda mrefu
humo mochwari. Wakafungua
sanduku moja, wakatoa maiti ya
msichana na kuiweka juu ya meza
moja kisha kuanza kuiosha huku
wakikinga maji na kuyaweka katika
sufuria kubwa kabla ya kuyaweka
katika kidumu kile.
“Mungu! Kumbe haya ndiyo
yanayotokea!” nilijikuta nikisema.
Waliendelea na zoezi lao mpaka
walipomaliza na kujaza kile
kidumu, yule mlinzi akaelekea nje
na kumpa yule mzee, gari
likawashwa na kuondoka mahali
hapo.
Wakati ikiwa imefika saa nane
usiku, hapo ndipo mganga yule
akatokea na kunifuata. Kabla ya
kuzungumza lolote, akaniangalia
machoni, aliiona hofu niliyokuwa
nayo.
“Upo sawa?” aliniuliza.
“Ndiyo! Nipo sawa na nipo tayari
kwa kazi,” nilimwambia.
Alichokifanya mganga yule ni
kuuchukua usinga wake, akaanza
kuimba wimbo ambao sikuwa
nikiuelewa. Aliimba kwa sauti
kubwa iliyonifanya nione kama
wale walinzi wangesikia lakini
haikuwa hivyo.
Waliendelea kupiga stori huku
mganga yule akiendelea na wimbo
wake. Alipomaliza, akalifuata
sanduku moja, akalitoa pale
lilipokuwa. Nilibaki nikiwa
nimeduwaa tu, sikuamini
kilichokuwa kikiendelea, sanduku
lilikuwa zito lakini yeye
alivyolishika ilikuwa ni kama mtu
aliyeshika kikaratasi.
Akaliweka chini, akalifungua na
kisha kuiangalia maiti ile.
Niliogopa, hata kusogea kule
sikuweza. Wakati nimesimama
huku nikiwa nimeduwaa, yule
mganga akachukua unga fulani na
kuipaka maiti ile kisha kuanza
kuzungumza maneno ambayo
sikuyaelewa, ghafla katika hali
iliyonishtua nikaiona maiti ile
ikiinua mkono wake.
“Mungu wangu!” nilisema kwa
mshtuko, sikuamini kile
nilichokiona. Mganga yule
hakunyamaza, aliendelea
kuzungumza maneno yale, mbali
na mkono, ile maiti ikainuka kisha
kukaa kitako mlemle kwenye
sanduku. Mpaka kufikia hatua hiyo,
nilitamani kukimbia. Jasho
lilinitoka.
 
Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 Nitajirike – 10

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA
“Huu una masharti makubwa
mawili,” aliniambia mganga.
“Yapi?”
“Moja, unatakiwa kuwaua wazazi
wako wote wawili,” aliniambia
huku akikishika kitunguli kidogo
kilichokuwa pembeni yake.
“Kuwaua wazazi wangu?”
“Ndiyo!”
“Na sharti jingine?” niliuliza
huku nikionekana
kuchanganyikiwa.”
“Kufanya mapenzi na maiti
ishirini..” aliniambia.
MWAGIKA NAYO HAPA…
Kwanza nikashtuka, sikuonekana
kuamini kile alichoniambia,
nikamuuliza mara mbilimbi
alisemaje, yeye akaniambia vilevile
kwamba nilitakiwa kufanya
mapenzi na maiti ishirini kama
nilitaka kuwa tajiri, hivyo
nilitakiwa kuchagua.
“Umechagua nini?”
“Kati ya nini na nini?”
“Kuwaua wazazi wako au kufanya
mapenzi na maiti ishirini?”
alinijibu kwa kuniuliza swali.
“Bora nifanye mapenzi na maiti
ishirini…” nilimwambia japokuwa
niliogopa mno.
Alichokifanya mzee yule ni
kuchukua unga mwingine na
kunipaka usoni kisha kuniambia
nitulie kwa muda. Nilitulia
hapohapo, sijui nini kilitokea,
ghafla, nikajikuta nikitokea katika
hospitali moja kubwa hapa jijini
Dar es Salaam, nilishangaa,
nilijiuliza nilifikikaje mahali hapo
lakini sikuwa na jibu lolote lile.
Kulikuwa na watu wengi waliokuwa
wakiendelea na shughuli zao,
wagonjwa waliokuwa wakiingia na
kutoka. Ghafla, nikasikia sauti ya
yule mzee ikiniambia kwamba
nilitakiwa kwenda mochwari,
sikujua ilikuwa wapi lakini
nikajikuta nikijiongoza mpaka
kufika katika mlango ambao
uliandikwa MOCHWARI kwa nje.
“Subiri hapo mpaka usiku,”
niliisikia sauti hiyo.
Nilifanya kama nilivyoambiwa,
nikasubiri mahali hapo. Ilikuwa
jioni kama saa kumi na moja hivi.
Hakukuwa na mtu aliyeniona,
wengi walinipita bila kunisalimia.
Ilipofika saa moja usiku, nikasikia
sauti ile ikiniambia niende ndani ya
mochwari ile, maelekezo mengine
angeniambia, nikafanya hivyo na
kuanza kuingia humo ambapo
kulikuwa na masanduku mengi
yaliyokuwa na maiti nyingi.
Nikaambiwa nisubiri. Nakuja
kutahamaki, eti ilikuwa saa sita
usiku. Nikabaki nikitetemeka tu.
*****
Ulikuwa usiku mkubwa, nakiri
kwamba hakukuwa na sehemu
iliyokuwa inatisha kama ilivyokuwa
mochwari. Ndani ya mochwari ile,
kulikuwa na majeneza ya maiti
ambazo zililetwa humo ndani na
nyingine tayari kwa kuchukuliwa
lakini pia kulikuwa na masanduku
mengi ambayo ndani yake
kulikuwa na maiti, baridi lililokuwa
humo ndani, lilikuwa kubwa mno.
Humo kulikuwa na walinzi wawili,
walikuwa wakilinda, nilijiuliza
walipata wapi ujasiri wa kuwa
ndani ya chumba kile, tena usiku
mzima huku wakionekana
kutokuwa na hofu hata kidogo.
Mimi, sikuwa nikionekana, yaani
hata niliposogea karibu yao,
hawakuwa wakiniona zaidi ya
kufanya vitu vyangu. Humo, ndipo
nilipojifunza kwamba kulikuwa na
mambo mengi yaliyokuwa
yakitokea.
Niliwaona watu wakija usiku
huohuo, walikuwa wakizungumza
na walinzi hao na kuwaambia shida
zao, wengine walifika kwa kuwa
walihitaji baadhi ya viungo kutoka
kwa maiti ili waende kufanya
mambo yao ya kishirikina.
Nilimuona mlinzi mmoja akitoka na
kwenda kwenye sanduku moja,
akalivuta kisha kuanza kuitoa maiti
iliyokuwa humo ndani. Mwili
wangu ulisisimka mno, sikuamini
nilichokuwa nikikiona, hofu ilinijaa
moyoni mwangu.
Mlinzi yule akaivua nguo maiti ile,
sikujua alichokuwa akikihitaji, yale
mambo ambayo nilikuwa
nikiyasoma kwenye vitabu vya
kusisimua, siku hiyo nilikuwa
nikiyaona kwa macho yangu.
Akachukua kisu ambacho
alikihifadhi sehemu maalumu,
nyuma ya mlango na kisha kuanza
kukata kifundo cha mguu cha maiti
ile kwani ndicho kilichokuwa
kikihitajika kwa hali na mali.
Ninayoyazungumza hapa,
niliyashuhudia kwa macho yangu.
Mapigo yangu ya moyo yalikuwa
juu mno, japokuwa kile kilikuwa
kikifanywa kwa maiti lakini
niliogopa na kuionea huruma,
niliona kama ilikuwa ikionewa.
Alipomaliza, mlinzi akakichukua
kifundo cha mguu ule na kisha
kumpa mwanaume aliyekuwa
amekifuata na kuondoka nacho.
Walinzi waligongesheana mikono,
kila mmoja alionekana kuwa na
furaha.
Wala haukupita muda mrefu,
nikaona mlinzi mmoja akitoka nje.
Sikutaka kubaki ndani, wakati
namsubiria yule mganga, nilitaka
kujua ni kitu gani kingine
kilichokuwa kikitokea.
Nilimfuata mlinzi, alikwenda moja
kwa moja kwenye gari moja ya
kifahari, Range SUV nyeusi na
kuongea na mtu aliyekuwa humo
ndani. Nilisogea kwani nilitaka
kuyasikiliza mazungumzo yao.
“Nahitaji maji ya maiti,” alisema
mzee aliyekuwa humo ndani ya
gari.
“Laki mbili! Hela ipo?” aliuliza
mlinzi yule.
“Ipo! Naomba ukaniwekee humu!”
Yule mzee sikuweza kumfahamu
kwa kipindi kile lakini sauti yake,
hapo baadaye nilimfahamu kwani
nilikutana naye mara kwa mara.
Baada ya kuzungumza hivyo,
akatoa kidumu na kumpa mlinzi
yule ambaye akakichukua na
kuondoka nacho.
Sikutaka kubaki hapo nje,
nikamfuata mlinzi mule mochwari
alipokwenda. Nilipoingia, nikakuta
akimwambia mwenzake kwamba
kulikuwa na dili jingine, kuna mtu
alifuata maji ya maiti.
“Hakuna tatizo! Twende kule
kwenye maiti za wiki iliyopita!”
alisema mlinzi aliyeletewa taarifa.
****
Je, nini kitaendelea? Usikose
kufuatilia kesho hapa kujua
kitakachoendelea katika sehemu
ya 11
 
Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 nitajirike – 11

ILIPOISHIA SEHEMU YA 10
YULE mzee sikuweza kumfahamu
kwa kipindi kile lakini sauti
yake, hapo baadaye nilimfahamu
kwani nilikutana naye mara kwa
mara. Baada ya kuzungumza
hivyo, akatoa kidumu na kumpa
mlinzi yule ambaye akakichukua
na kuondoka nacho.
Sikutaka kubaki hapo nje,
nikamfuata mlinzi mule
mochwari alipokwenda.
Nilipoingia, nikakuta
akimwambia mwenzake kwamba
kulikuwa na dili jingine, kuna
mtu alifuata maji ya maiti.
“Hakuna tatizo! Twende kule
kwenye maiti za wiki iliyopita!”
alisema mlinzi aliyeletewa
taarifa.
MWAGIKA NAYO HAPA…
Wakatoka na kuelekea kwenye
moja ya masanduku yaliyokuwa
mwisho kabisa ambayo yalikuwa na
maiti zilizokuwa na muda mrefu
humo mochwari. Wakafungua
sanduku moja, wakatoa maiti ya
msichana na kuiweka juu ya meza
moja kisha kuanza kuiosha huku
wakikinga maji na kuyaweka katika
sufuria kubwa kabla ya kuyaweka
katika kidumu kile.
“Mungu! Kumbe haya ndiyo
yanayotokea!” nilijikuta nikisema.
Waliendelea na zoezi lao mpaka
walipomaliza na kujaza kile
kidumu, yule mlinzi akaelekea nje
na kumpa yule mzee, gari
likawashwa na kuondoka mahali
hapo.
Wakati ikiwa imefika saa nane
usiku, hapo ndipo mganga yule
akatokea hapo ndani na kunifuata.
Kabla ya kuzungumza lolote,
akaniangalia machoni, aliiona hofu
niliyokuwa nayo.
“Upo sawa?” aliniuliza.
“Ndiyo! Nipo sawa na nipo tayari
kwa kazi,” nilimwambia.
Alichokifanya mganga yule ni
kuuchukua usinga wake, akaanza
kuimba wimbo ambao sikuwa
nikiuelewa. Aliimba kwa sauti
kubwa iliyonifanya nione kama
wale walinzi wangesikia lakini
haikuwa hivyo.
Waliendelea kupiga stori huku
mganga yule akiendelea na wimbo
wake. Alipomaliza, akalifuata
sanduku moja, akalitoa pale
lilipokuwa. Nilibaki nikiwa
nimeduwaa tu, sikuamini
kilichokuwa kikiendelea, sanduku
lilikuwa zito lakini yeye
alivyolishika ilikuwa ni kama mtu
aliyeshika kikaratasi.
Akaliweka chini, akalifungua na
kisha kuiangalia maiti ile.
Niliogopa, hata kusogea kule
sikuweza. Wakati nimesimama
huku nikiwa nimeduwaa, yule
mganga akachukua unga fulani na
kuipaka maiti ile kisha kuanza
kuzungumza maneno ambayo
sikuyaelewa, ghafla, katika hali
iliyonishtua, nikaiona maiti ile
ikiinua mkono wake.
“Mungu wangu!” nilisema kwa
mshtuko, sikuamini kile
nilichokiona. Mganga yule
hakunyamaza, aliendelea
kuzungumza maneno yale, mbali
na mkono, ile maiti ikainuka na
kisha kukaa kitako mulemule
kwenye sanduku. Mpaka kufikia
hatua hiyo, nilitamani kukimbia.
Jasho lilinitoka.
Kuna kipindi nilihisi kile
kilichokuwa kikitokea kilikuwa ni
ndoto, nilitamani kukimbia lakini
miguu ilikuwa mizito.
Kadiri muda ulivyozidi kusonga
mbele ndivyo nilivyozidi kushikwa
na hofu. Kumbuka kwamba hiyo
ilikuwa usiku wa manane, tena
tukiwa mochwari, najua
umeshapata picha ni jinsi gani
nilikuwa na hofu moyoni mwangu.
Yule mganga hakunyamaza, akawa
anazungumza maneno ambayo
sikuyaelewa kabisa. Aliponitupia
macho niliyahamisha yangu na
kuiangalia ile maiti iliyokuwa
imeketi kitako kama mtu aliyekuwa
akitaka kuzungumza na yule
mganga.
“Usiogope Zakia,” aliniambia huku
akiniangalia lakini nilikuwa na
hofu.
Nikaanza kuyakumbuka maneno ya
yule mganga aliyoniambia kipindi
cha nyuma kwamba kama kweli
nilitaka kuwa tajiri basi ilinibidi
nikubali sharti la kufanya mapenzi
na maiti ishirini, kwa hiyo ile maiti
iliyokuwa mbele yangu ilikuwa ya
kwanza.
Nilikubali lakini ndani ya mochwari
ile lilionekana kuwa jambo gumu
mno, kufanya mapenzi na maiti.
Tena kama ile iliyokuwa ikitisha
iliyoonekana kabla ya kuwa maiti,
mtu huyo alipata ajali mbaya,
kama si gari, basi ilikuwa treni
kwani mwili wake ulikuwa na
majeraha mengi.
“Njoo huku,” aliniambia yule
mganga, nikaanza kusogea kule
alipokuwa.
Akaniambia nikae kwanza,
nilitakiwa kuvuta pumzi na
sikutakiwa kuogopa. Nilikuwa
kimya, nilikuwa na hofu sana
nikiogopa.
Maiti ile ikafumbua macho yake na
kuanza kuniangalia, kuna kipindi
nilikuwa nikijiuliza kama kweli ile
ilikuwa maiti au nilikuwa
nikichezewa mchezo. Majibu ya
Swali langu hilo lilipatikana kila
nilipokuwa nikiuangalia mwili
wake, ilionesha dhahiri kwamba
ilikuwa maiti.
“Upo tayari?” aliniuliza mganga.
“Ndiyo! Ila….”
“Ila nini tena?”
“Nitaweza kweli?”
“Usijali! Utaweza. Kwani hujawahi
kufanya mapenzi na mwanaume?”
aliuliza mganga huku akiniangalia
usoni.
“Nimewahi!”
“Basi jua hakuna tatizo,”
aliniambia.
Nilibaki nikimwangalia tu, kuna
kipindi nilijuta kwa nini nilitaka
kuwa tajiri na wakati masharti ya
utajiri wenyewe yalikuwa magumu
kiasi hiki. Nilibaki nikisononeka
lakini kumbuka kwamba nilitamani
kuwa tajiri hivyo chochote
kilichokuwa kinatokea mbele
yangu, nilikubaliana nacho.
“Vua nguo zako,” aliniambia.
Wakati hayo yakiendelea ndani ya
mochwari, wale walinzi hawakuwa
wakijua kitu chochote kile,
hawakutuona hivyo kufanya kila
kitu kwa kujiachia. Baada ya
kumaliza kuvua nguo zangu na
kubaki kama nilivyozaliwa,
akaniambia nipande juu ya meza,
nikafanya hivyo, nikalala chali.
Ndugu yangu, ninachokwambia
hapa ni kweli kabisa, kilinitokea
katika maisha yangu, kipindi kile
nilipokuwa nikisaka utajiri kwa udi
na uvumba. Ghafla nikaiona maiti
ile ikisimama kutoka ndani ya
sanduku na kuanza kuvua nguo
zake zilizokuwa
zimechanikachanika kutokana na
ajali, baada ya hapo, akapanda pale
juu.
“Mkimaliza, utatoka nje, hili
sanduku usiwe na hofu nalo,
litarudi tu lilipokuwa,” aliniambia
yule mganga na kisha yeye kutoka
ndani ya mochwari ile na kwenda
kunisubiri nje.
****
Je, nini kitaendelea? Usikose
kufuatilia kesho hapa kujua
kitakachoendelea katika sehemu
ya 12
 
ILIPOISHIA
Sikutaka kubaki humo,
nilichokifanya ni kuinuka, kuvaa
nguo zangu na kutoka ndani ya
mochwari ile. Walinzi walikuwa
wakipiga stori, sikujali, nikatoka
mpaka nje, nilipofika huko,
nikamkuta mganga akiwa na
tabasamu pana kabisa huku
akitingisha kichwa chake juu chini,
chini juu kuonesha kukubaliana na
kile kilichofanyika.
SONGA NAYO
Mganga alinipa uhakika kwamba
kila kitu kingekuwa kama
kilivyotakiwa kuwa. Kwa kweli
nilimwamini sana na kuona kuwa
hivi karibuni ningekuwa tajiri
mkubwa mno nchini Tanzania na
hivyo kurudi kijijini nikiwa shujaa.
Siku iliyofuata, mganga akaniambia
nirudi nilipokuwa nikiishi ambapo
sikutakiwa kumwambia mtu yeyote
juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
Sasa ratiba ikawa ni kwenda kwa
mganga kila siku, ananichukua
kimazingara na kunipeleka
mochwari ambapo kama kawaida
nilikuwa nikiendelea kufanya
mapenzi na maiti.
Siku ya kwanza niliogopa sana
lakini siku zilivyokwenda, hofu
ikaniondoka na hivyo kuwa na
ushujaa mkubwa moyoni mwangu.
Nilipitia mengi kipindi hicho,
wakati mwingine nililetewa maiti
zilizoungua moto, zilitisha sana
lakini ilikuwa ni lazima nifanye
nazo mapenzi, wakati mwingine
nililetewa maiti zilizopata majanga
mengine, zote hizo, nilivumilia.
Siku zilikatika mpaka nilipobakiza
maiti moja. Mganga akaniambia
kwamba hiyo sikutakiwa kufanya
nayo kule mochwari bali nilitakiwa
kufanya nayo sehemu nyingine
kabisa, tena makaburini.
Kwa kweli niliogopa sana, sikujua
kitu kilichonitisha kwani kiukweli
kati ya makaburini na mochwari,
mochwari kulitisha zaidi. Usiku,
mganga akanichukua na kunipeleka
katika makaburi fulani yaliyokuwa
jijini Dar. Nilipofika karibu na
makaburi hayo, akaniambia niingie
ndani ya eneo la makaburi kisha
kuelekea katika kaburi la jamaa
mmoja aliyekufa miaka kumi
iliyopita, huyo jamaa aliitwa
Samweli Ramadhani.
“Nitalijuaje?”
“Utalijua tu, una uwezo mkubwa wa
kulijua kaburi hilo, wewe nenda,”
aliniambia mganga.
Wakati nimeingia ndani ya eneo la
kaburi hilo, kwa macho yangu
niliweza kuwaona wachawi,
walikuwa zaidi ya ishirini,
walisimama pembeni ya kaburi
moja la mtoto ambapo maiti yake
ilikuwa ikihitajika sana.
Sikujua kwa nini, sikufika pale
kuwafuatilia wachawi wale
niliowaona ila wao hawakuniona,
nilifika pale nikiwa na mambo
yangu, hivyo sikujali. Nilitembea
kwa tahadhari, makaburini
kulitisha sana, kulisisimua sana.
Nilipofika katika kaburi moja,
nikasimama, sikujua kama lilikuwa
lenyewe au jingine, nikasogelea
kuangalia jina, nikakuta
limeandikwa Samweli Ramadhani,
nikashangaa, nimejuaje kama hilo
kaburi ndilo lenyewe.
“Ila kwa nini maiti hii?” nilijiuliza,
ghafla nikasikia mganga akinijibu.
“Kwa imani zetu wanadamu,
tunasema jina la Samweli ni la
Kikristo na Ramadhani ni la
Kiislamu, hivyo ukifanya mapenzi
na maiti hii, Wakristo na Waislamu
wote watakuheshimu na utajiri
wako utamsisimua kila mtu,”
nilimsikia vema mganga huyo.
Nilisimama huku nikiwa sijui nini
cha kufanya, nilisubiri maelekezo,
nikaisikia sauti ya mganga
ikiniambia nisubiri, nikafanya
hivyo, ghafla, katika hali ambayo
sikuitarajia, nikaona hirizi kubwa
ikiwa imefungwa kiunoni mwangu,
ilikuwa nzito, kilichonishangaza,
hirizi ile kama ilikuwa na moyo,
kwani niliweza kuyasikia mapigo
kama ya moyo yakidunda kutoka
katika hirizi hiyo.
Ghafla, upepo mkali ukaanza
kuvuma mahali hapo, matawi ya
miti iliyokuwa makaburini
yakaanza kuyumbishwa huku na
kule. Nikasikia kelele za watu
wengi, sikujua zilitoka wapi lakini
nilizisikia masikioni mwangu.
Nikaanza kutetemeka, mara
nikahisi kama kuna mtu alikuwa
nyuma yangu, sikugeuka kujua
alikuwa nani, mtu huyo
akanisogelea na kunishika bega
kwa nyuma, pumzi zake nilisikia
vema karibu kabisa na masikio
yangu. Nikashindwa kuvumilia,
nikageuka, cha kushangaza
sikumuona mtu.
Wakati nikiendelea kutetemeka
kaburini pale, ghafla nikaliona lile
kaburi likianza kujifukua lenyewe
ndani yake kulikuwa na jeneza
likiwa limefunguliwa lakini
halikuwa na maiti, nikashangaa
sana.
Ghafla mwili wangu ukaanza
kusisimka, nikahisi tena nyuma
yangu kulikuwa na mtu, nilitaka
kugeuka, nikashindwa kufanya
hivyo, nikahisi nikishikwa bega kwa
nyuma, nilitetemeka zaidi, kijasho
chembamba kikanitoka mno.
“Unanukia vizuri mpenzi wangu!”
nilisikia sauti hiyo nyuma yangu,
nikazidi kutetemeka.
“Wewe nani?” nilijikuta nikiuliza
huku mihemo ya mtu huyo ikisikika
vema nyuma yangu.
 
SONGA NAYO
Nliuliza swali hilo huku
nikitetemeka sana, nilitamani
nipotee na kutokea sehemu tofauti
na hiyo. Mwili haukuacha
kusisimka, kuna kipindi niliyasikia
kabisa mapigo ya moyo
yalivyokuwa yakidunda kwa nguvu.
“Mimi ni mpenzi wako uliyemfuata
hapa makaburini, una ngozi laini
sana, hakika wewe ni mwanamke
wa ndoto yangu,” niliendelea
kuisikia sauti hiyo.
Mara mguso wa mtu huyo
ukahama kutoka begani mwangu
na kuanza kuelekea chini, nilizidi
kutetemeka mno, mikono yake
ikahamia katika mgongo wangu na
kuanza kuushikashika, baadaye
akahamia katika kiuno changu,
nikabaki nikianza kulegea mwili
wangu.
“Ni kipindi kirefu kimepita, miaka
kumi pasipo kumgusa mwanamke
yeyote yule, upo tayari mpenzi
wangu?” aliniuliza.
Sikumjibu, nilibaki kimya, wakati
nikiwa nimesimama vilevile, ghafla
nikaanza kuona mazingira ya
mahali pale yakianza kuondoka na
mazingira mengine kuingia.
Mbele yangu kukaonekana kuwa na
kitanda kikubwa, ndani ya chumba
kikubwa, alichonifanya ni
kunisukumia kitandani, niliona
kweli nimeangukia kitandani, ila
ukweli ni kwamba niliangukia
ndani ya kaburi lake, kitanda,
lilikuwa jeneza lake, alichokifanya,
naye akaja kwa juu yangu
mgongoni, nikajigeuza ili nimuone,
sikumuona, ila miguso yake,
ilionesha alikuwa hapo pamoja
nami kwani yeye ndiye alianza
kunivua nguo, yaani nalivuliwa
nguo na mtu nisiyemuona.
Nilitakiwa kutulia vilevile,
kumbuka kwamba nilifanya
mapenzi na maiti kumi na tisa na
hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho,
hivyo niliona kuwa na sababu zote
za kutulia kwani baada ya hapo,
nilikuwa na uhakika wa kupata
utajiri kama alivyoniambia mganga
yule.
Ndani ya kaburi lile ndipo
tulipoanza kufanya mapenzi, maiti
ile ilikuwa ikinuka sana, sikuwa
nikiiona ila niliihisi miguso yake
kila kona katika mwili wangu.
Nilifanya naye mapenzi kwa saa
moja ndipo akamaliza, nikahisi
akiondoka mahali hapo na kuisikia
sauti ya mganga ikinipongeza kwa
kazi nzuri niliyoifanya, sasa
ningekuwa tajiri mkubwa.
“Umefanikiwa, sasa utakuwa tajiri
mkubwa tu,” nilisikia sauti ya
mganga.
Nilichokifanya ni kutoka nje ya
kaburi na kuvaa nguo zangu.
Kilichonishangaza, ghafla nikaanza
kuona moshi mzito ukifuka kutoka
ndani ya kaburi lile, sikujua nini
kiliendelea, moshi ule mzito
ukalifunika kaburi lote hata
lisionekane, wakati nashangaa
ghafla moshi ule ukakatika na
kaburi lile kujifukia kama
lilivyokuwa mwanzo.
Sikutaka kubaki mahali hapo,
nikatoka na kuelekea nje ya eneo la
kaburi lile huku tayari ikiwa ni saa
nane usiku. Nilimkuta mganga
akiwa amekaa pembeni akinisubiri,
aliponiona, kwanza akatoa
tabasamu pana, nikamsogelea.
“Hongera sana, hakika umenifanya
nijisikie fahari sana,” aliniambia
mganga yule.
“Kwa hiyo lini nitapata utajiri?”
“Utaanza kesho, ila nataka ufanye
kitu.”
“Kitu gani?”
“Biashara yoyote ile…”
“Mmh!”
“Ndiyo hivyo! Utakapoanza, amini
kwamba ndipo utajiri
utakapoanzia,” aliniambia huku
akinikazia macho.
Nilichokiamini ni kwamba mara
baada ya kufanikiwa kufanya
mapenzi na maiti zile basi
ningepata utajiri kwa kukuta begi
la fedha likiwa sehemu kumbe
sivyo.
Akaniambia natakiwa kufanya
biashara ambayo ndiyo ingekuwa
chanzo cha utajiri wangu, sikuwa
na jinsi, japo kwa shingo upande,
nikakubaliana naye. Na hivyo
kuondoka mahali hapo.
Siku iliyofuata, nikamwambia
Dickson pale Ubungo kwamba
nilitaka kufanya biashara na
biashara yenyewe ambayo
niliichagua ilikuwa ni kuuza
magazeti, akanikubalia hivyo
kutafuta meza na kuanza kufanya
harakati zote za kuhakikisha
magazeti yanauzwa mara moja.
Siku mbili zilizofuata, tayari
nilikuwa na meza yangu, niliweka
juu magazeti mengi, nikatafuta
vitabu vya hadithi na kutulia. Kitu
cha ajabu ambacho sikuwahi
kukiona ni pale watu walipoanza
kumiminika katika meza yangu na
kuanza kununua magazeti.
Nilishangaa, huwa ni vigumu kwa
magazeti kumalizika kwa saa moja,
lakini huwezi kuamini, magazeti
mia moja niliyopewa, yote yaliishia
ndani ya saa moja tu. Si mimi
niliyeshangaa, hata watu wengine
wa pale walishangaa pia.
Haikuwa kawaida kabisa na sidhani
kama iliwahi kutokea. Magazeti
yakaisha lakini nikashangaa watu
wengine wakija mezani kwangu,
waliiona meza ikiwa tupu ila
wakawa wananiuliza kuhusu
magazeti, yapo au yamekwisha,
nilishangaa, meza ilikuwa tupu,
sehemu zingine zilikuwa na
magazeti, kwa nini hawakwenda
huko?
Huo ulikuwa mwanzo, niliendelea
kufanya biashara ya kuuza
magazeti, ikaanza kuyabadilisha
maisha yangu, nikawa naongezewa
magazeti mengi, nikaanza kuyaona
maisha yakianza kubadilika, fedha
ziliingia, baadaye nikaanzisha
biashara nyingine ya kuuza juisi na
maji, hiyo ndiyo iliyoniingizia fedha
zaidi na hivyo kupanga chumba
Manzese Midizini.
Naweza kusema huo ulikuwa
mwanzo tu, ndani ya miezi mitatu
tangu nianze kufanya biashara
hizo, nikashangaa nikiwa na akiba
ya milioni tatu chumbani kwangu.
Sikujua nilizipataje, ila nilichokijua
ni kwamba kulikuwa na nguvu
fulani nyuma yangu, nikafanikiwa
zaidi.
Ulipoingia mwezi wa tano tangu
nifanye biashara hizo, nikajikuta
nikiwa na milioni tano. Nikashtuka,
utajiri ukaanza kuninyemelea
pasipo kukumbuka kwamba
unapokuwa na utajiri wa kishetani
huwa huna furaha, huna amani ni
utajiri unaotesa na kuumiza mno.
Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea.
Mara ya kwanza, sikujali, ila
baadaye, nilikuja kujuta kwa nini
nilitaka utajiri.
 
ILIPOISHIA
Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea.
Mara ya kwanza, sikujali, ila
baadaye, nilikuja kujuta kwa nini
nilitaka utajiri.
SONGA NAYO
Kusema ukweli hakukuwa na
kipindi nilichokuwa na furaha
kama kipindi hicho, sikuamini
kilichokuwa kikiendelea, maskini
mimi, niliyeishi maisha ya ufukara
mkubwa mkoani Morogoro, eti leo
hii nilikuwa na mamilioni ndani ya
chumba changu.
Maisha yalibadilika kabisa,
nilifanya biashara kwa kujituma
kiasi kwamba hakukuwa na mtu
aliyehisi fedha zangu zilikuwa za
kishirikina, nilitaka niwe tajiri
mkubwa, mwenye biashara nyingi,
niingize hata milioni mia moja kwa
mwezi.
Nilijitahidi kufungua biashara
mbalimbali tena zilizoniingizia
fedha. Fedha zilimiminika,
hakukuwa na aliyejua kilichokuwa
kikiendelea zaidi ya Dickson tu
ambaye alikuwa rafiki yangu wa
karibu na ndiye aliyenipokea mara
baada ya kufika Dar es Salaam.
Nilifanikiwa sana, nikaanza
mipango ya kujenga nyumba yangu
kubwa maeneo ya Goba huku
nikinunua gari zuri kwa ajili ya
kutembelea. Ndiyo hivyo, maisha
yalibadilika na nilikuwa na kila
sababu ya kutumbua pesa
nilivyotaka.
Nakwambia kuhusu maisha yangu,
nakwambia kwamba inawezekana
kupata utajiri wa kishirikina lakini
kamwe utajiri huo mwisho wake
huwa mbaya mno. Niliwahi
kuzungumza na watu wengi, najua
nchi yetu imejaa maskini lakini
kamwe usithubutu kupata utajiri
kwa njia za kishirikina kwani huwa
na gharama yake, shetani hatoi kitu
pasipo kukuumiza, hatoi kitu pasipo
kukupa masharti ambayo anajua
kwamba utashindwa tu.
Wengi waliniona kama mwanamke
anayejua kufanya biashara sana
pasipo kujua nyuma ya maisha yale
kulikuwa na nguvu kubwa ya
kishetani. Kumbuka kwamba
familia yangu ilikuwa maskini sana,
wazazi wangu walihangaika
kwenda shambani kila siku
asubuhi, hivyo nilikuwa na kila
sababu ya kuwasaidia.
Nilichokifanya baada ya siku
kadhaa ni kurudi kijijini kwetu,
sikupanda basi, nilitumia gari
langu binafsi, Harrier nyeusi, mpya
kabisa. Sikutaka kwenda kijijini
moja kwa moja, nilitaka kupitia
Ifakara kuonana na Mudi, yule
mwanaume, utingo aliyenisaidia
kiasi cha fedha kilichonifikisha Dar
es Salaam, unamkumbuka?
Nilipofika Ifakara, nikaelekea
mpaka katika kituo cha daladala.
Wanaume wote wakabaki
wakiniangalia kwa matamanio,
nilikuwa mrembo mno, niliyenukia
fedha kila nilipopita, walinitamani
lakini kwa kuniangalia tu,
hawakuona kama nilistahili kuwa
nao.
“Unamuulizia Mudi anayeishi
Mazobezobe?” aliniuliza
mwanaume mmoja.
“Ndiyo! Yupo wapi?”
“Ametoka, ila msubiri, atarudi
muda si mrefu, amekwenda
Zilimpompa,” aliniambia kijana
huyo, Zilimpompa ulikuwa mmoja
wa mitaa hapo Ifakara.
Sikuwa na jinsi, sikutaka kuondoka
mahali hapo, nakumbuka niliwahi
kumwambia Mudi kwamba
nilikuwa nikielekea Dar kutafuta
utajiri na kuna siku ningekuwa
tajiri, hakuwa akiamini, alinisaidia
lakini najua aliona kwamba
nakwenda Dar kupoteza muda,
kujiuza na kufanya mambo
mengine.
Leo hii nilirudi tena kwake, sikuwa
Zakia yule maskini, nilikuwa Zakia
mwenye pesa, niliyeendesha gari,
niliyejipulizia manukato ya The
Princess ambayo yalikuwa ni zaidi
ya shilingi laki tano, nilikuwa na
gari la kifahari, yaani kila
nilichokuwa nacho, kilionesha
kwamba nilikuwa na pesa.
Baada ya saa moja, huku nikiwa
garini nimesinzia, mara nikasikia
kioo cha gari langu kikigongwa,
nilipoyafumbua macho yangu na
kumwangalia mgongaji, alikuwa
Mudi. Uso wake ulikuwa kwenye
mshangao mkubwa, kwanza
hakunijua mimi nilikuwa nani,
nikakishusha kioo.
“Mudi, mambo vipi?” nilimsalimia
huku nikimuonesha tabasamu
pana.
“Poa,” alinijibu huku uso wake
ukiwa kwenye maswali mengi.
“Unanikumbuka?”
“Hapana! Wewe unanijua?”
alinijibu na kunitupia swali.
“Jamani mpenzi! Kweli
hunikumbuki?” nilimuuliza huku
nikimfungulia mlango na kumtaka
aingie.
Akaingia, alionekana kujishtukia
sana, alikuwa mchafu, mavazi yake
yalichakaa sana. Humo, bado
alikuwa na maswali mengi, mimi
nilikuwa nani na kwa nini nilimuita
ndani ya gari? Hapo ndipo
nikamuweka wazi kwamba mimi
nilikuwa Zakia, mwanamke yule wa
miezi kadhaa iliyopita ambaye
nilikuwa na safari ya kwenda Dar.
“Zakia! Ni wewe?” aliniuliza huku
akinishangaa.
“Ndiyo! Nimeona nije kukusalimia,”
nilimwambia.
“Imekuwaje tena?”
“Nini jamani?”
“Kuwa hivyo!”
“Hahaha! Nilikwambia nakwenda
Dar kutafuta utajiri, si unaona
nimeupata,” nilimwambia huku
nikitoa tabasamu.
Alibaki akinishangaa, sikutaka
kujali sana, nilimwambia kwamba
siku hiyo nilikuwa mgeni wake,
nilitaka kulala naye, kumbuka
alinisaidia nauli, elfu hamsini,
nilitaka nimlipe, siyo fedha bali
kumpa mapenzi motomoto ambayo
asingeweza kuyasahau maisha yake
yote.
Tukaondoka na kuelekea katika
hoteli moja iliyokuwepo hapo
Ifakara, nikachukua chumba na
kuingia chumbani, tulipofika,
akakaa kitandani, akavua nguo,
akaenda bafuni, ila aliporudi,
nikashangaa sana, hakuwa yule
Mudi ninayemfahamu, alibadilika
na kuwa moja ya maiti niliyowahi
kufanya nayo mapenzi, maiti
iliyojaa damu ambayo nguo zake tu
zilionesha kwamba alipata ajali.
Nikashtuka sana!
“Kuna nini mpenzi?” aliniuliza
swali hilo, hapohapo nikamuona
akibadilika na kuwa Mudi.
Kiukweli nilichanganyikiwa sana,
nilitetemeka mwili mzima na kuhisi
mwili wangu kama umepigwa shoti
fulani ya umeme. Mudi
akanisogelea, akanitupa kitandani
na kutulia juu yangu. Nilibaki
nikimwangalia kwa macho yenye
kurembua, tayari nilianza kuingia
katika ulimwengu mwingine wa
mahaba.
“Unanukia vizuri mpenzi wangu…”
aliniambia, ghafla nikashtuka.
Maneno kama hayo niliambiwa na
maiti ile ya kule makaburini
kipindi alichotaka kufanya mapenzi
na mimi. Maneno yaleyale ndiyo
aliyoyazungumza Mudi, karibu
kabisa na masikio yangu.
“Nashukuru!” nilijibu huku
nikiachia tabasamu pana lenye
hofu.
“Umetafuta sana utajiri, hakika
utakuwa zaidi ya hapa,
ninachokitaka ni wewe kuwa
mpenzi wangu milele,” alisema
Mudi.
Kiukweli alinichanganya sana,
hapohapo nikamuona akitoka
katika sura ya Mudi na kurudi
katika sura ya moja ya maiti
niliyowahi kufanya nayo mapenzi
mochwari, hakika ilinitisha sana.
Nikataka nijitoe pale kitandani,
akanikandamiza zaidi. Nikahisi
kifua kikianza kubana na pumzi
kuanza kukata.
Je, Zakia atafanyaje na kwa nini
alitokewa na maiti aliyowahi
kufanyanayo mapenzi?
 
ILIPOISHIA
Kiukweli alinichanganya sana,
hapohapo nikamuona akitoka
katika sura ya Mudi na kurudi
katika sura ya moja ya maiti
niliyowahi kufanya nayo mapenzi
mochwari, hakika ilinitisha sana.
Nikataka nijitoe pale kitandani,
akanikandamiza zaidi. Nikahisi
kifua kikianza kubana na pumzi
kuanza kukata.
SONGA NAYO
Bado macho yangu yalikuwa
yakiiona maiti juu yangu, ilikuwa
imenikandamiza vilivyo pale
nilipolala, sikumuona Mudi kabisa,
nilijitahidi kujitoa kutoka hapo
kitandani lakini nilishindwa.
Nilianza kuhema juujuu, kuna
wakati nilihisi kama ningekufa
kwani nilibanwa sana kiasi kwamba
nguvu zikaanza kuniisha mwilini
mwangu. Wakati sura ile
ikiendelea kuwa ya hiyo maiti,
ghafla ikabadilika na kuwa sura ya
Mudi, nilishangaa, hata kule
kubanwa kote kukatoka.
“Kuna nini?” aliniuliza Mudi huku
akiniangalia usoni.
“Hakuna kitu,” nilijibu huku
nikionekana kuwa na hofu kubwa
usoni mwangu.
“Hapana! Kutakuwa na tatizo, kuna
nini?” aliniuliza Mudi huku akiwa
amenikazia macho.
Ni kweli kulikuwa na tatizo lakini
sikutaka kumwambia, najua
hakuwa akifahamu lolote lile,
niliiona maiti lakini kama
ningemwambia kuwa nimeiona
maiti badala ya kumuona yeye,
angenifikiriaje?
Nilijaribu kumwambia kwamba
hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo
angeendelea kama kawaida yake.
Tulifanya mapenzi siku hiyo,
sikutaka kuondoka, nililala na Mudi
hotelini hapo huku usiku mzima
nikiota ndoto za ajabu, mara
nakimbizwa makaburini na watu
waliovalia mashuka meupe, mara
nakuchukuliwa na kupelekwa
mochwari kisha kuingizwa katika
masanduku ya kuhifadhia maiti.
Mpaka tunaamka asubuhi, niliota
ndoto mbili, zote zilikuwa za
kutisha mno, sikujua kwa nini
ilikuwa hivyo, nilitamani nipate
majibu juu ya ndoto zile kwamba
kwa nini kipindi cha nyuma sikuwa
naota ndoto mbaya ila kipindi
hicho zilikuwa zikija mfululizo?
Sikutaka kujali japokuwa moyo
wangu ulikuwa na hofu kubwa.
Asubuhi hiyo tukanywa chai na
kumwambia Mudi kwamba
ningeondoka kuelekea katika kijiji
chetu cha Mbingu.
“Ni lazima niondoke mpenzi,”
nilimwambia kwa sauti ndogo,
ilikuwa kama saa nne asubuhi.
“Sawa! Ila ningependa niendelee
kuwa nawe, ila haina jinsi, kwenda
kuwaona wazazi ni jambo la msingi
sana,” aliniambia kwa unyonge
ambao ulinionesha kwamba hata
yeye hakupenda kuniona
nikiondoka.
Hakukuwa na jinsi, ilikuwa ni
lazima niondoke kuendelea na
safari yangu. Tulipoagana na
kwenda ndani ya gari langu,
nikatulia, nikauegemea usukani na
kuanza kufikiria kile kilichokuwa
kikiendelea katika maisha yangu.
“Tatizo nini tena?’ nilijiuliza lakini
sikupata jibu.
Sikutaka kubaki mahali hapo,
nikaondoka na kuendelea na safari.
Njiani, sikuwa na furaha hata
kidogo, wakati nikiwa nimebakiza
kilometa kumi kabla ya kufika
kijijini, nikashangaa kuona gari
likipunguza mwendo kisha
kusimama pembezoni mwa
barabara.
Nilishangaa, gari hilo halikuwa
bovu, kulikuwa na mafuta ya
kutosha, sasa kwa nini lilipunguza
mwendo na kisha kujizima, nilibaki
nikijiuliza sana lakini hata kabla
sijapata jibu, niliisikia sauti ya mtu
ikiniambia niangalie nyuma kwani
kulikuwa na kitu.
Haraka nikayapeleka macho yangu
katika siti za nyuma, nilichokiona
ni boksi dogo likiwa limefungwa
vizuri. Kwanza nikashtuka, sikujua
ni nani aliliweka boksi hilo na
ndani kulikuwa na nini.
Niliamini hakukuwa na mtu
aliyekuwa na uwezo wa kufungua
mlango wa gari langu kisha kuingia
ndani kwani ufunguo nilikuwa nao,
sasa nani alidiriki kuufungua
mlango na kuliweka boksi hilo?
Nikakosa jibu.
Nikatoka hapo mbele na kuelekea
nyuma, boksi lile liliandikwa jina
langu kwa juu, nilikuwa na hofu
kubwa lakini nilitakiwa kufungua,
ilikuwa ni lazima nijue ndani
kulikuwa na nini kwa nini lilikuwa
ndani ya gari langu.
Wakati nimelichukua boksi hilo,
cha kushangaza kabisa mapigo
yangu ya moyo yakaanza kudunda
kwa nguvu mno, kijasho
chembamba kikaanza kunitiririka,
sikujua sababu ya kuwa kwenye
hali hiyo, kumbuka hapo ilikuwa
porini, nilizungukwa na miti kila
kona, sikuogopa kuwa hapo, ila hilo
boksi ndilo lililonitia hofu.
Nikafungua na kuangalia ndani.
Kitu nilichokutana nacho,
kilinishtua sana, kulikuwa na kisu
kilichofungwa kitambaa chekundu
katika mpini wake, nikajiuliza
sababu ya kisu hicho kuwa garini
mwangu ilikuwa nini?
“Umekiona hicho kisu?” niliisikia
sauti ya mganga, niliangalia huku
na kule, sikuona mtu, nikashangaa.
“Ndiyo mkuu!”
“Unatakiwa kutoa sadaka moja kila
baada ya miezi miwili,” nilimsikia
akiniambia.
“Sadaka?”
“Ndiyo! Bado tuna kazi kubwa na
wewe, ni lazima ufanye
tunachokuagiza ili utajirike zaidi,”
aliniambia.
“Tuna?”
“Ndiyo! Sipo peke yangu, mimi na
watu wa giza,” aliniambia.
“Watu wa giza?”
“Ndiyo!”
“Akina nani?”
“Waliokupa utajiri,” alinijibu.
Hakika nilishangaa sana, maneno
aliyoniambia kama sikuwa
nikiyaelewa, ilikuwaje aseme
kwamba yeye alishirikiana na watu
wengine katika kunipa utajiri na
wakati nilichokijua ni kwamba yeye
peke yake ndiye aliyenipa utajiri
huo?
Nilishangaa sana lakini bado
sikuridhika, nilitaka kujua zaidi
kuhusu hizo sadaka alizosema
kwamba nilitakiwa kuzitoa,
zilikuwa sadaka za nini? Fedha au?
“Ni lazima uue?” nilisikia sauti hiyo
ikinipa majibu.
“Niue?”
“Ndiyo! Utajiri uliokuwa nao ni
utajiri wa damu, huwezi kuwa nao
milele mpaka utakapotoa damu, ni
lazima uue kila baada ya miezi
miwili, hakika utajiri utaongezeka
na kuwa mwanamke tajiri kuliko
wote nchini Tanzania,” aliniambia.
“Mimi niue?”
“Ndiyo! Hakika hautamfuata mtu
na kumuua, angalia tena kwenye
boksi,” iliniambia sauti hiyo, haraka
nikaangalia, macho yangu
yakakutana na kioo.
“Unakiona hicho kioo? Kichukue,
kiangalie, unaona nini?” iliniuliza,
nikakichukua na kuanza
kukiangalia, sikuiona taswira
yangu, taswira ambayo niliiona
ilikuwa ni ya baba yangu.
“Ichome taswira hiyo kwa hicho
kisu,” iliniambia.
“Unasemaje?” niliuliza huku jasho
likinitiririka, hakika niliogopa
kwani nilijua kwamba endapo
ningeichoma taswira ile, basi baba
yangu angekufa.
“Ichome…” sauti ya mganga
iliniambia, nikabaki nikitetemeka.
 
ILIPOISHIA:
“Ichome taswira hiyo kwa hicho
kisu,” iliniambia.
“Unasemaje?” niliuliza huku jasho
likinitiririka, hakika niliogopa
kwani nilijua kwamba endapo
ningeichoma taswira ile, basi baba
yangu angekufa.
“Ichome…” sauti ya mganga
iliniambia, nikabaki nikitetemeka.
SONGA NAYO…
Nilibaki nikitetemeka, sikujua ni
kitu gani nilitakiwa nikifanye
mahali hapo. Jinsi mganga yule
alivyoniambia kwamba niichome
taswira ya picha ya baba yangu
katika kioo kile.
Kumuua baba yangu? Kilikuwa kitu
kisichowezekana kabisa,
nilikumbuka namna alivyokuwa
akiyasumbukia maisha yangu
kipindi cha nyuma, nilikumbuka
jinsi alivyokuwa akijinyima kwa
ajili yangu, yaani nipate maisha
mazuri, hakujali kama alikuwa
akila au la, alichokijali ni mimi kula
na kulala sehemu nzuri.
Nilifanikiwa, nilitaka nimuoneshe
baba kwamba hatimaye ule
umasikini uliokuwa umetutafuna
kwa kipindi kirefu usingekuwepo
tena, nilitaka niwaoneshe wanakijiji
kwamba kitendo changu cha
kuondoka nyumbani kwetu na
kwenda kijijini kilikuwa sahihi
kwani kile nilichokitaka, tayari
nilikipata.
Nilibaki nikiiangalia taswira ile,
mawazo yote hayo yalinijia
kichwani mwangu wakati ambao
nilishika kisu kile. Mapigo ya moyo
yalikuwa juu mpaka kuhisi kwamba
kama angepita mtu yeyote mahali
hapo basi angeyasikia kwa jinsi
yalivyokuwa yakidunda.
“Zakia, ichome taswira hiyo,”
niliisikia sauti ya mganga huyo.
“Siwezi… nashindwa,” nilisema
pasipo kuogopa kitu chochote kile.
“Kwa nini unashindwa?” aliniuliza.
“Nilitafuta utajiri kwa ajili ya
wazazi wangu, sasa kwa nini
nimuue na wakati kila kitu
nilichokuwa nacho naye alitakiwa
kukiona?” niliuliza swali nililoliona
kuwa na hoja, ila kwa mganga
huyo, halikuwa na hoja yoyote ile.
“Basi acha tuuchukue utajiri wetu,
utarudi na kuwa masikini, tena
masikini mkubwa zaidi ya
ulivyokuwa,” aliniambia mganga
yule.
Nilichanganyikiwa, sikutaka
kuuachia utajiri ule kwani tayari
nilishaonja utamu wake, nilitaka
kuwa nao milele, yaani hata maisha
baada ya kifo kama kungekuwa na
matumizi ya fedha basi
nitakapokufa niende nao kwani
ulikuwa mtamu mno.
Kitendo cha kuniambia maneno
hayo, nikashindwa kuvumilia,
sikuwa tayari kuona utajiri huo
ukiondoka mikononi mwangu,
ilikuwa ni lazima nimuue baba
yangu.
Kwanza nikafikiria kwamba
alikuwa mzee, hakuwa na nguvu za
kutosha, kama ningemuacha basi
mwaka huohuo hapo baadaye
ilikuwa ni lazima afariki kwani
umri ulikuwa umekwenda sana.
Kitendo cha kufikiria hayo,
nikashangaa kupata majibu
kwamba ilikuwa ni lazima nimuue,
kama nisingemuua mimi basi
angekufa miezi michache ijayo.
Sikutaka kujiuliza tena, mawazo
hayo yakanipa nguvu na hivyo
kuchoma taswira ile. Nilipomaliza,
mganga akaniambia niwashe gari,
nikawasha na kuanza kuondoka
mahali hapo.
Nilichukua saa mbili, nikafika
katika Kijiji cha Mbingu. Kwanza
wanakijiji walipoliona gari hilo,
walishangaa sana, hakukuwa na
gari lolote la kifahari lililowahi
kufika kijijini hapo, magari yote
ambayo yaliwahi kufika yalikuwa
yale ya mizigo ambayo yalifuata
nafaka hapo kijijini, sasa watu
wakawa wanajiuliza, je, huyo
aliyeingia na gari la kifahari ni
nani?
Sikutaka kuteremka, unapofika
kijijini kwetu, kwa jinsi ilivyokuwa
ilikuwa vigumu sana kufika na gari
mpaka karibu na nyumba yetu,
ilikuwa ni lazima ufikie mbali,
uteremke na kuanza kutembea
kuelekea huko.
Watoto na watu wengine
walishasogea mahali gari
lilipokuwa na kuanza kuliangalia.
Hawakujua ndani ya gari hilo
kulikuwa na nani kwani vioo vya
gari hilo vilikuwa ‘tinted’.
Najua walikuwa na maswali,
nilichokifanya baada ya kukaa
ndani ya gari kwa dakika kama
tano, nikateremka, wengi
waliponiona, hawakunifahamu,
kwa jinsi nilivyovaa, miwani yangu
na nguo za thamani, hakukuwa
hata na mtu mmoja aliyehisi
kwamba mwanamke huyo
aliyekuwa akitembea nilikuwa
mimi.
“Huyu ni Mzungu?” nilimsikia
mtoto mmoja akiuliza, watoto
wengine walikuwa wakinifuata kwa
nyuma.
Nilitembea mpaka nilipofika karibu
na nyumba yetu, kilichonishtua
ambacho sikuwa nikikumbuka ni
msiba uliokuwepo. Watu zaidi ya
hamsini walikuwa mahali hapo,
nilisikia vilio kutoka kwa watu
kadhaa waliokusanyika nyumbani
kwetu, nilishangaa lakini baada ya
kukumbuka kwamba niliichoma
taswira ya baba katika kioo kile
nilichopewa ndani ya gari, moyo
wangu uliumia sana kwani
niligundua kwamba mimi ndiye
niliyemuua baba yangu.
“Baba amekufa! Nimemuua baba!”
nilijisemea moyoni na kuanza
kuelekea kule walipokusanyika
watu wengi.
Wanaume wengi ndiyo waliokuwa
wamekusanyika mbele ya nyumba
yetu, kama walivyokuwa watu
wengine kule nilikopaki gari, hata
hapo hakukuwa na yeyote
aliyegundua kwamba msichana
aliyefika, ambaye alivalia kisasa
alikuwa ni yule Zakia aliyeondoka
mwaka mmoja uliopita.
Nilisalimia, wakabaki
wakinishangaa, nikaingia ndani,
nikaelekea mpaka chumbani
ambapo nilikuta ndugu zangu
kadhaa wakiwa na mama yangu.
Hakukuwa na mtu aliyenigundua
zaidi ya mama ambaye baada ya
kuniona tu, kilio kikaongezeka, kila
mtu akabaki akijiuliza mimi ni
nani.
Moyo wangu uliumia mno,
sikuamini nilichokuwa nikikona,
sikuwahi kumuona mama yangu
akilia kama siku hiyo, nilijuta, mimi
ndiye niliyemuua baba kwa sababu
ya tamaa za kubaki na utajiri
niliokuwa nao.
Nikaungana nao, nikajitambulisha
kwamba nilikuwa nani, watu wote
wakashangaa. Kitu cha ajabu
kabisa kutokea, moyo wangu
haukuwa na maumivu makubwa
sana, nilisikitika kwa kuwa baba
alifariki lakini kusema kwamba
nilie sana kama watu wengine,
kwangu haikutokea kabisa.
Watu walinishangaa, walijiuliza
sana kuhusu mimi, nilionekana
kabisa kwamba nilikuwa na fedha,
nilikuwa na utajiri mkubwa,
sikutoka ndani, nilibaki nikiwafariji
wengine, harakati zote zikaendelea
siku hiyo, saa kumi jioni, tukaenda
kuzika katika makaburi ya kijiji na
kisha kurudi.
Kila niliyemwangalia, alionekana
kuwa na hamu ya kufahamu utajiri
mkubwa namna hiyo niliutoa wapi?
Kwani hata gari nililokuwa nalo,
lilikuwa gumzo sana kijiji kizima na
hata vijiji vya jirani. Eti yule Zakia
aliyekataliwa kuolewa na wanaume
kibao, leo alikuwa tajiri!
Haikuwaingia akilini.
 
Damu ya mtu kila baada ya miezi miwili si atamaliza ukoo wote?? Bado utakufa vile vile...yani upate utajiri kwa mateso uishi nao kwa matezo still ufe kwa mateso pia... Waiiii
 
Back
Top Bottom