Nilichokiona NHIF

Nilichokiona NHIF

Amani iwe nawe pia.
Naomba nikupe ushauri kidogo kuhusu malalamiko yako maana mi ni mwanachama mwenzako ambaye bima ya afya umewahi kunisaidia sana.

1. Kila taasisi kuna utaratibu wa kupata huduma. Mwanachama wa bima ya afya anatakiwa afanye maombi ya vitambulisho anapoajiriwa tu au pale anapopewa taarifa na mwajiri wake kuwa michango yake imewasilishwa bima ya afya.....Lakini wengi hupuuzia na kuleta maombi ya kupewa vitambulisho vya dharura pale wabapougua.

2. Pamoja na wengi kupuuzia (1) vitambulisho vya muda hutolewa papo hapo kwa wanachama waajiriwa isipokuwa wale wa Kikoa, Toto Afya kadi na wanachama binafsi.

3. Kuhusu foleni kwenye ofis za bima hua inatokea haswa kwa ofis za dar es salaam but sijawahi kusubiri zaidi ya nusu kwa ajili ya kupewa huduma.

4 Hawa jamaa wa nayo number ya bure kwa wateja wao. Free call ambayo unapopata shida yoyote mahala popote kuhusu huduma za bima ya afya unapiga free of charge na kusaidiwa.
0800 11 0063

Nadhani wote kama tutafuata taratibu zilizopo lawama zitakuwa hakuna.
Wewe utakuwa unafanya kazi hapo mpaka unatetea ujinga, hiyo no. Haipokelewi utapiga mpaka ukome nilishapiga sana haikupokelewa, nikaenda ofisini nipo nahudumiwa nikamuuliza mbona simu yenu haipokelewi? Akaniambia nenda kaulize maulizo nikaenda kumuuliza kaniambia hiyo no inapigwa na watu wengi kwa hiyo kama una uwezo upige ya ttcl, kwanini wasiweke no. Za cm ya mkononi za kulipia tutumie mnaweka ttcl inakula hela nyingi, shida yangu ilikuwa kurenew card nimelipa hela naambiwa card kupewa mpaka miezi 6 nikauliza je ikitokea unaumwa kabla card haujapata unafanyaje? Kaniambia inabidi ulipie, maana yake nhif inafanya kazi miezi 6 tu na siyo mwaka kama wanavyojinasibu kwa sababu ili upate card nyingine ni mpaka miezi 6, jirekebisheni
 
Ni rahisi sana kuwaona wafanyakazi wa nhif wakorofi na ni vigumu sana kujua ukorofi wa wanachama. Ni kweli usiopingika kuwa binadamu hatujakamilika lkn wanachama wengi wana mitazamo hasi hivo moja kwa moja wanapo fika ktk ofisi zao za nhif wanafika wakiwa tayari wanamajibu kichwani na ndio maana anaambiwa kibali kitumike ndani ya siku saba yeye anajiongeza kwa kujiaminisha kuwa ameambiwa atapewa baada ya siku saba. Pia wakuu tuwe makini kwa vitu tunavyo vijadili. Kuna mkuu anamzungumzia meneja wa morogoro kuwa anawajibu wanachama vibaya. IMETUSIKITISHA SANA KAMA WAZAWA WA MKOA WA MOROGORO. Tukiwa kama wenyeji hatuna taarifa ya aina hiyo na meneja wa mkoa morogoro ni miongoni mwa watu wanao jali wanachama kuliko kitu kingine chochote na ni mtu asie penda makuu kwanza usipo tambulishwa huwezi mjua coz kazi yoyote huifanya coz kwa mara ya kwanza kumuona akitoa huduma sikuamini kama ndiye kwa jinsi alivo mkarimu na unyenyekevu kwa wateja wake.
Nawasilisha
 
Amani iwe nanyi,

Majuzi nikitembelMuhimbiliza bima ya Afya ya taifa, mambo niliyoyaona yalinifedhehesha mno:

1. Kwenye front desk kulikuwa na Afisa mmoja aliyekuwa akiwapokea wateja na kuwahudumia na ukumbi ulikuwa na watu wengi kiasi kwamba wale walioona kuwa wanachelewa kupata huduma walikuwa wakimkaripia.

2. Wateja waliokuwa wakiwasilisha form zao za kujiunga wanaambiwa wake kuchukua kadi zao baada ya mwezi mmoja, hii ilinistaajabisha ikafanya nijiulize, kwanini kadi ya utambulisho tu ichukue mwezi mmoja wakati taasis nyingine huweza kutoa ID siku hiyohiyo? MF. Backleys bank, kitambulisho cha mpiga kula nk.

3. Wateja waliokuja kuomba vibali vya matibabu kupewa kibali baada ya siku saba, hii ilinistaajabisha zaidi, kwanini vibali visitolewe siku hiyohiyo?

Nashauri mamlaka husika iige mfano wa bima nyingine za Afya mf, Jubilee amabo ukisha sajiliwa unapewa barua maalum ya utambulisho pending kusubiri ID.

Nawasilisha
Pole kwa yaliyokukuta au uliyoyashuhudia. mimi binafsi nina mgonjwa na nilikuwa muhimbili nikaandikiwa kwenda kuchukua kibali, kweli nilipata kibali ndani ya nusu saa. ukiwa na barua ni rahisi kupata kibali, sijui hilo tatizo lilitokea wapi na kwanini ila nina mashaka sana na hilo jibu namba 3.
Hata ukiwa mkoani majibu ya vibali ni siku hiyohiyo labda kuwe na changamoto ya kimawasiliano.
 
Wewe utakuwa unafanya kazi hapo mpaka unatetea ujinga, hiyo no. Haipokelewi utapiga mpaka ukome nilishapiga sana haikupokelewa, nikaenda ofisini nipo nahudumiwa nikamuuliza mbona simu yenu haipokelewi? Akaniambia nenda kaulize maulizo nikaenda kumuuliza kaniambia hiyo no inapigwa na watu wengi kwa hiyo kama una uwezo upige ya ttcl, kwanini wasiweke no. Za cm ya mkononi za kulipia tutumie mnaweka ttcl inakula hela nyingi, shida yangu ilikuwa kurenew card nimelipa hela naambiwa card kupewa mpaka miezi 6 nikauliza je ikitokea unaumwa kabla card haujapata unafanyaje? Kaniambia inabidi ulipie, maana yake nhif inafanya kazi miezi 6 tu na siyo mwaka kama wanavyojinasibu kwa sababu ili upate card nyingine ni mpaka miezi 6, jirekebisheni

Kufanya kazi bima ya afya siyo dhambi hata wewe kuna sehemu unafanya kazi na naamini siyo kila kitu mpo sawa mapungufu ya hapa na pale ni kawaida. Kwenye taasisi za umma unapokwenda inatokea hujaridhishwa na huduma pia jaribu kumwona msimamizi au meneja wa eneo husika. Mbona kwenye mabank japo hela ni zenu lakini hua mnaunga foleni bila malalamiko? Tuache kulalamika tufuate taratibu. ...Bima ya afya nawatetea kwa sababu wamejitahidi sana kuboresha huduma ukilinganisha na walipo toka
 
naona wengi mnaosapoti huu uzi si watumiaji wa NHIF, kwa mtazamo wangu kwenye swala la matibabu ndo bima ya uhakika kuliko zote, mimi nilishawahi kupoteza kadi yangu ya bima na nilikuwa nina appointment ya kumuona dokta siku inayofuata nikaenda kutoa ripoti na nikawambia nina appointment hospitali the next day, wakanipa kibali cha kutibiwa siku hiyo hiyo wakati nikiendelea kusubiri kadi itoke. Na kuna vipimo vingine lazma uende kwenye ofisi zao wakupe kibali, niliwahi kwenda na nikapewa kibali siku hiyo hiyo tena haikuchukua zaidi ya dakika tano. Tofauti na bima zingine mfano AAR au ile jubilee zina kiwango maalum cha kutuma kwa siku mfano jubilee sharti kwa siku usizidishe 150,0000 na unawekewe laki 5 sijui 6 tu kwa mwaka ikiisha kabla ya mwaka ndo imekula kwako, lakini NHIF ni unlimited. Nina kadi zote mbili NHIF ambayo ni ya ofisini kwangu na jubilee ambayo ni ofisini kwa mume wangu lakini huwa napenda kuitumia NHIF mana najua sitapata upungufu wa kuambiwa mara hela imezidi ngoja tuwapigie simu
 
Amani iwe nanyi,

Majuzi nikitembelea ofisi za bima ya Afya ya taifa, mambo niliyoyaona yalinifedhehesha mno:

1. Kwenye front desk kulikuwa na Afisa mmoja aliyekuwa akiwapokea wateja na kuwahudumia na ukumbi ulikuwa na watu wengi kiasi kwamba wale walioona kuwa wanachelewa kupata huduma walikuwa wakimkaripia.

2. Wateja waliokuwa wakiwasilisha form zao za kujiunga wanaambiwa wake kuchukua kadi zao baada ya mwezi mmoja, hii ilinistaajabisha ikafanya nijiulize, kwanini kadi ya utambulisho tu ichukue mwezi mmoja wakati taasis nyingine huweza kutoa ID siku hiyohiyo? MF. Backleys bank, kitambulisho cha mpiga kula nk.

3. Wateja waliokuja kuomba vibali vya matibabu kupewa kibali baada ya siku saba, hii ilinistaajabisha zaidi, kwanini vibali visitolewe siku hiyohiyo?

Nashauri mamlaka husika iige mfano wa bima nyingine za Afya mf, Jubilee amabo ukisha sajiliwa unapewa barua maalum ya utambulisho pending kusubiri ID.

Nawasilisha

More deadly, mimi nilijaza fomu ya uhakiki, ikiwa ni pamoja na kumwongeza mtoto wangu kama mtegemezi. Ajabu, tangu October tarehe 20 mpaka leo sijapata kadi ya mtoto wangu na fomu yangu haijahakikiwa. Jana nilienda nikaambiwa bado haijarudi niendelee kusubiri. Nilipigwa na butwaa, na mbaya zaidi hakuniambia nije tarehe ngapi.

Haya ni maajabu ya Tanzania.
 
naona wengi mnaosapoti huu uzi si watumiaji wa NHIF, kwa mtazamo wangu kwenye swala la matibabu ndo bima ya uhakika kuliko zote, mimi nilishawahi kupoteza kadi yangu ya bima na nilikuwa nina appointment ya kumuona dokta siku inayofuata nikaenda kutoa ripoti na nikawambia nina appointment hospitali the next day, wakanipa kibali cha kutibiwa siku hiyo hiyo wakati nikiendelea kusubiri kadi itoke. Na kuna vipimo vingine lazma uende kwenye ofisi zao wakupe kibali, niliwahi kwenda na nikapewa kibali siku hiyo hiyo tena haikuchukua zaidi ya dakika tano. Tofauti na bima zingine mfano AAR au ile jubilee zina kiwango maalum cha kutuma kwa siku mfano jubilee sharti kwa siku usizidishe 150,0000 na unawekewe laki 5 sijui 6 tu kwa mwaka ikiisha kabla ya mwaka ndo imekula kwako, lakini NHIF ni unlimited. Nina kadi zote mbili NHIF ambayo ni ya ofisini kwangu na jubilee ambayo ni ofisini kwa mume wangu lakini huwa napenda kuitumia NHIF mana najua sitapata upungufu wa kuambiwa mara hela imezidi ngoja tuwapigie simu

Usituletee ujinga wako, may be wewe ni bosi wa NHIF na hapa unajitapatapa kutetea ofisi yako, hamna lolote. Mimi ni mtumiaji na ninashuhudia upuuzi unaofanywa na NHIF.
 
Hakuna kitu hapo, ni uzushi mtupu. Kupata kadi ya mwanangu ilichukua miezi miwili, na hapo baada ya kupiga sana kelele.
Inawezekana tayari washakuwa Mufilisi, wanashindwa tu kusema ukweli.

Watakuwaje mufilisi wakati kila mwezi tunakatwa hela kwenye mishahara yetu? Unajua Tanzania tumefikia pabaya, tusipoamka tutaendelea kupigwa bao la kisigino. Iko siku watu tutakuwa na murder case, maana ujinga ukizidi mtu unaweza kufanya jambo lisilo la kawaida.
 
Watanzania tunakufa hovyo and we get frustrated because of bureaucracy. Pumbafu
 
3. Hujaelewa mkuu. Unapewa kibali ambacho kinakuwa valid for 7 days. Ulisikia vibaya mkuu. Ulienda ofisi za wapi??
Wengi tunapata huduma hapo si wabaya jamani mie nina mgonjwa alienda kupata kibali kuna nyaraka walitaka toka kwa mchangiaji walifanya jitihada binafsi mgonjwa akapata huduma.Hatuwezi kukataa kwenye taasisi kama ile hawakosi watu wabaya lakini mimi nakiri hawa watu wako vizuri. Swala la kusubiri huduma kama udhaifu upo wajirekebishe ni mambo madogo.Ukipata magonjwa makubwa ndio utajua thamani ya huu mfuko.
 
Usituletee ujinga wako, may be wewe ni bosi wa NHIF na hapa unajitapatapa kutetea ofisi yako, hamna lolote. Mimi ni mtumiaji na ninashuhudia upuuzi unaofanywa na NHIF.
Nimeongea kistaarabu sijamtukana mtu, sijaona sababu ya wewe kunitukana, kama una point ongea kiustaarabu FARU JOHN wee
 
More deadly, mimi nilijaza fomu ya uhakiki, ikiwa ni pamoja na kumwongeza mtoto wangu kama mtegemezi. Ajabu, tangu October tarehe 20 mpaka leo sijapata kadi ya mtoto wangu na fomu yangu haijahakikiwa. Jana nilienda nikaambiwa bado haijarudi niendelee kusubiri. Nilipigwa na butwaa, na mbaya zaidi hakuniambia nije tarehe ngapi.

Haya ni maajabu ya Tanzania.
Kunawatanzania hawataki kuona ukweli ndo maana tunaangamia na hatupati haki zetu
 
Kufanya kazi bima ya afya siyo dhambi hata wewe kuna sehemu unafanya kazi na naamini siyo kila kitu mpo sawa mapungufu ya hapa na pale ni kawaida. Kwenye taasisi za umma unapokwenda inatokea hujaridhishwa na huduma pia jaribu kumwona msimamizi au meneja wa eneo husika. Mbona kwenye mabank japo hela ni zenu lakini hua mnaunga foleni bila malalamiko? Tuache kulalamika tufuate taratibu. ...Bima ya afya nawatetea kwa sababu wamejitahidi sana kuboresha huduma ukilinganisha na walipo toka
Kusubiri card miezi 6 ndiyo wamejitahidi? Yaani card inaisha mwezi wa kwanza 2017 ili upate nyingine ni mpaka miezi 6 ipite, sasa hapa ni bora tu wakasema hiyo hela utatibiwa miezi 6 kuliko kudanganya mwaka mmoja
 
Huo ni uongo mimi nasoma chuo katoka kupata kadi yangu ya bima ya afya nililipia na niliisubiri kwa muda wa siku 21 na nikapata message niende nikachukue card yangu sasa wewe unayesema miezi sita sina uhakika kama una hata card ya bima ya afya ya nhif na kama unayo cyo wewe unaelipia umekatiwa na mtu na huyo mtu ndo aliyeifuatilia so itakuwa vigumu wwe kujua ilichukua muda gani kupatikana. So tujaribu kucomment vitu ambavyo tuna uhakika navyo jamani
 
Jambo hili la kulipia 20000tshs kwa lost ID linanikera sana yaani watu hawa ni watumwa waovu sana michango wanapokea alafu ukipoteza ID yako wao kupewa nyingine uilipie hii si sawa kabisa.
 
Kupoteza ni uzembe wako mwenyewe..lazima ulipie banaaa.
 
Kwa nini hukuuliza urudi baada ya muda gaji au uliamua kukaa kimya ili uweze kuoata la kulalamikia kumbuka anaofanya kazi ni binadamu na wanadamu cyo wakamilifu vp sasa kama alisahau huku wewe hujamuuliza huoni wewe una makosa
 
Ila mbona mimi niliwahi kuyaokoa maisha ya mzazi wangu kupitia bima ya afya tena katika hali ya dharura na nilipata kibali cha matibabu kwa haraka bila hata ya usumbufu ila mimi naona ni bora tungefanya uchunguzi kwanza juu ya ukweli wa habari hii jamani
Hii habari imeandaliwa ktk mazingira ya kulaumu na ndio hulka ya watanzania walio wengi. NHIF imenifaa sana wakati wa kumuuguza marehemu mzee wangu. Kibali kilikuwa kinatolewa siku hiyohiyo na si mara moja bali tumeomba mara nyingi sana na mara zote tulipata siku hiyo hiyo. Kusema kuwa kibali cha matibabu kinatolewa baada ya siku saba ni uongo ulio wazi!
 
Huo ni uongo mimi nasoma chuo katoka kupata kadi yangu ya bima ya afya nililipia na niliisubiri kwa muda wa siku 21 na nikapata message niende nikachukue card yangu sasa wewe unayesema miezi sita sina uhakika kama una hata card ya bima ya afya ya nhif na kama unayo cyo wewe unaelipia umekatiwa na mtu na huyo mtu ndo aliyeifuatilia so itakuwa vigumu wwe kujua ilichukua muda gani kupatikana. So tujaribu kucomment vitu ambavyo tuna uhakika navyo jamani
Mkuu katika kukaa kwangu JF nimejifunza mengi sana; mtu akiwa na chuki binafsi tu anaweza kuzusha uongo wa aina yoyote tu. Kama jamaa aliyesema kibali cha matibabu ni baada ya siku saba ni muongo kabisa! Tena muongo sana na huenda ni mfanyakazi wa makampuni binafsi ya bima kwa hiyo anayapa promo kwa kuichafua NHIF! Tuwe makini na watu wa aina hii
Suala la foleni ni kawaida kwa taasisi inayohudumia watu wengi. Hata mabenki ya kibiashara yenye ushindani mkubwa bado yana foleni. Jamaa kalileta hapa ktk namna ya kulaumu na sio kutatua tatizo.
 
Watakuwaje mufilisi wakati kila mwezi tunakatwa hela kwenye mishahara yetu? Unajua Tanzania tumefikia pabaya, tusipoamka tutaendelea kupigwa bao la kisigino. Iko siku watu tutakuwa na murder case, maana ujinga ukizidi mtu unaweza kufanya jambo lisilo la kawaida.
Kufilisika ni pamoja na kushindwa ku-meet your daily financial demands. Sasa kwa sababu umeshaaanza kuwa maskini unakuwa na vichelewesho vingi ili malipo ya mwaka jana uweze kuyafanya mwakani. Ndio kana NHIF wanavyofanya. If not, ni sababu gani inayowafanya wawe na poor performance kiasi hicho
 
Back
Top Bottom