Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,264
- 4,740
Amani iwe nanyi,
Majuzi nikitembelea ofisi za bima ya Afya ya taifa, mambo niliyoyaona yalinifedhehesha mno:
1. Kwenye front desk kulikuwa na Afisa mmoja aliyekuwa akiwapokea wateja na kuwahudumia na ukumbi ulikuwa na watu wengi kiasi kwamba wale walioona kuwa wanachelewa kupata huduma walikuwa wakimkaripia.
2. Wateja waliokuwa wakiwasilisha form zao za kujiunga wanaambiwa wake kuchukua kadi zao baada ya mwezi mmoja, hii ilinistaajabisha ikafanya nijiulize, kwanini kadi ya utambulisho tu ichukue mwezi mmoja wakati taasis nyingine huweza kutoa ID siku hiyohiyo? MF. Backleys bank, kitambulisho cha mpiga kula nk.
3. Wateja waliokuja kuomba vibali vya matibabu kupewa kibali baada ya siku saba, hii ilinistaajabisha zaidi, kwanini vibali visitolewe siku hiyohiyo?
Nashauri mamlaka husika iige mfano wa bima nyingine za Afya mf, Jubilee amabo ukisha sajiliwa unapewa barua maalum ya utambulisho pending kusubiri ID.
Nawasilisha