Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

Leo nimeona maajabu, kituko, jambo la kusikitisha ambalo sikutegemea kuliona katika ofisi ya Serikali Kuu, ofisi ambayo ndio "ikulu" yetu ya Mwanza, ofisi ambayo inamwakilisha Rais.

Nimefika ofisi hiyo leo muda wa saa 5.00 asubuhi kufuatilia mambo fulani yanayohusiana na ofisi yangu ninapopatia riziki ya kila siku.

Nilipofika kwenye korido la jengo la zamani nikasikia sauti kubwa, sauti kali, matusi ya nguoni yakitokea ofisi ya masjala ya wazi/bayana (open registry), nikashuhudia watu wengi wamesimama kwenye korido hilo wanasikiliza matusi yale ambayo ama kwa hakika hayakuwa hata na "skin tight" yalikuwa makavu yakiporomoshwa kutokea ofisi hiyo ya Masjala kwa sauti kubwa.

Baadhi ya matusi hayo yalikuwa "MB.WA WEWE, MSEN.GE, YAANI WEWE NDIE UNANIFANYA NIITWE KWA MKUU WA MKOA," na matusi mengine mengi mengi machafu machafu.

Nikawapita watu waliokuwa wanasikilizia huo mziki wa matusi, nikaenda moja kwa moja hadi ofisi ya masjala kushuhudia kuna nini!!!

Oooooooooooooooops! nikakuta dada ambaye nimesikia wakimuita ASHA, ni Office Supervisor, anamtolea matusi hayo kaka ambaye ni mfungwa wa kifungo cha nje.

Mimi kama mtumishi wa umma, pia kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ya mwaka 2005, nilijisikia vibaya sana. Sikutarajia ofisi kubwa kama ile kukuta mtumishi anamtukana mwenzie matusi ya nguoni kwa sauti kubwa kama vile amapandisha mashetani!

Nikawauliza baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, huyu Asha anaumwa au ni tabia yake? wakasema Asha ndivyo alivyo na uongozi unajua tabia zake, lakini WANAOGOPA KULOGWA!

Sasa mimi siogopi kulogwa na huyo Asha wenu, nawaomba viongozi wa mkoa, kaka Mongela, Mtweve, Rubanzibwa fuatilieni utendaji wa huyo Asha hapo Masijala sio kwa matusi hayo!

Mwisho wanaJF msiponiona hapa JF kwa muda mrefu basi mjue labda Asha kaniloga nimekufa.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko
Labda ni Asha Boko alikuwa kwenye script/scene.
Au Asha Ngedere kwenye comedy.
 
huyo ingekuwa mimi anachezea kwanza vibao halafu mengine ndo yanafuata
 
huyo ingekuwa mimi anachezea kwanza vibao halafu mengine ndo yanafuata
Kosa la kupigana hadharani, halafu kumbuka aliyekuwa anatukanwa ni mfungwa ambaye anatumikia kifungo cha nje, hivyo angethubutu kujibu vibaya au kumpiga ina maaana angeeenda gerezani kabisa!
 
Wanasema Asha anaogopwa na staff wote, hahahhahaha, ni kama Fulani kembamba sana, vimishipa vimechomoza kila mahali. hahahahhahahah.
NIkauliza huyu Asha ni nani humu, wakasema ni office supervisor, amesoma Chuo cha Utumishi wa Umma ana Diploma ya Record Management. Jamani Asha ni hatari. shost usiponiona badi ujue Asha atakuwa kanidungua,hahahahahahah
bradha mshana jr yupo Asha atakua asha hawezi kukudungua mkuu
 
Back
Top Bottom