Nilidanganya kuwa mama amefariki ili nipate msaada, roho yangu inahuzunika sana

Pumbavu... unafkiri amekaa anawaza kukuandia wewe usome muda wote...bro tumia kichwa kikubwa kufikirika...unatumia Cha chini kufkiri ndo mana unaonekana zambwa
Yani utafikiri watu wanalipia vile,
Halafu wakiambiwa wahamie telegram, au wachangie wanaanza Shombo.
 
Anyway, sisemi story ni ya uongo. Wala sipo hapa kumpa changamoto Msimuliaji.

Lakini, hebu twende taratibu.. Umetoka dukani, kijana from nowhere akakupiga teke.. Ukampiga teke la kifua, akaanguka. Ukaokota jiwe unatoka kumpiga jiwe la kichwa!.. Ustadhi akatokea.

Mhmhhm!.. Tuendelee.
mkuu inawezekana mtaa niliokulia arusha ilikuwa ukiona mtu anainama kama anafunga kamba ya kiatu upigwa teke la kalio vibaya mno..
 
Sijui nikupe hongera au pole.

Nachagua kukupa hongera maana umeyashinda mengi ambayo yangekurudisha nyuma.

Kwenye kupambania maisha tunafanya mengi ya hatari na hilo lako la kumsingizia mama kifo likiwemo.

Hujawahi muacha mama mpweke na mengi umefanya kwa ajili yake.

Siku ukienda kumtembelea mwambie tu. Atakuangalia na atakuona ni mwanaume uliyekamilika na atakusamehe.

Utaishi kwa amani sana baada ya hapo.
 
Sijui nikupe hongera au pole.

Nachagua kukupa hongera maana umeyashinda mengi ambayo yangekurudisha nyuma.

Kwenye kupambania maisha tunafanya mengi ya hatari na hilo lako la kumsingizia mama kifo likiwemo.

Hujawahi muacha mama mpweke na mengi umefanya kwa ajili yake.

Siku ukienda kumtembelea mwambie tu. Atakuangalia na atakuona ni mwanaume uliyekamilika na atakusamehe.

Utaishi kwa amani sana baada ya hapo.
Well, shukran Sana mkuu. Nitajitoa ufahamu namchana live
 
Mkuu nimesoma hii hadithi nimekumbuka ile novel ya "Is it Possible?" Nadhani kwasababu umetaja Maasai na Arusha!

Ila all all Mungu Mkubwa! Naona mwanga mbele ya safari ya Maisha yako! Mungu akutangulie.!
nakitafuta sana hicho kitabu iwe soft copy au hard copy.kama unacho au unajua popote pa kukipata naomba msaada wako chief.
 
Nimepata kibarua/kazi mkuu.

Napiga usiku, mchana sometimes napiga/natafuta vibarua vya hapa na pale pia kama kuosha magari, pikipiki, saidia fundi n.k..

Naendelea kuufahamu mji kidogo kidogo.

Hicho ndicho ninachoweza kumshukuru MUNGU hadi sasa mkuu.

KARIBU MKUU, japo umetia kufuli chemba cha PiiEmu :D :D
Safi kbs..usome tu taratibu ..ntakuja jioni..acha nami nitafute
 
Tuendelee japo naona wengine wananitukana...


Kutokana na michango kuzidi shuleni na hakuna wa kutusaidia tukaamua twende kuomba msaada wa kusomeshwa na halmasauri. Likizo nzima tulikuwa tunaambiwa kila siku Njoo kesho, ikifika ijumaa tunaambiwa njooni j3. Umbali wa kutoka nyumbani Hadi halmasauri ni Kama 14km kwahiyo kwenda na kurudi ni 28km na tunaenda na kurudi kwa mguu. Hatimaye likizo ikaisha tunatakiwa kurudi shuleni na hatujapata msaada wa kusomeshwa, Jambo lililopelekea kaka yangu kukata tamaa ya kusoma na hakurudi shule tena.

Mimi niliendelea kuhudhuria pale halmasauri, kila siku nikiambiwa Njoo kesho nafika mapema. Kipindi Cha Kikwete ofisi za serikali zilikuwa hazijali watu kabisaa. Yaani unaingia ofisi ya umma asubuhi unamkuta mhusika anasoma gazette anakuambia yupo busy Njoo kesho. Kesho ukija unamkuta anacheza game kwa computer anakuambia Yuko busy na unaona kabisa anacheza game! Niliendelea kuhudhuria pale halmasauri bila kukata tamaa Hadi wakazoea kuniona pale.kumbuka likizo imeisha shule zimeshafunguliwa na nimeshapitiliza wiki moja.

Siku moja dada mmoja wa hapo ofisini akamuuliza bosi wake, kwanini huyu mtoto anakuja hapa kila siku, na Kama halmasauri hakuna fungu la kumsomesha ni kwanini unamuambia aje hapa kila siku?! Alimgombeza boss wake Hadi nikaogopa. Baadae akanitoa nje akaniuliza maswali machache; unaishi wapi? Shida yako Nini haswa, nikamwambia shida yangu nashindwa kuendelea na masomo kwasababu ya Ada. Akaniuliza nadaiwa shngapi jumla, Nilikuwa na report form inayoonyesha mchanganuo wa michango yote ninayodaiwa na nitakayodaiwa muhula ujao, pia Hilo fomu lilionyesha masomo na ufaulu wa mwanafuzi. Alishangaa kuona nimefaulu vizuri, nimeshika nafasi ya 2 Kati ya wanafunzi 208 darasani. Alirudi ndani ya ofisi akawaonyesha wenzake na kuwaambia japo kipato chake kidogo yeye hayuko tayari kuona mwanafuzi mwenye bidii darasani anaacha shule kwa sababu ya Ada. Alinirudia na kuniambia nirudi nyumbani nikajiandae na safari ya shule kisha baada ya siku tatu nipitie pale National House anapoishi, nikafanya hivyo.

Siku nilipoenda kwake nikakuta ameandaa bahasha yenye barua akaniambia niisome. Sikuamini macho yangu, Alimuandikia mkuu wa shule kumuomba (yeye dada) anilipie michango kwa installment. Nilipomaliza kuisoma, akaweka pesa ninazodaiwa muhula uliopita akafunga bahasha, akanipa Ela nyungine nikafanye shopping kisha nirudi pale kwake, nikafanya hivyo.

Huyo dada ni mtu wa Kanda ya ziwa na ni mmoja ya makabila wanaotuhumiwa kwa kuwa na dharau na kujisifu na hapo alikuwa anaishi na mume wake na walikuwa na mtoto mmoja,alikuwa mkarimu Sana na sikuona chechote Kati ya hizo sifa wanaotuhumiwa nazo. Kawaida tulikuwa tukitaka kusafiri tunalala kwenye basi ili asubuhi Tuendelee na safari, huyo dada akanizuia nisilale kwenye basi nilale kwake.mume wake pia ni mtumishi wa halmasauri Ila ni mtu wa tungi sana Hadi Leo.

Namna hiyo nilianza ukurasa mpya wa maisha ya shule. nilisoma kwa bidii hadi nikawa nawakimbiza class. Nilikuja kusikia kwamba mkuu wa shule anamshinikiza huyo dada aache kunisomesha kwani Hata yeye alijisomesha kwa kuuza maji hivyo vijana wa sikuizi tunadeka Sana na hatupo tayari kujitosa kikamilifu kwenye mapambano ya maisha. Japo yule dada hakuufanyia kazi ushauri wake niliumia Sana. Niliomba Mungu aingilie katika kwa sababu nimeshindwa kuelewa huyu mwalimu inamhusu Nini nikilipiwa Ada na mtu ambaye siyo ndugu yake Wala hajaombwa anichangie.

Ndugu msomaji unaposikia theory of "Karma", hii kitu ni kweli kabisaa. Usifanye jeuri au dhulma kwa kuwa unayemfanyia yeye hana uwezo wa kukufanya chechote. Huyo mtu, Hayati Magufuli alipoingia madarakani, aliwafukuza kazi wafanyakazi wenye vyeti feki nayeye alifukuzwa. Mwaka huo huo bomoa bomoa ilipitia maduka yake na rooms za kupangisha, alikuwa na magari mawili, moja likaibiwa na lingine likapata ajali Mbaya likaharibika Sana hadi amelipaki tu, mwaka mmoja baadae shamba lake ekari 150 likapimwa na kuonekana lipo kwenye Hifadhi ya nyuki, serikali ikamnyang'anya bila fidia kwani alikuwa anamiliki kiujanja ujanja, yaani ndani ya miaka mitatu akawa kapuku. Na watoto wake nao kila wakifika kidato cha nne wanapiga dundo wanamletea sifuri japo alijitahidi kuwapeleka tution za gharamana, wawili wengine wakamletea mimba. Mimi Niendelea na masomo Hadi nikamaliza kidato cha nne.


Nitakuja kuelezea nilivyonusuriaka kujiunga na ugaidi..... Samahani kwa uandishi mbaya Sisi Wamaasai kiswahili hutuchenga. Kuna watu humu wananifahamu na walinisapoti, story Kama huamini au haikupendezi siyo lazima utukane watu
Nilikuja kusikia kwamba mkuu wa shule anamshinikiza huyo dada aache kunisomesha kwani Hata yeye alijisomesha kwa kuuza maji hivyo vijana wa sikuizi tunadeka Sana na hatupo tayari kujitosa kikamilifu kwenye mapambano ya maisha.

Da
 
Nilikuja kusikia kwamba mkuu wa shule anamshinikiza huyo dada aache kunisomesha kwani Hata yeye alijisomesha kwa kuuza maji hivyo vijana wa sikuizi tunadeka Sana na hatupo tayari kujitosa kikamilifu kwenye mapambano ya maisha.

Da
Kuna watu wakaanga rungu si mchezo
 
Back
Top Bottom