Kumbe ni kweli bila siasa uwezi kutoka kimaisha mbona hawa walikimbilia siasa ile hali niwasomi wa juu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Prof Juma Kapuya alifundisha Botany pale mlimani, lakini kinachomtambulisha sasa ni ubunge wa Urambo Magharibi/Kaliua huko na uwaziri wa elimu, michezo, kazi,vijana, ulinzi nk.

Prof Philemon Sarungi alikuwa mzalendo wa kwanza kuwa bingwa wa fani ya mifupa, lakini hiyo haikumsaidia "kula nchi", badala yake "kilichomtoa" ni ubunge, uwaziri, ukuu wa mkoa, ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM.

Dr Mohamed Bilal ni mtaalam wa nuclear physics, lakini bado hakuonekana wa maana katika fani hiyo, hadi alipoingia siasa za ukatibu mkuu wakati huo Mkapa akiwa Waziri wa Elimu ya Juu,Sayansi na Technolojia,baadae uwaziri kiongozi, kugombea urais nk.Na sasa yeye na academics issues ndio basi tena

Dr Ali Mohamed Shein ni mwanasayansi mahiri tena katika fani yenye wataalamu wachache sana ya "molecular genetics", akiwa ameandika PhD thesis yake kuhusu "inborn errors of metabolism", lakini huko hakuona "utamu" hadi alipoingia kula nchi na wenye meno wengine kwenye siasa.Baada ya kifo cha Vice President Dr Omar Alli Juma,hakuwahi kugeuka nyuma.

Ukifanya "search" ya jina "Mark Mwandosya" kwenye google scholar utadondoshewa hints kibao za machapisho ya kisomi, na utashangaa kwa nini profesa kama huyu hakukaa chuo kikuu kufundisha na kuendeleza fani hiyo, badala yake yuko kwenye siasa!Kwanini hakutaka kurithisha maarifa haya na uweledi wake kwa vijana akazama kwenye siasa!?Jibu ni jepesi sana.....Maisha baada ya kustaafu!!Chapaaa!!

Wako wengine kibao kina Profesa David Mwakyusa,kina Dr Kadhege mzee wa LG100 wakaenda kuwa ma-DC huko Mbozi wakaacha taaluma zao kufundisha Udsm na wakawekwa kapu moja na kina Mulongo.Kuna kina Dr Kabwe S Kabwe,huyu ni daktari wa binadamu na Rais wa DARUSO-MUCHS(MUHAS siku hizi) enzi hizo.Kaacha taaluma yake na anakimbizana na vyeo vya kupewa,kajiweka kundi moja na kina Anthony Mtaka.

Gwiji wa Jiolojia Afrika,juzi tulivyopatwa na tetemeko Bukoba tukaambiwa moja ya changamoto ya GST sio mitambo tu,bali hata wataalamu wa fani hiyo,na kwa Tz wapo wawili tu level ya Phd..Mmoja ndio huyo Muhongo Sospeter,na yeye "kakimbilia" kwenye siasa na hataki tena kurudi kufundisha ili kuzalisha kina "Muhongo" wengine kwa vizazi vijavyo.Halafu unasema mtu azidi kusoma!!Usome nini wakati bongo siasa ndio kila kitu?

Mwingine alikuwa mwalimu wa Kemia.Alifundisha Organic Chemistry kwa madaha na staha.Akaongeza masters na baadae Phd.Kaukacha ualimu na hana mpango wa kurudi tena.Kazama kwenye siasa mpaka kufikia "cheo cha juu" ktk ulimwengu wa siasa.Ualimu umebaki kwenye vyeti na kumbukumbu tu.Anahimiza twende Isukamahela,Sikonge-Tabora kuongeza nguvu za walimu wa Sayansi shule za kata.Mhhhh...Nani aende na wao walikimbia?Vijana komaeni na siasa...Huko hakuna maisha.

Tujiulize, ni matatizo ya mfumo (hauwatunzi wataalamu wake) au ya elimu ya wataalamu hawa (wanashindwa kuitumia kuleta mabadiliko kwenye fani zao?) Maana kipimo cha kwanza cha elimu kuwa inafaa au la, ni jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko kwa msingi wa malengo ya elimu ile. Sasa hawa wasomi wetu ni kwamba elimu imewatupa au wao ndio wameitupa elimu?

Miaka kadhaa huko nyuma,Prof fulani maarufu Tz alistaafu kazi,baada ya kufundisha kwa zaidi ya miaka 30.Akitoa magwiji na wataalamu mbalimbali.Mafao yake hayakuzidi milioni 100.Huyu ni Phd holder,mtaalamu mbobezi...aliyetumia akili na koo lake miaka nenda rudi.. hicho ndicho kiasi alichofungshiwa kurudi nacho nyumbani.Wakati huku Bungeni Jah People na Maji marefu wanakunja 200 baada ya miaka mitano tu.Unakaa unajiuliza...Hivi inakuwaje mtu toka UN-Habitat anakuja kukaa kundi moja la Kibajaji wa Mtere?Jibu ni pesa...Pesa rahisi rahisi ipo huko.

Ooh vijana mjiajiri...Fursa zipo kila kona...Hizo fursa mbona nyie hamzitumii?Mbona nyie hamjiajiri?Kila siku kukimbizana na vyeo vya uteuzi kwenye bodi za mashirika ya umma na nafasi za kisiasa.Wacha tubanane huko huko...Siku elimu ikilipa watu watahamia huko.

Emeritus Prof...Walau unapata mkwanja hata baada ya kustaafu kwa serikali kuthamini mchango wako.Huku ni kapa bin kwapa.Ndio maana si ajabu kumkuta Prof mstaafu wa Udsm akila part time RUCO na Makumira ili kuganga njaa...Wacha tubanane humu humu
 
Wana taaluma vyuo vikuu wana maslahi mazuri ukilinganisha na watumishi wa kada nyingine nyingine . Mwalimu wa sekondari mwenye Bachelor degree take home yake haifikii nusu ya take home ya mwanataaluma chuo kikuu mwenye bachelor degree kama yeye.
 
Umegusa jambo muhimu sana hapo mkuu…. nchini kwetu utaalamu au usomi sio deal.
 
Wana taaluma vyuo vikuu wana maslahi mazuri ukilinganisha na watumishi wa kada nyingine nyingine . Mwalimu wa sekondari mwenye Bachelor degree take home yake haifikii nusu ya take home ya mwanataaluma chuo kikuu mwenye bachelor degree kama yeye.

Kwa hiyo...
 
Prof Juma Kapuya alifundisha Botany pale mlimani, lakini kinachomtambulisha sasa ni ubunge wa Urambo Magharibi/Kaliua huko na uwaziri wa elimu, michezo, kazi,vijana, ulinzi nk.

Prof Philemon Sarungi alikuwa mzalendo wa kwanza kuwa bingwa wa fani ya mifupa, lakini hiyo haikumsaidia "kula nchi", badala yake "kilichomtoa" ni ubunge, uwaziri, ukuu wa mkoa, ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM.

Dr Mohamed Bilal ni mtaalam wa nuclear physics, lakini bado hakuonekana wa maana katika fani hiyo, hadi alipoingia siasa za ukatibu mkuu wakati huo Mkapa akiwa Waziri wa Elimu ya Juu,Sayansi na Technolojia,baadae uwaziri kiongozi, kugombea urais nk.Na sasa yeye na academics issues ndio basi tena

Dr Ali Mohamed Shein ni mwanasayansi mahiri tena katika fani yenye wataalamu wachache sana ya "molecular genetics", akiwa ameandika PhD thesis yake kuhusu "inborn errors of metabolism", lakini huko hakuona "utamu" hadi alipoingia kula nchi na wenye meno wengine kwenye siasa.Baada ya kifo cha Vice President Dr Omar Alli Juma,hakuwahi kugeuka nyuma.

Ukifanya "search" ya jina "Mark Mwandosya" kwenye google scholar utadondoshewa hints kibao za machapisho ya kisomi, na utashangaa kwa nini profesa kama huyu hakukaa chuo kikuu kufundisha na kuendeleza fani hiyo, badala yake yuko kwenye siasa!Kwanini hakutaka kurithisha maarifa haya na uweledi wake kwa vijana akazama kwenye siasa!?Jibu ni jepesi sana.....Maisha baada ya kustaafu!!Chapaaa!!

Wako wengine kibao kina Profesa David Mwakyusa,kina Dr Kadhege mzee wa LG100 wakaenda kuwa ma-DC huko Mbozi wakaacha taaluma zao kufundisha Udsm na wakawekwa kapu moja na kina Mulongo.Kuna kina Dr Kabwe S Kabwe,huyu ni daktari wa binadamu na Rais wa DARUSO-MUCHS(MUHAS siku hizi) enzi hizo.Kaacha taaluma yake na anakimbizana na vyeo vya kupewa,kajiweka kundi moja na kina Anthony Mtaka.

Gwiji wa Jiolojia Afrika,juzi tulivyopatwa na tetemeko Bukoba tukaambiwa moja ya changamoto ya GST sio mitambo tu,bali hata wataalamu wa fani hiyo,na kwa Tz wapo wawili tu level ya Phd..Mmoja ndio huyo Muhongo Sospeter,na yeye "kakimbilia" kwenye siasa na hataki tena kurudi kufundisha ili kuzalisha kina "Muhongo" wengine kwa vizazi vijavyo.Halafu unasema mtu azidi kusoma!!Usome nini wakati bongo siasa ndio kila kitu?

Mwingine alikuwa mwalimu wa Kemia.Alifundisha Organic Chemistry kwa madaha na staha.Akaongeza masters na baadae Phd.Kaukacha ualimu na hana mpango wa kurudi tena.Kazama kwenye siasa mpaka kufikia "cheo cha juu" ktk ulimwengu wa siasa.Ualimu umebaki kwenye vyeti na kumbukumbu tu.Anahimiza twende Isukamahela,Sikonge-Tabora kuongeza nguvu za walimu wa Sayansi shule za kata.Mhhhh...Nani aende na wao walikimbia?Vijana komaeni na siasa...Huko hakuna maisha.

Tujiulize, ni matatizo ya mfumo (hauwatunzi wataalamu wake) au ya elimu ya wataalamu hawa (wanashindwa kuitumia kuleta mabadiliko kwenye fani zao?) Maana kipimo cha kwanza cha elimu kuwa inafaa au la, ni jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko kwa msingi wa malengo ya elimu ile. Sasa hawa wasomi wetu ni kwamba elimu imewatupa au wao ndio wameitupa elimu?

Miaka kadhaa huko nyuma,Prof fulani maarufu Tz alistaafu kazi,baada ya kufundisha kwa zaidi ya miaka 30.Akitoa magwiji na wataalamu mbalimbali.Mafao yake hayakuzidi milioni 100.Huyu ni Phd holder,mtaalamu mbobezi...aliyetumia akili na koo lake miaka nenda rudi.. hicho ndicho kiasi alichofungshiwa kurudi nacho nyumbani.Wakati huku Bungeni Jah People na Maji marefu wanakunja 200 baada ya miaka mitano tu.Unakaa unajiuliza...Hivi inakuwaje mtu toka UN-Habitat anakuja kukaa kundi moja la Kibajaji wa Mtere?Jibu ni pesa...Pesa rahisi rahisi ipo huko.

Ooh vijana mjiajiri...Fursa zipo kila kona...Hizo fursa mbona nyie hamzitumii?Mbona nyie hamjiajiri?Kila siku kukimbizana na vyeo vya uteuzi kwenye bodi za mashirika ya umma na nafasi za kisiasa.Wacha tubanane huko huko...Siku elimu ikilipa watu watahamia huko.

Emeritus Prof...Walau unapata mkwanja hata baada ya kustaafu kwa serikali kuthamini mchango wako.Huku ni kapa bin kwapa.Ndio maana si ajabu kumkuta Prof mstaafu wa Udsm akila part time RUCO na Makumira ili kuganga njaa...Wacha tubanane humu humu
Umefact mkuu.Hongera
 
aise naona bora nikaline shamba kuliko kupoteza muda kusoma nilipofika inatosha siasa sipendi so ngoja nikaanzishe McDonald ya Tz niajiri walalahoi wenzangu.
Ila mkuu hongera sana coz Nimegundua kitu hapo in bora tukaanzisha chuo cha siasa ili tuwe wakweli.
Unafki sipendi ndo maana sipendi ujinga
 
Mwanahabari Huru suala hili si kwa Tanzania tu bali Afrika nzima. Siasa ni kimbilio la wengi kuingiza hela za haraka haraka na huko ndipo wanakoenda kujiua kwa sababu wanatiliana unafiki sana na kutupiana ugoro wa Mze Akilimali, usipokuwa muangalifu unageuzwa msukule. That's why I never take wanasiasa seriously, licha ya uwongo wao pia ni washirikina mno na ni watu wasio na huruma na wenzao.
 
Nasikia huwezi kukalia kile kiti cha bunge, kama hujaaga kwenu vizuri.
 
Back
Top Bottom