Nilidanganya kuwa mama amefariki ili nipate msaada, roho yangu inahuzunika sana

TUENDELEE..

Wakati nasubiri matokeo ya kidato Cha nne nilienda arusha kufanya kibarua Cha kulisha ng'ombe. Jamani ng'ombe wa kisasa wanakula! Yaani sikutarajia Kama kazi ingekuwa ngumu hivyo. Ng'ombe walikuwa Saba. Kuwalisha tu asubuhi moja ni mziki. Na wanalishwa asubuhi, mchana na jioni, mbaya zaidi wanapenda kulia Lia na kila wakilia boss anawaka kinyamaa anadai ng'ombe Wana njaa Hata Kama ndio nimetoka kuwalisha, mshahara ni elfu 40 kwa mwez! Nilivvokuwa mgeni nilona Kama Kazi inataka kunishinda lakini kadri siku zinavyoenda nikaanza kuzoea kazi hivyo nikakomaa nayo maana sikuwa na alternative.

Kulikuwa na duka naagizwa kupeleka maziwa ya Bill kila asubuhi na jioni na kuna mda napita hapo mchana kununua pumba. Siku moja nimepitia apo dukani Kuna chalii akaja akanipiga teke. Nimegeuka Wala sikuuliza nikamrukia teke la kifua Hadi akaanguka chini. Nikainua jiwe kubwa kabla sijamuangushia Kuna ustadhi akatoke akanizuia. Yule chalii akaamka akakimbia. Siku zikasonga yule ustadhi nilikuwa namuona Mara nyingi pale kijiweni. Siku moja mchana akaniita akaniambia Kuna deal anataka tuongee nikamwambia ntarudi baada ya nusu saa. Nikaenda maskani fasta nikawanywesha ng'ombe maji nikarudi kijiweni. Nilimkuta ustadhi ananisubiri akaniuliza unapendelea kula Nini mchana huu nikamwambia ugali na nyama choma akaagiza tukala. Sasa wakati tunakula akawa ananipamba na maujiko ooh Mara kijana unaonekana jasiri Sana, ooh Mara kijana unaonekana mpambanaji Sana me nikawa naitikia tu kwamba ni kweli.. ni kweli. Akaniuliza unafanya Kazi gani apa mjini nikamwambia ukweli kwa kila kitu maana me nilidhani Kuna mchongo anataka kuniunganishia. Baada ya kunihoji mda mrefu akaanza kunishawishi kwamba Kuna Kazi atanipa itakayobadili kabisa maisha yangu laki inatakiwa niwe mwanaume kamili. Aliniuliza Mara nyingi Kama nipo tayari, binafsi nikajua bila shaka ni Kazi ya madawa ya kulevya maana kabla ya hapo niliwahi kusikia stori kwamba biashara ya madawa ya kulevya Ina utajiri wa haraka.

Tuliagana kwamba niendelee kujitafakari Kama Nina uwezo wa kuhimili Kazi yenye malipo makubwa au niendelee kuwa maskini. Binafsi nilimwambia nipo tayari kuanza Kazi Hata siku hiyohiyo lakini akasisitiza niendelee kujitafakari lakini iwe siri nikamwambia poaa akachukua namba yangu tukaagana, hiyo ilikuwa mwanzoni mwa mwezi March, 2015.

Mwishoni mwa mwezi huo akanitafuta tuonane, Mara hii tulionana kwenye ukumbi wa hoteli moja kali Sana pale arusha mjini. Nilimkuta yule Jamaa, round hii akiwa amevaa suti kali na amenyoa ndevu, Yuko na wenzake wawili tulisalimiana wakanikaribisha nikae,stori za hapa na pale baada ya Kama dakika 20 wakaja vijana wengine wanne jumla tukawa watu nane. Tulipiga msosi ambao ni adimu Sana kwangu na baadae wakaanza kutu motivate kwamba kuuaga umaskini ni kitu kinachowezakana kwa mda mfupi jambo ambalo lilinifanya nifurahi Sana baada ya hapo tulipewa kila mtu shiling elfu hamsini bure na tukaambiwa tukutane kesho yake kwenye bustani flani hapo arusha mjini. Nilifurahi Sana na nikaanza ku imagine jinsi nitakavyofanya Kazi kwa bidii na kuachana na umaskini. mda wote nilikuwa nadhani ni Kazi ya madawa ya kulevya. Kesho yake tukakutana baada ya stori mbili tatu jamaa akatuchana live kwamba Kazi ni kuilinda maslahi ya Somalia dhidi ya udhalimu wanaofanywa, na tutatakiwa kwenda kwenye kozi ya miezi mitatu kabla ya kusajiliwa.alsema tukiwa kwenye kozi tutakuwa tunalipwa elfu 50 kila siku na tukishamaliza kozi tutakuwa tunalipwa laki tatu kila siku! Niliogopa kidogo lakini nikiwaza wingi wa hizo tarakimu na nikilinganisha Kazi ngumu ninazofanya kwa ujira wa elfu 40 kwa mwezi, automatically uwoga unaisha kabisa. Tulipewa kila mtu elfu 50 na tukaambiwa tujiandae mda wowote tutatakiwa kusafirishwa kwenda somalia sehemu inayoitwa Ghuba ya Aden.

Mnamo April, 2 vyombo vya habari vilitangaza kwamba Kuna shambulizi la kigaidi limetukea Chuo kikuu Cha Garisa nchini Kenya na kugharimu maisha ya watu zaidi ya mia moja. Baada ya siku chache tulisikia kwamba wachache Kati ya magaidi waliokamatwa mmoja wao ni Mtanzania tena alikuwa ni mwanafuzi wa kidato Cha tano, Bihawana Dodoma! Hapo nikapata picha kwamba, awa jamaa ni Al-shabaab na mchezo wao ni kuwarubuni vijana wa masikini kijiunga na ugaidi. Kutokana na idadi hiyo ya vifo vya watu wasio na hatia, nikajihoji nikaona nisije nikapoteza uelekeo wa maisha yangu kwa sababu ya ahadi za utajiri ambao hakuna mwenye uhakika kwamba nitapata. Nikabadili mawazo na nikavunja sim card yangu ili wale jamaa wasinipate hewani, nikabadili ratiba za kwenda dukani, nikamuomba chalii flani awe anapeleka maziwa dukani badala yangu.

Siku zilisonga matokeo ya mtihani yalitoka nimefanya vizuri na baada ya miezi michache nikapangwa kidato Cha tano. Niliwaaga rasmi familia ya boss wangu nikaanza mchakato wa kwenda shule. Yule dada aliyekuwa ananisomesha alihamishwa kikazi mkoa mwingine lakini Marafiki zake wananifahamu hivyo walipopata habari kwamba natakiwa kwenda shule walinichangia nikafanikiwa kijiunga na kidato Cha tano.

Mwaka wa kwanza ulienda vizuri, mziki ulikuja kuwa tofauti nilipoingia kidato Cha sita.niliishiwa na sikuwa na pesa za matumizi, nikiwapigia wale watu wangu mda mwingi wanakuwa busy. Ilifika wakati nikawa Hata sabuni ya kufulia Sina nikawa naamka usiku wa manane kupita kwe mabafu na kukusanya vipande vya sabuni vilivyobaki baada ya watu kuoga, nilivifinyanga kwa pamoja Kama tonge la ugali, Sasa unakuta zingine ni yeusi zingine nyeupe ivyo yaani nafua usiku wa manane ili watu wasijue. Naamka alfaniri naoga navaa uniform nakaa standby, mswaki mfukoni wenzangu wakianza kujiandaa atakayefungua tranka nagongea mafuta ya kujipaka, mwingine atakayefungua tranka nagongea dawa ya meno, naenda jalalani naokota zile counter book yaliyotupwa yameandikwa nusu, nakata natumia upande uliobaki ivyo yaani siku zinasogea.

Kadri siku zinavyosonga ndio Hali ikazidi kuwa tete washkaji masnitch wakaanza kuniongea kwa madem zao hamu ya kusoma ikaisha kabisa nilitamani ningejiungaga na wale jamaa wa somalia lakini Sina namba zao tena, nikatamani nirudi mtaani kupiga vibarua yaani mawazo yakawa yana bishana yenyewe kwa yenyewe kichwani

Itaendelea...
WW ND ULIINGIA CHAKIKE WALE WAKIKUWA TEETH
USALAMA WA TAIFA TISS
MAMBO YA NNJE NA ULIKUWA UNAPELEKWA SOMALIA KAMA SLEEPER AGENT


AKILI ZAKO NDOGO NDO ZIKAKUGHARIMU



SASA HIVYI UTAKUTA UNALILIA UMASKINI
SHIT
 
WW ND ULIINGIA CHAKIKE WALE WAKIKUWA TEETH
USALAMA WA TAIFA TISS
MAMBO YA NNJE NA ULIKUWA UNAPELEKWA SOMALIA KAMA SLEEPER AGENT


AKILI ZAKO NDOGO NDO ZIKAKUGHARIMU



SASA HIVYI UTAKUTA UNALILIA UMASKINI
SHIT
TISS hawafanyi kazi zao kizembe ivyo
 
Mkuu hapa sijakufuata wewe halafu nipo kabla yako, kwanza member mwenyewe kwangu bado mchanga.

Na JF siyo ya babako. Kwenye jukwaa nilikuwepo kabla yako shahidi mamayako utanieleza Nini!!?
Unaendeleaje hapo sengerema?!
 
Back
Top Bottom