Nilichoshuhudia ni unyanyasaji wa hali ya juu

Nilichoshuhudia ni unyanyasaji wa hali ya juu

Villanova tito

Senior Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
148
Reaction score
154
Kuna siku nilimsindikiza jamaa yangu fundi sofa set kwenda warehouse moja inajumlisha vitambaa vya sofa mtaa wa gerezani.

Nikaingia ndani nikakuta huyo mzee wa kichaga ameajili vijana zaidi ya kumi wa kike kama receptionist na wa kiume kama makuli, lakini nilichoshuhudia pale watu wanafanya kazi punda akasome kuna supervisor wa hapo ni mzee mchaga mlevi yaan mule ndanik yeye ndo anasauti yaan ukiingia asubuhi utatoka saa mbili usiku.

Hakuna mda wa kupumzika vijana wanabeba bundle nzito
Ujira kwa siku Tsh 5000-8000
Then wanafanyakazi wakiwa peku hawana gloves wala mask
Ukikutwa tu umesimama huna kazi, yaani unafanya kazi ngumu kwa matusi na kejeli
Wabongo acheni kunyanyasa wenzenu
 
Eeeheee... yaani umeshuhudia!!
Bora wewe wamesema la moyoni..
Maana humu tulizipa kusikia Wahindi wa waarabu na wa China.
 
Hujawahi kukaa na kundi la watu wengi unaowalipa kwa kutwa ukienda nao kisomi na kistarabu wanakuona wewe ni babu yao mazoea ya kijinga na kazi kuharibika.

Kujiajiri na kuajiri watu sio kazi nyepesi kazi za nguvu zinatumia mpaka bangi wewe utamwongoza mvuta bangi bila kuwa resi humuwezi ataishia kukupangia wewe kiongozi wake namna ya kufanya kazi. Theoretically wanaonewa ila practically hiyo ndo staili iwafaayo. Kuna majukumu ukipewa inabidi ujivike roho ya chuma, ubabe, ukauzu mpaka sauti yako ikisikika kimya kinatawala kwa sekunde kadhaa katika hilo eneo, kibarua anafikiria ukigundua tu kakudanganya kazi na malipo yaliobakia ndio basi tena.
 
Back
Top Bottom